TAMWA YAWA KUTANISHA WADAU WA USALAMA BARABARANI

23 February 2017
Published in NEWS
Chama cha Wanahabari Tanzania – TAMWA kimekutana na wadau mbalimbali wa usalama barabarani kujadili mambo mbalimbali yahusuyo usalama Barabarani hususani marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani. Mkusanyiko huo ulifanyika katika Ofisi za TAMWA zilizopo Sinza Mori – Dar es Salaam. Mkusanyiko huo wa wadau ulihusisha baadhi ya wabunge wa kamati ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya mambo ya ndani, wawakilishi wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani pamoja wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia. Washiriki walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na hali ilivyo sasa, ambapo ilielezwa kuwa hali ilivyo kulingana na takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.25 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 hadi 50 hujeruhiwa na wengine hupata ulemavu wa kudumu wengi wao wakiwa ni vijana wenye nguvu kazi ya Taifa. Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) 2015. Kwa upande waTanzania Bara, taarifa kutoka jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016 jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani. Katika vifo hivyo wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676. Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo idadi yake 3,649 ikifuatiwa na pikipiki kwa idadi ya 2,544. Maeneo ambayo yanapewa kipaumbele katika maboresho ya sheria ya Usalama barabarani ya 1973 ni: ulevi, mwendokasi, uvaaji kofia ngumu, vizuizi kwa watoto na ufungaji mikanda. TAMWA ina imani kwamba endapo maboresho ya Sheria mama ya usalama barabarani itafanyiwa marekebisho basi tutafanikiwa kutokomeza ajali zinazosababishwa na makosa ya kibinadamu nchini.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper