Wafanyakazi wa TAMWA leo tarehe 23/Juni /2016 wamepatiwa mafunzo mafupi  ya Jinsi  ‘kufuatilia miradi’, hususani mradi unaofadhiliwa na Legal Service Facility(LSF).

Mkufunzi  Dr.Patrick Mwakilama, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam(TUDARCO), ndiye aliyekuwa anatoa mafunzo hayo ambayo watekelezaji wa maradi huo kutoka TAMWA walihudhuria.

WAFUATILIAJI MRADI WA LSF TAMWA WANOLEWA

Chama cha wanahabari wanawake Tanzania – TAMWA kimefanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini kupanga mkakati utakaowezesha kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hapa nchini.

TAMWA YAFANYA MKUTANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUZUNGUMZIA UKATILI NA UNYANYASAJI KIJINSIA

Wabunge wa Bunge la Tanzania leo tarehe 26 Juni, 2016 wameunga mkono juhudi za TAMWA katika uhamasishaji umma kuhusu matatizo yaliyopo kwenye matumizi ya pombe kupita kiasi na madhara yake kiafya na kijamii. Hayo yamezungumzwa leo hii katika mkutano kati ya wabunge na waandishi wa habari kama ulivyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania –TAMWA. 

 

Mkutano huo uliochukua sura ya pekee, kwa kuwa na mada nne (4) zilizowasilishwa ikiwemo iliyohusu masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria za pombe zilizopo nchini, madhara ya pombe na ongezeko la magonjwa ya akili na madhara ya pombe na afya ya Jamii nchini.

 

Wabunge kwa umoja wao walikiri kuwa pamoja na changamoto zilizopo, na kusema kuwa nchini kwetu, pombe aina ya viroba imekuwa ni changamoto kubwa ambapo mbali na kuharibu akili za vijana pia vinachafua mazingira.

 

Aidha, Mwenyekiti wa vikao vya Bunge na Mbunge wa Ilala Mheshimiwa Zungu alikiri kuwa, pombe ni adui ambaye anatakiwa kudhibitiwa, na kufananisha hata uwepo wa majanga kama vile ndoa za umri mdogo kufananisha na maamuzi yanayo amuliwa kwenye vikao vya pombe.

 

Mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa Bunge, Msekwa D. mjini Dodoma, ulikutanisha  wajumbe wa kamati tatu ambazo ni Sheria ndogondogo, kamati ya Maendeleo ya Jamii Mipango na ile inayohusika na Serikali za Mtaa. Mkutano huu umefanikiwa kutokana na ufadhili wa IOGT-NTO Movement.

WABUNGE WAIPONGEZA TAMWA

Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania – TAMWA kimezindua mradi wa kutoa elemu ya usalama barabarani ili kuokoa vifo vya wanawake, watoto  na jamii kwa ujumla vinavyotokana na kutozingatia sheria za usalama barabarani.

TAMWA YAZINDUA MRADI WA USALA MA BARABARANI

Gari aina ya Land Cruiser Hardtop inauzwa kwa bei nzuri. Mawasiliano piga: 0222772681 au 0222771005 au 0754546387

GARI INAUZWA

FLAT YENYE VYUMBA VIWILI, SEBULE, MALIWATO NA JIKO INAPANGISHWA KWA BEI NAFUU. IPO KISUTU SOKONI. MAWASILIANO PIGA: 0222772681 AU 0222771005 AU 0754285701

FLAT INAPANGISHWA
Wanachama wa chama cha waandishi wa habari Tanzania TAMWA, leo wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa masuala ya wanawake na uchumi yatakayoendana na mabadiliko ya Tazania kutoka uchumi wa chini na kwenda uchumi wa kati na wa viwanda.
WANACHAMA WA TAMWA WAPATIWA MAFUNZO YA UANDISHI WA MASUALA YA WANAWAKE NA UCHUMI

Imetolewa Tar 4/8/2016.

Tumekusanyika hapa leo kuonyesha kushangazwa na kusikitika kwetu baada ya kuona taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa Serikali ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ili kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu.

TAMKO LA MTANDAO WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI TANZANIA KUHUSU NIA YA MWANASHERIA MKUU KUKATA RUFAA

Chama cha wanahabari wanawake Tanzania – TAMWA kimekutana na wanahabari kutoka mikoa ya kanda za ziwa ili kutoa mrejesho wa mafanikio na changamoto walizokutana nazo wanawake  kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

TAMWA YAKUTANA NA WANAHABARI KANDA YA ZIWA

Ukatili wa kijinsia ndani ya Wilaya ya Mvomero umepungua na unazidi kupungua siku hadi siku.

Hayo yamebanishwa na wanakamati wa GEWE walipotembelewa na maofisa kutoka TAMWA.

“Kwa kweli tunasema tena kwa kujiamini kuwa ukatili hapa kwetu mtibwa umepungua tena kwa kiasi kikubwa ukilingalisha na siku za nyuma, ila wanaofanya ukatili kwa sasa, wanafanya kwa kujificha chinichini maana wanaogopa kuwa tutawatumbua na kuwachukulia hatua”. Ni maneno ya mwanakamati Asha Shabani wakati akieleza mafanikio ya mradi wa GEWE.

Mafanikio haya ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa kina mama, watoto na hata kwa wanaume yamekuja baada ya TAMWA kufanya mafunzo mapema mwezi Aprili mwaka huu (2016), Mafunzo yaliyolenga kujenga, kuimarisha usawa wa kijinsia na kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini (GEWE II) kwa kamati zake na waandishi wa habari kuachilia mbali ambayo yalifanyika miaka ya nyuma.

Matokeo ya mradi wa GEWE yamezidi kuonekana na kuthibitika kwa wanakamati wa GEWE, wahanga wa ukatili na wananchi kwa ujumla kwani wamepata uwezo wa kuzungumza na vyombo vya habari bila kuwa na wasiwasi na kueleza matatizo na mafanikio wanayoyapata katika kutoa huduma kwa jamii na kuimarisha ushirikiano na waandishi wa habari.

Willy Mtembela, mmoja wa wajumbe wa kamati ya GEWE kata ya Mtibwa anasema kuwa, wao kama kamati wanajivunia kwa utendaji wao kwani wameweza kutoa elimu ya ukatili sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni ambapo walienda wakiwa wameambatana na waandishi wa habari na kutoa elimu ya jinsia na ukatili kwa watoto mashuleni ambapo waligundua mengi yanayowasibu watoto wakiwa katika mazingira ya shuleni, njiani na hata nyumbani.

GEWE II ni mradi unaotekelezwa na TAMWA na ulianzishwa kwa lengo la kujenga, kuimarisha usawa wa kijinsia, na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini katika wilaya 10 za Tanzania bara na visiwani

Jumla ya watoa habari 120, wasaidizi wa sheria 120 na waragibishi 120, polisi, viongozi wa dini, afya walipewa mafunzo jinsi ya kushughulikia ukatili wa kijinsia na wanaendelea na zoezi la kuratibu shughuli hizo katika ngazi za Vijiji hadi Kata.

GEWE KUTOKOMEZA KABISA UKATILI WA KIJNSIA

TGNP kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania (AATz),pamoja na mashirika yanayotetea haki za wanawake na watoto ambayo ni TAMWA, WiLDAF na TAWLA wameshiriki katika kufanikisha maadhimisho ya Tamasha la Jinsia la Wilaya pamoja na kusanyiko dogo la Kilimanjaro Initiative ambayo kwa pamoja yamefanyika kuanzia tarehe 8 hadi 10 Septemba 2016.

Maadhimisho haya yamefanyika katika Mkoa wa Morogoro wilaya ya Morogoro katika kata ya Mkambarani kwenye viwanja vya Moseka. Tamasha hili ni sehemu ya maandalizi ya kusanyiko kubwa la wanawake wa Afrika la haki ya umiliki ardhi, linalotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu.

Dhima kuu ya maadhimisho haya ni “Jinsia, Demokrasia na Maendeleo: Ardhi, Huduma bora za Jamii ni Haki Kwa maendeleo endelevu”. 2016 ukiwa ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa (FYDP) vyote vikiwa vimelenga kutokomeza umasikini na kupunguza mwanya kati ya walio nacho na wasio nacho, ni muda muafaka kwa mihimili yote ya serikali, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi kuhakikisha rasilimali za nchi hasa ardhi na huduma bora za jamii zinafikika kirahisi na kwa usawa kwa makundi yote hususan wanawake ambao ni wazalishaji wakubwa wa chakula nchini.

Malengo ya maadhimisho haya ni: kuimarisha, uwezo wa kuchambua, kutafiti na kutathimini masuala yahusuyo umiliki na usimamizi wa ardhi kwa wanawake, huduma za jamii; kupanua na kuimarisha ushirikiano katika vuguvugu la kuwakomboa wanawake na kuchangia katika mjadala wa utengenezaji wa tamko la kitaifa la madai ya wanawake ya ardhi ambayo yatakuwa ni sehemu ya tamko la kikanda la wanawake kuhusiana na masuala ya ardhi (Kilimanjaro Initiative). Maadhimisho yaliendeshwa pamoja na warsha na mijadala mbalimbali pamoja na tukio la upandaji wa mlima Uluguru kwa baadhi ya Wanawake ili kupaza sauti za wanawake juu ya madai ya haki ya umiliki na usimamizi wa ardhi kwa wanawake nchini Tanzania.  

Jinsia, Demokrasia na Maendeleo: Ardhi, Huduma bora za Jamii ni Haki Kwa maendeleo endelevu

Wanachama na wafanyakazi wa kituo cha usuluhishi ( CRC ) wamekutana pamoja leo tarehe 15.09.2106 katika ukumbi wa TAMWA uliopo Sinza mori Dar es salaam kujadili mpango kazi wa miaka 5 ambao unatarajia kuanza mwaka 2017-2021,CRC ni kutuo cha usuluhishi cha TAMWA ambacho kilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma ya ushauri unasihi na msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia .

Kituo kimefanikiwa kutoa huduma kwa wahanga takribani 70 kwa mwezi na kimeweza kujengea uwezo wasaidizi wa sheria 60 katika kata za Ruangwa mjini,Nachingwea( Ruangwa ),Luchingu ( Newala ), Makumbusho (Kinondoni),Nchinga ( Lindi Vijijini ). Aidha kimefanikiwa kutoa huduma kwa njia ya simu na mtandao kwa wahanga kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani.

WANACHAMA WA KITUO CHA USULUHISHI ( CRC  ) WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAZI WA MIAKA 5 UTAKAOANZA 2017-2021.

Chama cha wanahabari wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na waandishi kutoka mkoa wa Kilimanjaro walikutana kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa ushirikiano ulio thabiti katika mradi endelevu wa majaribio kwa wasaidizi wa kisheria na serikali za mitaa kulinda haki za wanawake kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia.

Mkutana huo uliofanyika tarehe 20 September, 2016 ulikutanisha wadau mbalimbali pamoja na wanahabari. Ambapo pia wanahabari wamewezeshwa kutoa taarifa ya kazi wanazofanya wasaidizi wa kisheria hususani katika kuelimisha jamii ili kupinga vita ukatili wa kijinsia kwa kupitia vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii.

Mmoja wa wanahabari wa Boma Hai FM, Omary Mlekwa pamoja na wanahabari wenzake walieleza na kutoa mifano ya kazi nzuri ambazo wasaidizi wa kisheria wanazifanya na zinaleta usawa katika jamii. Hii imejidhihirisha wazi kutokana na jinsi jamii sasa ilivyoelimika kwani aina yeyote ya ukatili imekuwa ikitolewa taarifa mapema. Hivyo basi, kupitia wao sifa nyingi zimesikika kwani wamekuwa ni watu wa karibu sana kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure.

Mradi huo unaoendeshwa na TAMWA kwa ushirikiano na Kilimanjaro Women Information Exchange and Consultancy Organisation (KWIECO) kwa ufadhiliwa wa Legal Service Facility (LSF) ambao TAMWA waliweza kukutana na wasaidizi wa kisheria mnao tarehe 23/9/2016 kutoka kata tano (5) za Ivaeny, Graragua, Sanya Juu, Biriri na Nasai. Kwa madhumuni ya kujadili changamoto kwa kutumia   mpango mkakati wa kihabari ulioandaliwa na wasaidizi wa kisheria. Mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Amani Centre uliopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na kufunguliwa na Afisa   mradi huo Bi Suzana Charles Mwaitenda . Sehemu kubwa ya mkutano ilikuwa ni ufuatiliaji wa mradi na kuhakikisha utekelezaji wa mradi shirikishi wa wasaidizi wa kisheria na serikali za mitaa katika   kulinda haki za wanawake unakuwa ni wa mafanikio.

TAMWA YAKUTANISHA   WANAHABARI WILAYANI SIHA MKOANI KILIMANJARO

Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa tarehe 11 Oktoba ya kila mwaka, wafanyakazi wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) wamevitembelea  baadhi ya vyombo vya habari nchini. Lengo kubwa likiwa ni kuwapongeza wanahabari kwa namna  wanavyoibua na kuandika habari za ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto pamoja na  kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto, jambo  ambalo limewafungua wananchi kuona ni hatua zipi za kuchukua pindi wanapoona vitendo hivyo katika jamii au familia vinatokea.

Mbali na pongezi, TAMWA wanavipongeza vyombo vya habari vyote nchini kutokana na kuweza kutoa nafasi kubwa kuchapisha habari za ukatili wa kijisia kwa wingi na hata kuzipa uzito wa kuzichapisha  katika kurasa  za mbele tofauti na miaka ya nyuma.

TAMWA KUTEMBELEA VYOMBO VYA HABARI

Mashirika yanayotetea haki za Wanawake nchini kwa kushirikiana na TGNP Mtandao wameandaa kongamano la wanawake barani Afrika litakaloanza tarehe 14-16 Octoba, 2016, kongamano hilo litafanyika Kilimanjaro na litahusisha wanawake wakulima wadogowadogo barani Afrika kutoka nchi takribani 20.

 

Kwa kutambua changamoto zinazoendelea kuwapata wanawake wa Afrika katika suala zima la upatikanaji, utumiaji na umiliki wa ardhi na rasilimali, aidha, mashirika ya ActionAid Tanzania, TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania (AATZ), International Land Coalition, Oxfam, Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) na Institute for poverty, land and Agrarian Studies (PLAAS) wamefadhili Kongamano  hilo la Ardhi kwa Wanawake wa Afrika, linalojulikana kama wazo la Kilimanjaro  (“Kilimanjaro Initiative”). Kwa kuzingatia kufanana kwa kiasi kikubwa kwa changamoto hizi katika ukanda wote wa Afrika.

 

Kongamano hili limelenga kuleta sauti za wanawake wa Afrika pamoja ili kuwakilisha maadhimio ya wanawake wa Afrika  kuhusu nini wanataka katika kutetea na kulinda haki ya ardhi na kuleta mabadiliko yenye kuchochea maendeleo ya wanawake wa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

 

Ardhi ni rasilimali muhimu na ni kichocheo kikuu katika maendeleo ya uchumi inayochangia takribani 10% ya pato la Taifa kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Sekta ya kilimo inaajiri zaidi ya 75% ya watanzania na kati yao zaidi ya  50% ni wanawake. Licha ya Sera ya Taifa ya Ardhi 1995 pamoja na Sheria za Ardhi Na.4 na Na.5 za mwaka 1999 kuweka usawa kati ya wanawake na wanaume  kumiliki ardhi, nafasi ya wanawake  katika kupata, kutumia, kudhibiti na kumiliki ardhi na rasilimali zingine bado hairidhishi.  Wakati huo huo, wanawake wanakadiriwa kuchangia asilimia 60 - 80% ya uzalishaji wa chakula, na ndio hasa wamekuwa wakilisha familia.

 

Inakadiriwa kwamba, tofauti ya usawa wa kijinsia katika kipato ni kubwa kati ya wanaume na wanawake kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha la Duniani, 2015, huku hali hiyo ikichangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa umaskini uliokithiri kwa wanawake.

KONGAMANO LA ARDHI LA WANAWAKE WA AFRIKA MLIMA KILIMANJARO

Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania -TAMWA kimeamua kuungana na Watanzania, Serikali na wadau wote katika kupambana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika, ili kuokoa vifo vya watanzania baada kuanza utekelezaji wa mradi wa usalama barabarani.

Mradi wa usalama barabarani una lengo kubwa la kuona  kwamba, wanahabari wanapata weledi wa kuandika habari hizi kwa mapana yake, lakini hasa kwa kuzingatia kuwa wanatoa elimu kwa jamii ya Tanzania kuhusu masuala ya usalama barabarani. Kwa kuanza TAMWA imeendesha mafunzo ya siku tatu kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa habari hizi. Awamu ya pili na tatu ya mafunzo itafuatia siku chache  zijazo.

TAMWA inaamini kuwa wananchi wengi watapokea elimu hii kwa kusoma habari katika magazeti, na kusikiliza Radio na hata kuona vipindi mara kwa mara kutoka kwenye televisheni.

MAFUNZO YA KWANZA KWA WANAHABARI –JINSI YA KUWA MAHIRI KATIKA KUANDAA NA KUANDIKA AU KUTANGAZA TAARIFA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA USALAMA BARARANI

Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewakutanisha wadau wa mradi wa Legal Services Facility (LSF) ambao ni waandishi wa habari, wasaidizi wa kisheria na wafanyabiashara wa masokoni kutoka katika masoko matatu ambayo ni soko la Ilala, Kiwalani na Buguruni mkoa wa Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa ufatiliaji wa mradi huo, ambapo wasaidizi wa kisheria na waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika kutoa elimu kupitia vyombo vya habari katika kushughulikia suala la wanawake kukosa fursa za uongozi masokoni na changamoto zingine amabazo wanakutana nazo masokoni. washiriki walijadili mafanikio, changamoto, na nini kifanyike katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa za uongozi katika masoko na kuhakikisha wanajengewa uwezo wa kupambana na changamoto zote wanazokutana nazo.

TAMWA YAKUTANISHA WADAU WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJARIBIO WA LSF (ILALA) AWAMU YA PILI

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzani - TAMWA leo kimeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.

 

Kauli mbiu ya mwaka huu, ya “Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia: Elimu Salama Kwa Wote”, inalenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa kwa kushirikiana na serikali kumlinda mtoto hasa wa kike katika kumhepusha na vizuizi ili aweze kufikia ndoto zake.

TAMWA YAUNGANA NA WADAU WA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

Wanasheria na Maafisa ustawi wa jamii wa Kituo cha usuluhishi TAMWA leo tarehe 7/12/2016 wametembelea kata ya Makumbusho maeneo ya Mwananyamala kwa Mwinjuma kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahitaji wa msaada huo . Ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .

Msaada huo ulitolewa kwa watu 15 kwa wakazi wa eneo hilo ambapo waliweza kusaidiwa. Mashauri mengi yaliyoletwa mbele ya Kituo cha usuluhishi TAMWA ni ya ndoa, matunzo, ardhi, mirathi na madai.

Msaada wa kisheria na ushauri nasihi uliambatana na utoaji wa elimu kwa wakazi wa Mwananyamala kuhusu sheria mbalimbali jinsi ya kutoa taarifa na wapi pa kupeleka taarifa wakiwa wanahitaji msaada wa kisheria.

Kituo cha usuluhishi bado wanaendelea kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi katika Ofisi zao zilizopo TAMWA – Sinza Mori.

TAMWA WAADHIMISHA SIKU YA MSAADA WA KISHERIA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA NA USHAURI NASIHI KATIKA KATA YA MAKUMBUSHO, WILAYA YA KINONDONI, DAR ES SALAAM

Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimeanza mkutano wake wa siku mbili kupanga mpango kazi wa mwaka 2017 ili kuhakikisha wanawafikia wanawake na watoto. Pia kujitathmini katika mafanikio na changamoto walizokutana nazo najinsi walivyozimaliza.

Mkutano unafanyika katika ukumbi wa mkutano kibaha (kibaha conference center) na umehudhuriwa na wafanyakazi wote wa chama hicho wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga.

TAMWA YAJIPANGA KWA MWAKA 2017

Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Equality For Growth (EFG), wamefanya mkutano na wasaidizi wa kisheria kuhitimisha mradi uliofanyika wilaya ya Ilala kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2017 Maeneo ya Buguruni Sokoni, Ilala sokoni na Kiwalani sokoni.

Lengo la kufanya mkutano huo ni kupata mrejesho wa utekelezaji wa mradi uliofanyika maeneo hayo ili kujua ni kwa kiwango gani kumefanikiwa katika kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake masokoni,kujua changamoto zake na nini kifanyike baada ya kumalizika kwa mradi huu. Wadau hao ambao ni wasaidizi wa kisheria , wahandishi wa habari na viongozi wa masokoni wametoa mirejesho wa utekelezaji wa mradi katika maeneo yao ambapo wameonyesha mafanikio makubwa ya kupungua kwa ukatili wa kijinsia masokoni, na elimu kwa jamii maeneo ya sokoni juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia.

Wadau wameonyesha mafanikio mengine makubwa katika kuleta usawa wa kijinsia masokoni kama vile mwongozo na katiba ambapo imetoa fursa ya uongozi kwa wanawake katika nyanja mbalimbali. Katiba hiyo imetoa nafasi nne (4) za upendeleo kwa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi, na pia imetoa fursa ya uongozi wa juu kwa wanawake mfano nafasi ya mwenyekiti ikichukuliwa na mwanaume basi nafasi ya makamu wa mwenyekiti lazima ichukuliwe na mwanamke. Katiba hizo zimetoa tamko la usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi.

TAMWA kwa kushirikiana na EFG wamewawezesha wanawake mbalimbali kiuchumi kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali na VICOBA ambapo wengi wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kiuchumi na wanaweza kijiendesha maisha yao na familia zao bila wasiwasi wowote. Wadau wameomba muendelezo wa mradi huu pamoja na ushirikiano ili tuweze kumkomboa mwanamke kiuchumi,kifikra na kutokomeza ukatili wa kijinsia masokoni.

TAMWA YAFANYA MKUTANO  NA WASAIDIZI WA KISHERIA KUHITIMISHA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI ULIOFANYIKA WILAYA YA ILALA  MAENEO YA BUGURUNISOKONI, ILALA SOKONI NA KIWALANI SOKONI

Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimezindua mradi mpya unaofadhiliwa na Sourthen African AIDS Trust (SAT) unaolenga kukomesha ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti katika wilaya ya Kinondoni na Temeke mkoani Dar es salaam.

Mradi huo umezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga katika Hoteli ya Elegancy iliyopo Sinza Mori Dar es salaam.

Mwezeshaji katika uzinduzi wa mradi huo ni Bi Valerie Msoka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika yanayopinga ndoa za utotoni(TECMN).

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo waalimu, wanafunzi, madakatari, mahakimu, pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Temeke.

Aidha kupitia mradi huo, TAMWA itatumia vyombo vya habari katika kutoa elimu ya masuala ya ubakaji na ulawiti kwa watoto ndani ya jamii kwa kushirikiana na kitengo chake cha usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinachotoa ushauri nasihi na msaada wa kisheria.

TAMWA YAZINDUA MRADI MPYA UNAOLENGA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UBAKAJI

WELCOME TO TAMWA WEBSITE

 The Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) is a non-profit sharing, non-governmental and non-partisan organisation registered under the Societies Ordinance on 17th of November 1987 with registration number SO 6763. The Association

Contemporary educational background approach does its best to engulf classmates in exploring concept, providing them with quite a few tasks to figure on as it may. Prerequisites for some types of educational paperwork boost routine buy essay Who knew essay article writing could well be so really difficult. To tell the truth, at basic tier, it has been hardly ever quite hard, but like we rise the academic concentrations it can get harder and tougher

in 2004 complied with the new NGO law of 2002. Tamwa has two offices in Dar -es- Salaam and Zanzibar. Zanzibar office located at Mombasa area near SOS is rented, but the office in Dar -es-Salaam situated at Sinza-Mori,  along Shekilango Road, Kijitonyama, Kinondoni District, is Association's property.

The founder members of TAMWA are; Fatma Alloo, Edda Sanga, Leila Sheikh, Rose Haji, Ananilea Nkya, Valerie Msoka, Pili Mtambalike, Elizabeth Marealle, Rose Kalemera,  Jamilla Chipo, Nellie Kidela and Halima Shariff.  Currently the Association has over 100 members with a minimum qualification of Diploma in Journalism and three years work experience in the media industry. Members are working in public and private media houses as editors, reporters, programme managers, producers, public relations and communication officers. The AGM is the supreme organ of the Association but it delegates its powers our to the GB which meets four times a year to evaluate the performance  of the Secretariat an organ to execute day today activities of the Association.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Visitors Counter

246905
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
2906
6055
15607
182281
129170
112735
246905

Your IP: 54.211.193.74
2017-02-21 10:03

Events - Calendar

February 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28

FOLLOW US ON FACEBOOK

Map

JoomShaper