NEWS

NEWS (98)

Wanafunzi wa shule ya Kimataifa ya Dar es Salaam International Academy wametembelea Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa lengo la kujifunza umuhimu wa vyombo vya habari katika kutetea haki za wanawake na watoto katika jamii. Wanafunzi hao walipokelewa na Afisa wa kitengo cha jinsia TAMWA, Bi Godfrida Jola na kuwaeleza  maana halisi ya ukatili wa kijinsia pamoja na vitendo wanavyofanyiwa watoto na wanawake katika jamii vinavyokiuka haki zao za msingi na kupelekea ukatili wa kijinsia.   Pia walielezwa  ni kwa jinsi gani vyombo vya habari vinavyoweza kuwa chachu ya kumaliza ukatili wa kijinsia kupitia kalamu zao na vipindi vya  redio vya kuelimisha jamii. Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali na kujionea kazi  mbalimbali zinazofanywa na TAMWA katika kupambana na ukatili wa kijinsia unaoendelea katika jamii mbalimbali hapa nchini.

DANIDA NA TAMWA WASAINI MKATABA MPYA

19 April 2017 Written by
Published in NEWS
Balozi wa Dernmark (Bwana Einar Jensen) na Mkurugenzi wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania – TAMWA (Bibi Edda Sanga), wamesaini mkataba mpya wa miaka mitano (2017 – 2021) wenye lengo la kuihamasisha jamii kujenga na kuimarisha haki na usawa wa kijinsia ili kutokomeza ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini. TAMWA imekuwa ikitekeleza mradi huo kwa ufadhili wa DANIDA kuanzia tarehe 30 October 2012.

MKUTANO MKUU WA TAMWA 2016/17

31 March 2017 Written by
Published in NEWS
Wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kama ilivyo ada wamekutana kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka 2016/17. Mkutano huo umeanzaleo tarehe 31/03/2017 na utamalizika kesho Jumamosi tarehe 31/03/2017 katika Ofisi za TAMWA zilizopo Sinza Mori - Dar es Salaam. Mkutano huu wa siku mbili unawapa fursa Wanachama kujadili mafanikio yaliyopatikana, pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji. Mkutano mkuu wa TAMWA ndicho chombo cha juu chenye mamlaka na maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama.

TAMWA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI

24 March 2017 Written by
Published in NEWS
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimekutana na wahariri kutoka Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kujadili namna ya kuripoti habari zinazohusu masuala ya usalama barabarani. Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga , amewashukuru wahariri kwa ushirikiano mkubwa waliotoa wakati wa utekelezaji wa mradi wa Usalama Barabarani awamu ya kwanza ambao ulichukua miezi saba kukamilika. Pia aliwaomba kuanza kwa pamoja utekelezaji wa awamu nyingine ya mradi mpya ambao utahusisha mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam. Kwa kauli moja wahariri waliridhia kutoa ushirikiano wa dhati kwa kuandika na kurusha habari zenye kulenga kushawishi maboresho ya sheria ya sasa ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 na pia kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya sheria na kanuni za usalama barabarani.
Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kupitia kitengo chake cha usuluhishi na ushauri nasihi (Crisis Resolving Center – CRC), leo kimehudhuria na kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa watu waliohudhuria maazimisho ya siku ya ustawi wa jamii duniani. Maadhimisho hayo yameyofanyika  katika viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Akiongea katika maadhimisho hayo, Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangala, amesema kuwa ni wakati sasa kwa Wataalam wa ustawi wajamii kupitia wizara hiyo kuwa na sheria  ya kitaaluma ya ustawi, ambapo amemwagiza katibu mkuu wa wizara yake kuhakikisha mswada huo kufikishwa bungeni mwaka huu mwezi wa tisa ili upitishwe na kuwa sheria. Waziri Kigwangala amesema kwa sasa kumekua na mmomonyoko wa maadili, zikiwemo mimba za utotoni, utumiaji wa madawa ya kulevya, mapenzi ya jinsia moja, ubakaji pamoja na ulawiti. Aidha amewataka Maafisa ustawi wa jamii kuendelea kusimamia na kuelimisha Jamii kuhusiana na ongezeko la vitendo viofu katika jamii. Kauli mbiu ya siku hii ni, “USTAWI WA JAMII: KUKUZA NA KUIMARISHA JAMII NA MAZINGIRA”.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper