PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (40)

Wadau wa Uchaguzi Mkuu 2015 mkoani Arusha wamevitaka vyombo vya habari kuripoti zaidi masuala ya watangaza nia au wagombea wanawake katika chaguzi zijazo nchini.  Wadau waliohudhuria warsha ya kujadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti habari za wanawake wakati wa uchaguzi mkuu 2015 iliyotolewa na TAMWA kwa msaada wa shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) walisema kuwa vyombo vingi vya habari vilishindwa kuripoti habari za watangaza nia ama wagombea wanawake kutokana na kujikita zaidi katika biashara, na hivyo kuripoti zaidi habari wanazoona zinauzika zaidi wakati wa uchaguzi.   Wadau pia walisema kuwa baadhi ya wanahabari walitaka kupewa malipo ya aina fulani kutoka kwa baadhi ya watangaza nia au wagombea wanawake ili kuripoti habari zao jambo ambalo watangaza nia au wagombea hao wanawake walishindwa kulitekeleza. Pia walisema kuwa watangaza nia au wagombea wengi wanawake hawakupata nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kutokana na kukosa maarifa ya kutosha ya jinsi ya kutumia vyombo vya habari.   Walipendekeza ili kuondokana na changamoto hizo katika siku zijazo, kunapaswa kutolewa mafunzo ya kutosha kwa Jukwaa la Wahariri (TEF), Wawakilishi wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (wanawake na wanaume) kutoka mikoa yote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Baraza la Habari Tanzania, Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania ili kuunga mkono watangaza nia au wagombea wanawake katika chaguzi zijazo. Pia walipendekeza kuendelea na warsha za pamoja kati ya vyombo vya habari na wanasiasa kujenga majukwaa ya kimtandao na kujenga mahusiano mazuri. Warsha ilifanyika Disemba 23 2016 na kuhudhuriwa na washiriki 28 (wanawake 17, wanaume 11) kutoka makundi ya waandishi wa habari, wahariri, waandishi wa blogu, watangaza nia, wagombea na viongozi wa kisiasa. Edda Sanga Executive Director
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika yanayotetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.   Kauli mbiu kitaifa mwaka huu ni “Tanzania ya Viwanda: Mwanamke ni Msingi wa Mabadiliko Kiuchumi” ambayo inatutaka wote tushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya mitazamo, fikra na matarajio ya kimaendeleo hasa kwa wanawake. Aidha kauli mbiu ya mwaka huu inatazamia serikali na wanasheria kuboresha sera na sheria ili ziweze kuleta uwezo wa ustawi na kuwawezesha wanawake wawe na uwezo wa kufikia mabadiliko yao ndani ya familia  na kuleta usawa katika maamuzi .   Inakadriwa kuwa duniani kote ni asilimia 50 tu ya wanawake ambao wanajishugulisha na kazi rasmi ikilinganishwa na asilimia 76 ya wanaume. Aidha kazi nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wanawake ni za hali ya chini na zinawaingizia kipato duni.   TAMWA inaamini kuwa azma ya nchi ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na viwanda  itafikiwa endapo haki ya elimu kwa mtoto wa kike itapewa kipaumbele na kuhakikisha sera na sheria kandamizi kwa wanawamke na watoto wa kike zitarekebishwa na kuwezesha ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na maamuzi.   Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yana lengo la kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda  na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.   Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2017, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.   Kauli mbiu mwaka huu ni “Ujenzi wa daraja shirikishi na imara kati ya Afrika na Dunia kuondoa ukeketaji ifikapo mwaka 2030” (“Building a solid and iteractive bridge between Africa and world to accelerate ending FGM by 2030) ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Kiafya wa demografia wa (TDHS-MIS) mwaka 2015-16, umeeleza kuwa mwanamke mmoja kati ya kumi amekeketwa licha ya elimu ya kuhusu madhara ya ukeketaji kuendelea kutolewa kwa jamii kila mara   Utafiti huo umebaini kuwa, uelewe kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka kutoka asilimia 71 ya wanawake hadi kufikia asilimia 97. Aidha, utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha wanawake wenye umri kati ya miaka 15-29 waliokeketwa kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwaka 2015.   TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapata elimu endelevu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake kwa kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.   Aidha TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ikiwemo vitendo vya ukeketaji na aina zote za ukatili wa kijinsia     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper