NEWS

NEWS (98)

WABUNGE WAIPONGEZA TAMWA

26 June 2016 Written by
Published in NEWS
Wabunge wa Bunge la Tanzania leo tarehe 26 Juni, 2016 wameunga mkono juhudi za TAMWA katika uhamasishaji umma kuhusu matatizo yaliyopo kwenye matumizi ya pombe kupita kiasi na madhara yake kiafya na kijamii. Hayo yamezungumzwa leo hii katika mkutano kati ya wabunge na waandishi wa habari kama ulivyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania –TAMWA.    Mkutano huo uliochukua sura ya pekee, kwa kuwa na mada nne (4) zilizowasilishwa ikiwemo iliyohusu masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria za pombe zilizopo nchini, madhara ya pombe na ongezeko la magonjwa ya akili na madhara ya pombe na afya ya Jamii nchini.   Wabunge kwa umoja wao walikiri kuwa pamoja na changamoto zilizopo, na kusema kuwa nchini kwetu, pombe aina ya viroba imekuwa ni changamoto kubwa ambapo mbali na kuharibu akili za vijana pia vinachafua mazingira.   Aidha, Mwenyekiti wa vikao vya Bunge na Mbunge wa Ilala Mheshimiwa Zungu alikiri kuwa, pombe ni adui ambaye anatakiwa kudhibitiwa, na kufananisha hata uwepo wa majanga kama vile ndoa za umri mdogo kufananisha na maamuzi yanayo amuliwa kwenye vikao vya pombe.   Mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa Bunge, Msekwa D. mjini Dodoma, ulikutanisha  wajumbe wa kamati tatu ambazo ni Sheria ndogondogo, kamati ya Maendeleo ya Jamii Mipango na ile inayohusika na Serikali za Mtaa. Mkutano huu umefanikiwa kutokana na ufadhili wa IOGT-NTO Movement.
Chama cha wanahabari wanawake Tanzania – TAMWA kimefanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini kupanga mkakati utakaowezesha kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hapa nchini.

WAFUATILIAJI MRADI WA LSF TAMWA WANOLEWA

23 June 2016 Written by
Published in NEWS
Wafanyakazi wa TAMWA leo tarehe 23/Juni /2016 wamepatiwa mafunzo mafupi  ya Jinsi  ‘kufuatilia miradi’, hususani mradi unaofadhiliwa na Legal Service Facility(LSF). Mkufunzi  Dr.Patrick Mwakilama, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam(TUDARCO), ndiye aliyekuwa anatoa mafunzo hayo ambayo watekelezaji wa maradi huo kutoka TAMWA walihudhuria.
IKIWA ni mwakawa 25, Umoja wa Mataifa ulipopitisha azimio la kuwakumbuka watoto waliouawa kinyama na Serikali ya Makaburu ya nchi hiyotarehe 16 Juni, 1976 katikakitongoji cha Soweto kilichopoAfrikaKusini.Tanzania imekuwamiongoni mwa nchi zinazoadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, siku hii imekuayamanufaa kwa watoto na jamii ambapo elimu ya kujitambua na haki za msingi kwa watoto imefikika.   CHAMA cha wanahabariwanawake Tanzania (TAMWA), kinaungana na Dunia nzima kuadhimisha siku hii muhimu. TAMWA imeendesha kampeni ya siku kumi na sita inayoitwa #NAMPENDANITAMLINDA kuwahamisisha wazazi kuwapenda na kuwalinda watoto wao. Tunatoa wito kwa wananchi wote kuwalinda watoto kwani ni  Tunu ya Taifa, tuwalinde tuwathamini na kuwapenda watoto.   Pichani juu ni baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA wakiongozwana Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Mama Edda Sanga hukuwakiwa na jumbe mbalimbali katika maadhimisho yasiku ya mtotowa AFRIKA.

#NAMPENDANITAMLINDA COMPAIGN

14 June 2016 Written by
Published in NEWS
MARA nyingi wazazi tunakosa muda wa kukaa na watoto wetu na kuwaambia kuwa tunawapenda, kama nawe ni mmoja wao tumia fursa hii kumwambia mwanao, ‪#‎NAMPENDANITAMLINDA” una siku mbili tuu, hujachelewa. Ungana na watu mbalimbali kutoka barani Afrika na duniani kote kusherekea siku mtoto wa Afrika 2016 kwa kuonyesha upendo kwa watoto. ‪#‎Africanchildday2016 ‪#‎SikuyamtotowaAfrika2016 ‪#‎Childhood ‪#‎childrights ‪#‎teamchildren ‪#‎watototaifalakesho ‪#‎DANIDA ‪#‎TAMWA ‪#‎GEWE ‪#‎UNFPA

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper