TAMWA

TAMWA

UZINDUZI WA KITABU CHA MIAKA 30 YA TAMWA

19 November 2017
Dr.Harrison Mwakyembe akizindua Kitabu kinachoelezea Historia ya Miaka 30 ya TAMWA

UZINDUZI WA TAMWA ONLINE TV

19 November 2017
Dr.Harrison Mwakyembe akizindua TAMWA Online TV itayokuwa ikirusha kipindi cha Sauti ya Siti ambacho kinaakisi maisha halisi ya wanawake, watoto na makundi maalumu na changamoto wanazokutana nazo katika jamii

HAPPY 30th ANNIVESARY TAMWA

17 November 2017
Siku kama ya Leo Miaka 30 iliyopita, kilizaliwa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA). Katika kuazimisha siku hii, Leo tutakuwa na Tukio la KUCHANGIA Ujenzi wa Kituo cha Ushauri Nasihi, Saikolojia na Msaada wa Kisheria kuanzia SAA 12 Jioni hadi SAA 4 Usiku katika Ukumbi wa Kisenga LAPF International Conference Center (KLICC) ulipo Kijitonyama jengo la Millenium Tower.    Mgeni Rasmi ni Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.    Tafadhali Tuma Mchango wako:    TIGOPESA Malipo weka namba ya kampuni/kumbukumbu 606060    MPESA Malipo weka namba ya kampuni/kumbukumbu 370077    ***Mkono Ubebao Mwana ndio Uleao Taifa***
Ndugu Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini TAMWA, Mkurugenzi wa TAMWA, Board ya TAMWA Wanachama wa TAMWA Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali. Habari za asubuhi!   Nafurahi kuwepo na ninyi hapa leo katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TAMWA. Hongera sana Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA   Pia pokeni salamu nyingi kutoka kwa wafanyakazi wote wa ITV/Radio One !   Kwa ujasiri kabisa, Ningependa kueleza furaha yangu kwa kujumuika na nyinyi siku hii ya leo katika kuzindua wiki ya maadhimisho ya miaka 30 ya chama cha  TAMWA.   Ndugu Waandishi wa habari TAMWA ni chama maarufu kinachojulikana sana  hapaTanzania pamoja na nje ya nchi siyo tu kwa kuanzishwa miaka 30 iliyopita bali kwa uwezo na mafanikio yake katika utetezi na ushawishi  wa masuala yanayoendana na dhima yake. Inakumbukwa na wengi hadi leo jinsi chama cha  TAMWAkilivyosimama kidete mwaka 1998 kuwahamasisha waheshimiwa wabunge kule Dodoma katika kutunga sheria ya makosa ya kujamiiana na kule Zanzibar ambako pia kiliweza kulishawishi balaza la wawakilishi kuibadilisha sheria ya mwaka 1985 ambayo mtoto mwari akipata ujauzito alikuwa akifungwa miaka miwili. Hayo ni mafanikio makubwa katika upande wa ushawishi na utetezi.   Kwa muda wa miaka 30, TAMWA imejikita zaidi katika kutimiza dira yake ambayo ni Tanzania yenye amani inayoheshimu haki za binadamu kwa mtazamo wa kijinsia. Ili kufanikisha dira hiyo, shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa pande zote mbili – Tanzania Bara na Zanzibar. TAMWA imeiwezesha jamii mbali mbali hapa nchini kuongea kwa uwazi kuhusu ukatili wa kijinsia na vitendo hivyo kuvichukulia harua za kisheria pale inapotakikana. TAMWA imekuwa na ushirikiano wa kupigiwa mfano na vyombo vyote vya habari hapa nchini. Hayo yote myafanyayo yamo katika vipaumbele vya Serikali. Kwa hiyo, tunapenda TAMWA ifahamu kuwa jamii inathamini sana mchango wenu katika kujenga jamii huru na yenye kuthamini mchango wa wanawake katika  kufikia malengo ya mipango na mikakati ya serikali ya awamu ya tano chi ni ya Mheshimiwa  Rais Dr John Pombe Magufuli. Kwa namna ya pekee ITV na Radio One inatoa pongezi za dhati kwa juhudi za TAMWA kwa kuongeza usawa wa kijinsia hapa nchini. Halikadhalika ITV na Radio One itaendela kutoa ushirikiano na TAMWA katika kuelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kupiga vita aina zote za ukatili wa kijinsia. ITV na Radio One inatambua kwamba TAMWA ina dhamira ya  kujenga na kuendeleza kituo chake kwa lengo la kuongeza huduma za ushauri nasihi pamoja na msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Napenda kukuhakikishia ndugu Mkurugenzi wa TAMWA, kwamba sisi ITV/Radio One tupo pamoja nanyi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kutoa usaidizi ili kutimiza dhamira yenu njema na yenye faida kubwa kwa jami yetu. Ndugu washiriki wa maonesho haya, Fursa hii ya maonesho ni muhimu sana kwani inatuongezea uelewa na hata kutupa huduma mbalimbali bila ya gharama ikiwa ni pamoja ushauri nasihi, huduma za kisheria, huduma za afya na maarifa mbalimbali yatakayo fundishwa katika semina zilizo andaliwa ikiwa ni pamoja na masuala ya Ujasiriamali, Misingi ya uandishi wa habari na athari za ukatili wa kijinsia. Mwisho nawatakia maonesho mema na yenye tija kwa wote. Na kwa heshima kubwa Nazindua wiki ya Maadhimisho ya Miaka 30 ya TAMWA. 

WIKI YA MAONYESHO KUELEKEA MIAKA 30 YA TAMWA

14 November 2017
Baadhi ya kazi za mikono za wanawake wajasiriamali katika wiki ya MAONYESHO kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 30 ya TAMWA.

UZINDUZI WA WIKI YA MAONYESHO MIAKA 30 YA TAMWA

14 November 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Redio One, Bi Joyce Mhaville akizindua rasmi wiki ya maonyesho kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 30 ya TAMWA

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 30 YA TAMWA

09 November 2017
KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 30 YA TAMWA HUDUMA ZIFUATAZO ZITATOLEWA BURE: MSAADA WA KISHERIA,  USHAURI NASIHI,  HUDUMA ZA AFYA,  NA DAWATI LA JINSIA (POLICE DESK).   MAHALI:  SINZA MORI, OFISI ZA TAMWA. MUDA: TAREHE 14 HADI 16 NOVEMBA 2017 SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 12   WOTE MNAKARIBISHWA.
Wanaharakati wenzangu, karibuni TAMWA, mahali adhimu ambapo tumeamua kuzindulia maadhimisho ya miaka 30 ya Chama Cha Wandishi Wa Habari Wanawake Tanzania. Jina la TAMWA si geni masikioni mwa Watanzania walio wengi, ikizingatiwa hiki ni chama kikongwe cha wanahabari Tanzania ambacho mithili ya chombo baharini, kimehimili mawimbi, makubwa na madogo, mitikisiko na misukosuko ya hapa na pale, na bado kikaweza kuelea katika bahari tulivu. Itoshe kusema, tumetoka mbali. Mimi mbele yenu ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha TAMWA, kwa niaba ya wenzangu kumi na mmoja, tulio hai ni kumi, ambapo wawili wametangulia mbele za haki. Namshukuru Mungu ametujalia neema ya kuuona Mwaka uliotutunuku fursa ya kuanzisha Chama hiki, japokuwa tunazindua harakati za maadhimisho haya, tukiwa na takriban siku 78 kufikia kilele hapo tarehe 17 Novemba Mwaka huu. Tungependa ndugu zetu, marafiki zetu, wadau wetu, Watanzania wenzetu mmoja mmoja na katika ujumla wenu, muungane nasi kufurahia fursa hii ya kuadhimisha siku hii muhimu ambayo katika historia ya kuwepo kwetu, tunahesabu mafanikio lukuki tuliyoyapata. Moja ya mafanikio hayo ambayo ni vigumu kusahau ni ushawishi, kuzengea na kuzonga kuliko fanyika kwa ustadi mkubwa , tukiwa na wenzetu TGNP, TAWLA, MEWATA, WLAC, LHRC, CRC na mashirika mengine kama hamsini hivi tukitetea kubadilika kwa sera, na sheria kandamizi zinazomnyima haki mwanamke na mtoto, hasa mtoto wa kike. Furaha yetu ilikamilika , pale Mwaka 1998 tulipofanikiwa kuongea na wabunge, wakatuelewa na kuwazawadia Watanzania SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA , maarufu kama SOSPA. Utakumbuka pia sheria hii iliboreshwa Mwaka 2005 Uzuri wa sheria hii ya SOSPA, ni kwamba kwa mara ya kwanza, ilitamkwa wazi kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, ikampa mtoto wa kike ulinzi wa kutofanyiwa ukatili akiwa chini ya umri wa miaka 18. Huko Zanzibar, sheria ya spinster ambayo ilimtaka mtoto wa kike aliyepata mimba chini ya umri wa miaka 18 afukuzwe shule na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, wakati mwanaume aliachwa huru kutokana na kutokuwa na kifaa cha DNA, marekebisho yalifanyika katika sheria hiyo ambapo kifungo kwa mtoto wa kike kilifutwa na mwanamume aliyempa mimba anawajibika kutoa matunzo ya mtoto hadi atakapofika miaka 18. Januari 2008 ulizinduliwa mpango wa kuboresha hali za wanawake kiuchumi na kijamii uitwao WEZA, ambao ulitekelezwa na shirika la CARE TANZANIA, kwa kushirikiana na TAMWA ZBR. Mpango huu uliangalia shehia ya Unguja Kusini, na Kaskazini Pemba kwa kuhusisha makundi 300 ya wanawake 6,000 ambao waliunda vikundi vya kuweka na kukopeshana kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya uzalishaji mali na kuongeza kipato kwa ajili ya ustawi wa jamii. Azma hii ni katika kuhalalisha usemi maarufu kwamba ukimwezesha mwanamke, umeiwezesha jamii. Mafanikio zaidi ni pale kwa kushirikiana na wenzetu wanasheria, Mwaka 1999 sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji, iltoa fursa kwa wanawake kumiliki ardhi, na kwa mara ya kwanza, wanawake waliruhusiwa kushiriki katika kutoa suluhu ya migogoro ya ardhi. TAMWA, kwa ujasiri mkubwa, ilivunja ukimya wa mauaji ya vikongwe yaliyokuwa yakiendelea Shinyanga na kufanikiwa kufanya suala hilo liwe ajenda ya kitaifa. Aidha kwa kutumia vyombo vya habari tukishirikiana na mashirika mengine, tulifanikiwa kuongeza idadi ya wanawake bungeni kutoka asili mia 20 mwaka 2000 hadi 36 mwaka 2005 na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tulimpata spika wa bunge mwanamke, Mama ANNE Semamba Makinda ambaye ametuwakilisha vizuri hadi alipostaafu. Kama kuna kazi kubwa na ya kusifika imefanywa, na inaendelea kufanywa kwa ufadhili wa DANIDA toka mwaka 2012 ni katika GBV, ambapo TAMWA ikishiriana na CRC kituo cha usuluhishi na ushauri nasihi , na bila kusahau bang style ambayo kwa mfumo wake inafanana na kampeni. Mfumo huu tuliutumia sana TAMWA, ambapo vyombo vya habari vinatumika kwa wakati moja kuandikia na kutangaza suala moja kupitia angle tofauti tofauti kwa kipindi cha wiki, wakati mwingine hata zaidi. Huu ni mkakati tuliouibua wakati tunapanga mipango iliyotupatia ushindi wa SOSPA. Matokeo yake ni makubwa , HAYANA KIFANI. Kwa mtindo huo vile vile tumekemea na kuhamasisha jamii iachane na mila potofu, za kuwaoza kinguvu watoto wa kike katika umri mdogo kwa wanaume ambao wana umri mkubwa. Sifa nyingine kubwa kwa TAMWA, ni mafunzo ambayo tumeendesha kwa nyakati mbali mbali kwa wandishi wa habari ili waziandike kwa jicho la jinsia. Tumepinga ukatili dhidi ya watoto, tumehamasisha wazazi na walezi wawapeleke watoto wa kike shuleni ili wapate elimu, maarifa na ujuzi vitakavyosaidia kuwapa mawanda mapana ya fursa zilizopo ili wafaidi Maisha yaliyo bora kwa ajili yao na watoto wao. Hatimaye tumeelimisha, tumehamasisha na tutaendelea na harakati hizo tukiamini watoto wa kike na wakiume wakizifahamu haki zao za kijamii, kiafya na kiuchumi, wataweza kuzipigania na kuzitetea, na hivyo taifa letu kuondokana na umaskini ili maendeleo endelevu yatapatikane katika kipindi kifupi. Wanaharakati wenzangu, TAMWA toka mwanzo iliamini sana katika kufanya utafiti kabla ya kushughulikia tatizo lolote lile. Kwa mfano, tuliona wengi wetu tumejengwa kuimba nyimbo za kikoloni kama vile London bridge is falling down au where are you going my pretty maid. Huu ni utamaduni wa wenzetu ambao waliuingiza katika lugha yao. Baada ya kutafakari, tukaona haina mantiki sisi Watanzania na hasa watoto wetu kuendelea kuimba nyimbo zinazo upaisha utamaduni wa wenzetu wakati tuna nyimbo zetu nzuri zinazo akisi mandhari mazingira, hulka, malezi na mazoea yetu. Tunazielewa zinatuhusu na zina mantiki, nyimbo kama mabata madogo madogo yanaogelea katika shamba zuri la bustani, au maua mazuri yapendeza au kofia nyembamba nk .Tukamtafuta mwanamziki wetu , mdogo wake marehemu Patrick Balisidya ambaye alitutengenezea cassette nzima ya nyimbo za watoto ambazo tuliwapa RTD wakati huo wazitumie kuweka mahanjam katika vipindi vya watoto. Kwa Bahati mbaya cassette haipo lakini kitabu kipo. Vivyo hivyo, wakati huo, suala la madawa ya kulevya lilikuwapo japo si kwa ukubwa tunaoushuhudia leo. Tulifanya utafiti na kuangalia kiini chake, madhara yake na kuandika machapisho kadhaa kuihadharisha jamii kuingia katika angamizo la kizazi cha sasa na kijacho kama hatutafanya kazi ya ziada kuweka sheria kali dhidi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya. Waswahili wanasema mwanzo wa makubwa ni madogo na pia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha. Kwetu TAMWA tulikemea, Tuliandika sana na kufanya vipindi kadhaa redioni. TV wakati huo ilikuwa Znz tu. Baadhi ya machapisho hayo ni Sauti ya Siti, ambayo ni sauti ya wanawake. Tumekuza sana sauti za wanawake na watoto, kudai washirikishwe katika maendeleo ya nchi ili kero zao zitatuliwe na mchango wao uthaminiwe na kuheshimiwa, waweze kuishi Maisha yenye hadhi na yenye ustawi. Haya ni baadhi tu ya mengi yaliyofanywa na TAMWA. Wakati tunaendelea na harakati hizi, tukiwa na umri huu mkubwa wa miaka 30. tunawiwa kuchukua nafasi hii ya kipekee kabisa, kuwashukuru wote, hasa wandishi wa habari ambao mmetuwezesha kuwafikia watanzania kwa idadi kubwa kwa kipindi chote hiki. Kama usemi wa Misri unavyodhihiri wakati wakizungumzia umuhimu wa mto Nile kwa uhai wao, kwamba no Nile, no Egypt, na sisi TAMWA tunasema no media no TAMWA. Nadhani mnanielewa. Kupitia kwenu vyombo vya habari, uelewa wa jamii umeongezeka, utayari wao kukemea madhila haya tunauona, tunausikia na tunausoma. Kwa ushahidi zaidi tena wa kisayansi, TAMWA, inafanya kazi na inaendelea kufanya kazi katika wilaya kumi kwa ufadhili wa DANIDA unaoitwa GEWE I & 2 toka Mwaka 2012. Wilaya hizo ni WETE, (PEMBA KASKAZINI ) UNGUJA MJINI MAGHARIBI,UNGUJA KUSINI, KISARAWE,NEWALA MTWARA,MVOMERO MOROGORO,LINDI VIJIJINI,RUANGWA LINDI, KINONDONI NA ILALA DSM. Wakati mradi unaanza, uelewa wa watu katika wilaya hizo ulikuwa 11% , baada ya miaka 2, utafiti uliofanywa ulionyesha ongezeko la 4% hadi kufikia 16%. Kwa jicho la haraka haraka tunaweza kusema asili mi anne ni ndogo sana lakini ni kubwa kwa kipindi kifupi cha miaka miwili kwani kadri tunavyoendelea kuhamasisha na kuwapa uelewa na mbinu za kuchukua hatua, tutaona mabadiliko makubwa zaidi. Nini siri ya mafanikio yetu? Tunapenda pia kutamka wazi, kwamba kujitolea kwetu, nyakati zile kwa hali na mali, na ujasiri wetu kushughulikia masuala ambayo kijamii bado yalikuwa na hat leo tunaweza kusema yana ukakasi, kumetujengea uwezo wa kuendelea kutetea haki za wanawake na watoto katika mfumo wa kisayansi. Uwezo wa kuthubutu umekuwa nguzo madhubuti na yote tuliyofanya tuliyaamini na tulichukulia kazi hiyo kama wito kwa jamii. Sisi tumepata faida ya kuwa wandishi tuisaidie jamii kwa ujumla wake nayo ipaze sauti lakini zaidi tulilenga wale walio dhalili miongoni mwetu wakiwamo wanawake , walemavu na watoto.   HUKO TUENDAKO: Masuala ya unyanyasaji , ukatili wa kijinsia bado yapo, na naweza kusema ukatili umepitiliza kiwango cha ubinadamu. Hata ukatili kwa watoto unazidi. Hapa nazungumzia ubakaji ulawiti, utumikishaji watoto katika mashamba, majumbani , kwenye madanguro, ukatili wanaofanyiwa watoto mitaani majumbani mwetu na ndugu zetu, marafiki zetu, wageni wetu na majirani pia. Mengi ya matukio haya hayaripotiwi TAMWA inasikitishwa sana na jamii inayoishi karne ya 21 kukosa ujasiri wa kuripoti na zaidi kukosa uzalendo wa kutoa ushuhuda ili haki itendeke.Kama anavyosema Rais wetu Mh. Magufuli, rushwa inasababisha haki isitendeke na sote tunajua jinsi ambavyo baadhi ya wenye mamlaka wanavyopindisha sheria na kufanya mwenye haki aonekane mhalifu na mhalifu aonekane mwenye haki. Katika masuala ya ukatili na unyanyasaji rushwa imekithiri sana na ni kikwazo kikubwa sana katika kazi inayofanywa na TAMWA. Bila ushirikiano wa dhati kati ya familia zetu na vyombo vya dola, madaktari, walimu, majirani, madhehebu ya dini na serikali, matatizo haya ya kijamii hayawezi kuisha. Tutaendelea kujenga kizazi kiso maadili, kilichopondeka mioyo, kisichojiamini, kilichodhoofu kiafya, kiakili ambacho pia kitakuwa hakina mwelekeo. Kituo cha usuluhishi na ushauri nasihi hapa TAMWA, kina uwezo wa kuwahudumia waathirika wa matatizo hayo, lakini hatuna mahali stahiki pa faragha ambapo mteja anaweza kujieleza kwa uwazi na kwa kujiamini. TAMWA inataraji kuweka jitihada zaidi katika kuwasaidia vijana hasa katika kukabiliana na tatizo jipya la ukatili wa kijinsia utokanao na matumizi ya ya mitandao, yaani internet. Tunawasaidia vijana ili wawe na mtazamo chanya katika Maisha yao na vizazi vyao. Wawe na mbinu za kutambua kupambana na ukatili huu mpya unaoendelea kukua kwa nguvu na kusambaa kwa haraka katika jamii yetu. TAMWA, inataraji kuongeza mawasiliano ya karibu na vijana kupitia kurasa za face book, instagram twitter na kuboresha tovuti yetu ya www.tamwa.org ili iwe na taarifa nyingi zaidi za muhimu kwa jamii hasa kwa kizazi kipya cha .com. Kwa mantiki hiyo, lengo la mkutano huu, ni kuzindua harambee ya kuchangisha fedha ili tupate kituo cha kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia ikiwezekana nchi nzima. Aidha, tunaandaa kitabu kinacho akisi safari yetu ya miaka 30, yakiwemo mafanikio, matatizo, changamoto na mafunzo tuliyo pata katika kipindi chote hiki. Tuna mpango pia wa kutengeneza documentary ya kielectroniki itakayoelezea mengi zaidi kuhusu TAMWA. Tuna imani kubwa Watanzania watatuchangia kwa hali na mali , ili haya tuliyopanga kufanya, yawezekane. Tunaomba tuwe sote katika mwelekeo wetu wa kutetea haki za binaadamu, kapinga ukatili dhidi ya wanawake, walemavu na watoto, ili TANZANIA yetu iwe na amani endelevu. ASANTE SANA KWA KUSIKILIZA.   NJIA ZA KUCHANGIA: 1. KWA NJIA YA TIGO PESA: - Piga *150*01# OK Chagua Lipia Bili Ingiza Namba ya kampuni 606060 Weka Namba ya kumbukumbu 606060 Ingiza Kiasi kisha namba yako ya siri kukamilisha. Jina la kampuni ni TAMWA   2. KWA NJIA YA BENKI: Jina la Bank CRDB Account namba: 01J2027600600 Jina la Account: TAMWA   Kwa maelezo zaidi tupigie simu namba 0222772681 au 0222771005 TAMWA.
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) mwishoni mwa wiki kiliandaa mafunzi ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, mafunzo hayo yalijumuisha waandishi 23 kutoka wilaya ya kibaha, bagamoyo kisarawe na mkoa wa dare s salaama. Leongo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuweza kuandika na kuandaa habari za kuelimisha jamii kuhusu masuala ya usalama barabarani.
Page 1 of 17

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper