TAMWA YAFANYA MKUTANO NA WASAIDIZI WA KISHERIA KUHITIMISHA MRADI WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI ULIOFANYIKA WILAYA YA ILALA MAENEO YA BUGURUNISOKONI, ILALA SOKONI NA KIWALANI SOKONI

02 January 2017
Published in NEWS
Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Equality For Growth (EFG), wamefanya mkutano na wasaidizi wa kisheria kuhitimisha mradi uliofanyika wilaya ya Ilala kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2017 Maeneo ya Buguruni Sokoni, Ilala sokoni na Kiwalani sokoni. Lengo la kufanya mkutano huo ni kupata mrejesho wa utekelezaji wa mradi uliofanyika maeneo hayo ili kujua ni kwa kiwango gani kumefanikiwa katika kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake masokoni,kujua changamoto zake na nini kifanyike baada ya kumalizika kwa mradi huu. Wadau hao ambao ni wasaidizi wa kisheria , wahandishi wa habari na viongozi wa masokoni wametoa mirejesho wa utekelezaji wa mradi katika maeneo yao ambapo wameonyesha mafanikio makubwa ya kupungua kwa ukatili wa kijinsia masokoni, na elimu kwa jamii maeneo ya sokoni juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia. Wadau wameonyesha mafanikio mengine makubwa katika kuleta usawa wa kijinsia masokoni kama vile mwongozo na katiba ambapo imetoa fursa ya uongozi kwa wanawake katika nyanja mbalimbali. Katiba hiyo imetoa nafasi nne (4) za upendeleo kwa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi, na pia imetoa fursa ya uongozi wa juu kwa wanawake mfano nafasi ya mwenyekiti ikichukuliwa na mwanaume basi nafasi ya makamu wa mwenyekiti lazima ichukuliwe na mwanamke. Katiba hizo zimetoa tamko la usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi. TAMWA kwa kushirikiana na EFG wamewawezesha wanawake mbalimbali kiuchumi kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali na VICOBA ambapo wengi wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kiuchumi na wanaweza kijiendesha maisha yao na familia zao bila wasiwasi wowote. Wadau wameomba muendelezo wa mradi huu pamoja na ushirikiano ili tuweze kumkomboa mwanamke kiuchumi,kifikra na kutokomeza ukatili wa kijinsia masokoni.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper