NEWS

NEWS (98)

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzani - TAMWA leo kimeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hasa watoto wa kike.   Kauli mbiu ya mwaka huu, ya “Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia: Elimu Salama Kwa Wote”, inalenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa kwa kushirikiana na serikali kumlinda mtoto hasa wa kike katika kumhepusha na vizuizi ili aweze kufikia ndoto zake.
Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewakutanisha wadau wa mradi wa Legal Services Facility (LSF) ambao ni waandishi wa habari, wasaidizi wa kisheria na wafanyabiashara wa masokoni kutoka katika masoko matatu ambayo ni soko la Ilala, Kiwalani na Buguruni mkoa wa Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa ufatiliaji wa mradi huo, ambapo wasaidizi wa kisheria na waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika kutoa elimu kupitia vyombo vya habari katika kushughulikia suala la wanawake kukosa fursa za uongozi masokoni na changamoto zingine amabazo wanakutana nazo masokoni. washiriki walijadili mafanikio, changamoto, na nini kifanyike katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa za uongozi katika masoko na kuhakikisha wanajengewa uwezo wa kupambana na changamoto zote wanazokutana nazo.
Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania -TAMWA kimeamua kuungana na Watanzania, Serikali na wadau wote katika kupambana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika, ili kuokoa vifo vya watanzania baada kuanza utekelezaji wa mradi wa usalama barabarani. Mradi wa usalama barabarani una lengo kubwa la kuona  kwamba, wanahabari wanapata weledi wa kuandika habari hizi kwa mapana yake, lakini hasa kwa kuzingatia kuwa wanatoa elimu kwa jamii ya Tanzania kuhusu masuala ya usalama barabarani. Kwa kuanza TAMWA imeendesha mafunzo ya siku tatu kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa habari hizi. Awamu ya pili na tatu ya mafunzo itafuatia siku chache  zijazo. TAMWA inaamini kuwa wananchi wengi watapokea elimu hii kwa kusoma habari katika magazeti, na kusikiliza Radio na hata kuona vipindi mara kwa mara kutoka kwenye televisheni.
Mashirika yanayotetea haki za Wanawake nchini kwa kushirikiana na TGNP Mtandao wameandaa kongamano la wanawake barani Afrika litakaloanza tarehe 14-16 Octoba, 2016, kongamano hilo litafanyika Kilimanjaro na litahusisha wanawake wakulima wadogowadogo barani Afrika kutoka nchi takribani 20.   Kwa kutambua changamoto zinazoendelea kuwapata wanawake wa Afrika katika suala zima la upatikanaji, utumiaji na umiliki wa ardhi na rasilimali, aidha, mashirika ya ActionAid Tanzania, TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania (AATZ), International Land Coalition, Oxfam, Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) na Institute for poverty, land and Agrarian Studies (PLAAS) wamefadhili Kongamano  hilo la Ardhi kwa Wanawake wa Afrika, linalojulikana kama wazo la Kilimanjaro  (“Kilimanjaro Initiative”). Kwa kuzingatia kufanana kwa kiasi kikubwa kwa changamoto hizi katika ukanda wote wa Afrika.   Kongamano hili limelenga kuleta sauti za wanawake wa Afrika pamoja ili kuwakilisha maadhimio ya wanawake wa Afrika  kuhusu nini wanataka katika kutetea na kulinda haki ya ardhi na kuleta mabadiliko yenye kuchochea maendeleo ya wanawake wa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.   Ardhi ni rasilimali muhimu na ni kichocheo kikuu katika maendeleo ya uchumi inayochangia takribani 10% ya pato la Taifa kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Sekta ya kilimo inaajiri zaidi ya 75% ya watanzania na kati yao zaidi ya  50% ni wanawake. Licha ya Sera ya Taifa ya Ardhi 1995 pamoja na Sheria za Ardhi Na.4 na Na.5 za mwaka 1999 kuweka usawa kati ya wanawake na wanaume  kumiliki ardhi, nafasi ya wanawake  katika kupata, kutumia, kudhibiti na kumiliki ardhi na rasilimali zingine bado hairidhishi.  Wakati huo huo, wanawake wanakadiriwa kuchangia asilimia 60 - 80% ya uzalishaji wa chakula, na ndio hasa wamekuwa wakilisha familia.   Inakadiriwa kwamba, tofauti ya usawa wa kijinsia katika kipato ni kubwa kati ya wanaume na wanawake kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha la Duniani, 2015, huku hali hiyo ikichangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa umaskini uliokithiri kwa wanawake.

SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE

11 October 2016 Written by
Published in NEWS
Maadhimisho ya Kimataifa Siku ya Mtoto wa kike Duniani yalitangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2011. Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalifanyika Oktoba 2011, TAMWA inaupongeza Umoja wa Mataifa kuanzisha Siku hii muhimu ambayo imelenga kuikumbusha jamii juu ya malezi bora ya mtoto wa kike. Siku hii ya mtoto wa kike ni siku pekee ya kuikuimbusha jamii kuhusu haki za mtoto wa kike na pia kuwawezesha wasichana kutambua fursa zilipo mbele yao katika ujenzi ya jamii mpya enedelevu yenye kuleta usawa. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watoto wa kike wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali zikiwemo kukatishwa masomo, kuozeshwa kwa lazima, ubakaji, ukeketaji pamoja na kutelekezwa na kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zake. Kwa mujibu wa utafiti wa UNICEF uliofanyika 2009 unaonyesha kuwa, wasichana wanne kati ya kumi walifanyiwa ukatili wa kiji sia kabla ya kutimiza miaka 18. Aidha takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 61 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 ambao hawakusoma na asilimia 39 ya wanawake wenye umri kama huo wenye elimu ya msingi tu waliolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18 ukilinganisha na wanawake wenye umri kama huo ambao wana elimu ya sekondari au zaidi. Hali hii inafanya ndoa za utotoni kuwa ni sehemu ya ukatili kwa mtoto wa kike. Aidha katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto kike Duniani, TAMWA inaona kuwa kuna umuhimu wa kuziaangalia upya changamoto kisheria kwani zimekuwa kizingiti kwa mtoto wa kike katika kukuwa kwake, kutambua haki zake za msingi kama vile kupata elimu, malezi bora na mahitaji yote ya msingi, lakini pia kumuwezesha katika kujifunza namna ya kupambana na kila aina ya ukatikili anaokumbana nao ndani ya jamii. “Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni “mimba na ndoa za utotoni zinaepukika, chukua hatua kumlinda mtoto wa kike”

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper