PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (41)

Uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Mwaka 2015 ulionyesha kuwa wanawake walikosa nafasi kwenye vyombo vya habari. Kutokana na ufuatiliaji wa habari za magazeti sita uliofanywa katikati ya Septemba na Oktoba mwaka jana, TAMWA iligundua kuwa; ni asilimia 11 tu ya wanawake ndio waliopata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa Uchaguzi mkuu. TAMWA imebaini kuwa kati ya vyanzo vya habari 2,577 vilivyotumika kwenye habari wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka jana, wanaume waliotumika kama vyanzo vya habari walikuwa 2,256 sawa na asilimia 88 ikilinganishwa na wanawake 303 tu ambao ni sawa na asilimia 11. Vyanzo vya habari ambavyo havikujilikana kuwa ni mwanaume au mwanamke vilikuwa 18 tu ambavyo ni sawa na asilimia 1.
   Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA  kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada hapa nchini,  leo Ijumaa tarehe 29 Januari, 2016 saa  08:00 asubuhi kitafanya mkutano wa siku moja kujadili yaliyojiri katika kongamano la nchi za Africa lenye lengo la mpango mkakati uliojadiliwa kwa ajili ya  kutokomeza mimba za utotoni lililofanyika hivi karibuni Desemba, 2015 Lusaka nchini Zambia.       Mkutano huo ambao utafanyika katika ofisi za TAMWA Sinza Mori, Dar es Salaam, utahusisha pia wadau mbalimbali  wanaopigania  haki za watoto, kujadili ufanisi na utekelezaji wa sheria zilizopo ili kuweka mpango mkakati wa kulaani ndoa za umri mdogo hapa Tanzania na jinsi ya kusonga mbele.

TAMWA YAPONGEZA UONGOZI WA AWAMU YA TANO

12 November 2015 Written by
Published in PRESS RELEASE
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinapongeza uongozi mpya ulioapishwa Novemba 5, 2015 chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper