TAMWA YAKUTANISHA WAFANYAKAZI WAKE TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUBORESHA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA MRADI WAKE MPYA

09 August 2017
Published in NEWS
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), leo Tarehe 9 August, 2017 kimewakutanisha wafanyakazi wake kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika mkutano wa siku 3 unaofanyika katika hoteli ya Mbezi Garden jijini Dare s salaam.  Lengo kuu ni kushiriki pamoja katika kupitia na kuboresha mfumo wa ufatiliaji na tathmini ya programu yake mpya inayohusu utawala na haki za binadamu inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo wa DANIDA. Mradi huo unalenga kuwakinga wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuweka mfumo bora wa taarifa zinazohusu ukatili huo ili jamii ichukue hatua kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake. Mradi huo unatekelezwa katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar ambazo ni  Ilala, Kinondoni, Kisarawe, Mvomero, Ruangwa, Lindi Vijijini, Newala, Mjini Magharibi, Kusini Unguja and Wete Pemba. TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika mabadiliko ya jamii yanayoweza kusaidia kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper