PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (40)

Chama cha wanahabari wanawake tanzania -TAMWA kinaungana na watanzania katika maadhimisho ya nne ya umoja wa mataifa ya wiki ya usalama barabarani (UN Road Safety week) yatakayoadhimishwa kuanzia tarehe 08/05 na kufikia kilele tarehe 14/05. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “udhibiti wa mwendo kasi kwa vyombo vya vya usafiri”  TAMWA inawaasa wadau wa usalama barabarani wakiwemo Wabunge  kuadhimisha wiki hii kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani hasa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi,  ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto.  Kutokana na idadi kubwa ya vifo na ajali  barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara.  Wakati tunadhimisha wiki ya umoja wa mataifa ya Usalama Barabarani, tumeshuhudia matukio mbalimbali ya ajali ambayo chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Mfano wa tukio ni la tarehe 6 Mei, wiki iliyopita ambapo watanzania walipatwa na simanzi pale ambapo wanafunzi 32 na waalimu wao wawili pamoja dereva walivyopata ajali na kufariki papo kwa papo.  Madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ambapo inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.25 hufa kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.Wakati huo huo watu zaidi ya milioni 20 hadi 50 wamebaki na majeraha makubwa na aidha ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi kwa mwaka. Kwa mujibu ya repoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2015 ambapo jumla ya ajali 5,152 ziliripotiwa kwenye Jeshi la Polisi kuanzia Januari hadi Juni 2016. Pia takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani Nchini. Edda sanga, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii . Lakini pia kwa mda wa miaka mitatu iliyopita Nchi karibia 17 zinazowakilisha wananchi milioni 409 zimetunga na kufanyia maboresho ya sheria angalau kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndio vyanzo vikubwa vya ajali na Nchi hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika kudhibiti ajali, ila Tanzania haipo miongoni mwa nchi hizo. Ni mda mwafaka sasa Tanzania kuchua hatua kwa matendo”. Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini kinaungana na mashirika ya kihabari nchini kote kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ulimwenguni ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 3 Mei ambapo mwaka huu kitaifa yatafanyika mjini Mwanza. Maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu yake mwaka huu ni “Fikra Yakinifu kwa wakati Muhimu; Jukumu la Vyombo vya Habari katika kuendeleza Jamii zenye Amani, Haki Jumuishi” TAMWA imewataka wanahabari kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi hasa katika kuhakikisha wanazingatia usawa katika kutoa taarifa mbalimbali zikiwemo zile zinazohusu wanawake,watoto na wanaume. Aidha katika maadhimisho ya mwaka huu, TAMWA inawapongeza wanahabari na vyombo vya habari nchini kwa jinsi vinavyoshirikiana katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatolewa taarifa bila woga na wahusika wanachukuliwa hatua stahiki kwakua vitendo hivyo huchangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla. TAMWA katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto, kwa kipindi cha mwaka 2015 na 2016 wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2,350 na wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsi ya kuandika habari za ukatili wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali. TAMWA katika kutekeleza mradi wake wa GEWE II kimeweza kuhunda kamati za kuelimisha jamii jinsi ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya kumi za Tanzania na Bara na visiwani ambazo zinawahusisha wanahabari ili kuziwezesha jamii kushirikiana na vyombo vya habari kuweza kuvitolea taarifa vitendo hivyo bila woga ambapo kamati hizo zimesaidia kuibua matukio hayo. TAMWA inaamini kuwa kupitia maadhimisho haya wanahabari kote nchini watafanya kazi zao kwa weledi na uaminifu na kuandaa habari zenye usawa wa pande zote husika pamoja na kuibua mambo yanayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo ili yafanyiwe kazi pia kujihepusha na habari ambazo kwa sehemu zinaweza kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao wenyewe au wananchi katika taifa la Tanzania. Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji - TAMWA
Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kupiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe hasa zile zilizofungwa kwenye mifuko aina ya viroba ziambatane na uundwaji wa sera ya pombe ya Taifa itakayosaidia katika kudhibiti matumizi ya vilevi hapa nchini.   Sera ya hiyo  italazimisha sheria zinazoambatana  kurekebishwa ambapo pia zitawawezesha wafanyabiashara, watengenezaji na wauzaji wa kinywaji hicho kutambua haki, madhara na makosa yao mapema katika utoaji  huduma, na hiyo    itaisaidia serikali katika usimamizi madhubuti, na mwenendo wa udhibiti utakuwa wazi  tofauti na  sasa ambapo serikali imeamua kupiga marufuku kwa kushtukiza, jambo ambalo  limepelekea   kuleta madhara kwa wafanyabiashara ambao kwa namna moja au nyingine hawakuwa wanajua madhara yake.   Matumizi ya pombe aina ya viroba hayana budi kuwekewa sera, na sheria ziboreshwe hasa juu ya matumizi kwani yanachangia madhara makubwa ya kiafya kwa jamii  pamoja na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, migogoro majumbani, utelekezaji wa familia, ubakaji, ajali barabarani na pengine kuharibu nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla   Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA, kupitia kupitia kituo chake cha usuluhishi (CRC), kimekuwa kikiomba uwepo wa sera ya Taifa juu ya matumizi ya Pombe nchini kama ilivyo nchini Kenya na Uganda, aidha kimekuwa kikitoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya pombe kupita kiasi ambapo kwa mwaka 2016 kiliweza kuwapa ushauri nasihi wananchi wapatao 490, kati ya hao wanawake walikuwa 355, wanaume 92 na watoto walikuwa 45 walioathirika kwa namna mbalimbali kutokana na unywaji pombe kupindukia.     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper