PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (40)

Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania -TAMWA kinaungana na Watanzania katika maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambayo yataanza tarehe 26/09 na kufikia kilele tarehe 01/10. TAMWA inawaasa wadau wa usalama barabarani kuadhimisha wiki hii kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani hasa 'Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1972. Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi, ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto. Kutokana na idadi kubwa ya vifo na ajali  barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara. Kwa mujibu wa takwimu za kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani nchini, Muhammed Mpinga  zinasema kuanzia Januari hadi Julai,2016,  watu 1580 wamekufa kutokana na ajali barabarani, wengine 4659 walijeruhiwa katika ajali  5152 zilizotokea nchi nzima.  Waliokufa kutokana na ajali za pikipiki ni 430, waliojeruhiwa ni 1,147 katika ajali 1356.  Na takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) Watu milioni 1.25 hufariki kila mwaka Kwa ajali za barabarani.   TAMWA inatambua kwamba wanawake wengi na watoto ndio wenye kubeba mzigo mkubwa unaotokana na ajali barabarani, ingawa takwimu zinaonyesha kuwa  waathirika wa juu wa usalama barabarani ni wanaume. Ila ukweli ni kwamba wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi kwani watoto hukosa huduma na mahitaji  ya msingi baada ya kupoteza watu wanaowategemea. Edda Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaokufa katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii ". Kauli mbiu ya wiki ya usalama barabarani mwaka huu ni  "Hatutaki ajali barabarani - Tunataka kuishi salama”. Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji
Ndugu Wanahabari,  Taasisi zinazotetea haki za Wanawake na watoto nchini, tunalaani vikali ukatilii dhidi ya wanawake unaondelea kukithiri nchini.  Tukio la udhalilishaji wa Kijinsia kwa mwanamke mmoja lililotokea hivi karibuni katika mji mdogo wa Dakawa, wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, na kusambazwa kwa video ya udhalilishaji huo kwenye mitandao ya kijamii ni moja ya matukio ambayo hayapaswi kufumbiwa macho.  Huu ni udhalilishaji mkubwa na ukatili ambao amefanyiwa mwanamke huyu, na ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002) ambayo imeainisha makosa ya kujamiiana.  Pamoja na sheria za ndani, Serikali yetu imeridhia mikataba na matamko mengi kuhusu haki za wanawake na usawa wa kijinsia mfano mkataba wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW); pamoja na Mkataba wa haki za watoto (CRC), Tamko la Kimataifa la haki za binadamu (UDHR 19) ambalo linatambua haki za wanawake na watoto kama mojawapo ya haki za binadamu.
Chama cha Wanahabari Wanawake TAMWA, kimeandaa mafunzo ya siku mbili yatakayofanyika kuanzia leo tarehe 13 na 14 Aprili, 2016 yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari na kamati zinazoshughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia ili kuongeza uelewa wa kuvitolea taarifa vitendo hivyo.   Mafunzo hayo ya kamati na waadishi wa habari yatafanyika wilaya katika ya Mvomero mkoani Morogoro, wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, na wilaya Ruangwa mkoani Lindi zikiwa ni miongoni mwa wilaya 10 za Tanzania Bara na Visiwani, ambazo kwa kushirikiana na TAMWA zinatekeleza mradi wa Kujenga, Kuimarisha Usawa wa Kijinsia, na Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto hapa nchini (GEWE II).   Tangu mwaka 2012, TAMWA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto, kiliunda kamati za kushughulikia ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi ya vijiji hadi kata katika Wilaya 10 za Tanzania Bara na Visiwani.   Aidha, TAMWA katika utekelezaji wa mradi wa GEWE II kupitia Kamati za kushughulikia ukatili wa kijinsia, kwa kushirikiana na vyombo vya habari, watu wamekuwa wakivitolea taarifa vitendo hivyo, vikiandikwa na kutangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutoka asilimia 56.9 kwa mwaka 2012 kabla ya kuanza kwa mradi mpaka asilimia 69.2 mwaka 2014 baada ya utekelezaji wa mradi.   Jumla ya watoa habari 120, wasaidizi wa sheria 120 na waragibishi 120, polisi, Viongozi wa dini, afya walipewa mafunzo jinsi ya kushughulikia ukatili wa kijinsia na wanaendelea na zoezi la kuratibu shughuli hizo katika ngazi za vijiji hadi kata.   GEWE II ni Mradi unaotekelezwa na TAMWA ambao ulianzishwa kwa lengo la kujenga, kuimarisha usawa wa kijinsia, na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini katika wilaya kumi za Tanzania bara na Visiwani zikiwemo Wete (Pemba Kasikazini), Unguja Mjini Magharibi (Unguja Magharibi), Unguja Kusini, Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruangwa (Lindi), Kinondoni na Ilala Dar es Salaam       Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper