NEWS

NEWS (98)

TAMWA YAWA KUTANISHA WADAU WA USALAMA BARABARANI

23 February 2017 Written by
Published in NEWS
Chama cha Wanahabari Tanzania – TAMWA kimekutana na wadau mbalimbali wa usalama barabarani kujadili mambo mbalimbali yahusuyo usalama Barabarani hususani marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani. Mkusanyiko huo ulifanyika katika Ofisi za TAMWA zilizopo Sinza Mori – Dar es Salaam. Mkusanyiko huo wa wadau ulihusisha baadhi ya wabunge wa kamati ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya mambo ya ndani, wawakilishi wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani pamoja wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia. Washiriki walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na hali ilivyo sasa, ambapo ilielezwa kuwa hali ilivyo kulingana na takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.25 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 hadi 50 hujeruhiwa na wengine hupata ulemavu wa kudumu wengi wao wakiwa ni vijana wenye nguvu kazi ya Taifa. Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) 2015. Kwa upande waTanzania Bara, taarifa kutoka jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016 jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani. Katika vifo hivyo wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676. Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo idadi yake 3,649 ikifuatiwa na pikipiki kwa idadi ya 2,544. Maeneo ambayo yanapewa kipaumbele katika maboresho ya sheria ya Usalama barabarani ya 1973 ni: ulevi, mwendokasi, uvaaji kofia ngumu, vizuizi kwa watoto na ufungaji mikanda. TAMWA ina imani kwamba endapo maboresho ya Sheria mama ya usalama barabarani itafanyiwa marekebisho basi tutafanikiwa kutokomeza ajali zinazosababishwa na makosa ya kibinadamu nchini.
Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimezindua mradi mpya unaofadhiliwa na Sourthen African AIDS Trust (SAT) unaolenga kukomesha ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti katika wilaya ya Kinondoni na Temeke mkoani Dar es salaam. Mradi huo umezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga katika Hoteli ya Elegancy iliyopo Sinza Mori Dar es salaam. Mwezeshaji katika uzinduzi wa mradi huo ni Bi Valerie Msoka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika yanayopinga ndoa za utotoni(TECMN). Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo waalimu, wanafunzi, madakatari, mahakimu, pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Temeke. Aidha kupitia mradi huo, TAMWA itatumia vyombo vya habari katika kutoa elimu ya masuala ya ubakaji na ulawiti kwa watoto ndani ya jamii kwa kushirikiana na kitengo chake cha usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinachotoa ushauri nasihi na msaada wa kisheria.
Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Equality For Growth (EFG), wamefanya mkutano na wasaidizi wa kisheria kuhitimisha mradi uliofanyika wilaya ya Ilala kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2015 hadi 2017 Maeneo ya Buguruni Sokoni, Ilala sokoni na Kiwalani sokoni. Lengo la kufanya mkutano huo ni kupata mrejesho wa utekelezaji wa mradi uliofanyika maeneo hayo ili kujua ni kwa kiwango gani kumefanikiwa katika kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake masokoni,kujua changamoto zake na nini kifanyike baada ya kumalizika kwa mradi huu. Wadau hao ambao ni wasaidizi wa kisheria , wahandishi wa habari na viongozi wa masokoni wametoa mirejesho wa utekelezaji wa mradi katika maeneo yao ambapo wameonyesha mafanikio makubwa ya kupungua kwa ukatili wa kijinsia masokoni, na elimu kwa jamii maeneo ya sokoni juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia. Wadau wameonyesha mafanikio mengine makubwa katika kuleta usawa wa kijinsia masokoni kama vile mwongozo na katiba ambapo imetoa fursa ya uongozi kwa wanawake katika nyanja mbalimbali. Katiba hiyo imetoa nafasi nne (4) za upendeleo kwa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi, na pia imetoa fursa ya uongozi wa juu kwa wanawake mfano nafasi ya mwenyekiti ikichukuliwa na mwanaume basi nafasi ya makamu wa mwenyekiti lazima ichukuliwe na mwanamke. Katiba hizo zimetoa tamko la usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi. TAMWA kwa kushirikiana na EFG wamewawezesha wanawake mbalimbali kiuchumi kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali na VICOBA ambapo wengi wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kiuchumi na wanaweza kijiendesha maisha yao na familia zao bila wasiwasi wowote. Wadau wameomba muendelezo wa mradi huu pamoja na ushirikiano ili tuweze kumkomboa mwanamke kiuchumi,kifikra na kutokomeza ukatili wa kijinsia masokoni.

TAMWA YAJIPANGA KWA MWAKA 2017

15 December 2016 Written by
Published in NEWS
Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimeanza mkutano wake wa siku mbili kupanga mpango kazi wa mwaka 2017 ili kuhakikisha wanawafikia wanawake na watoto. Pia kujitathmini katika mafanikio na changamoto walizokutana nazo najinsi walivyozimaliza. Mkutano unafanyika katika ukumbi wa mkutano kibaha (kibaha conference center) na umehudhuriwa na wafanyakazi wote wa chama hicho wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga.
Wanasheria na Maafisa ustawi wa jamii wa Kituo cha usuluhishi TAMWA leo tarehe 7/12/2016 wametembelea kata ya Makumbusho maeneo ya Mwananyamala kwa Mwinjuma kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahitaji wa msaada huo . Ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia . Msaada huo ulitolewa kwa watu 15 kwa wakazi wa eneo hilo ambapo waliweza kusaidiwa. Mashauri mengi yaliyoletwa mbele ya Kituo cha usuluhishi TAMWA ni ya ndoa, matunzo, ardhi, mirathi na madai. Msaada wa kisheria na ushauri nasihi uliambatana na utoaji wa elimu kwa wakazi wa Mwananyamala kuhusu sheria mbalimbali jinsi ya kutoa taarifa na wapi pa kupeleka taarifa wakiwa wanahitaji msaada wa kisheria. Kituo cha usuluhishi bado wanaendelea kutoa msaada wa kisheria na ushauri nasihi katika Ofisi zao zilizopo TAMWA – Sinza Mori.

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper