PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (41)

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2017, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.   Kauli mbiu mwaka huu ni “Ujenzi wa daraja shirikishi na imara kati ya Afrika na Dunia kuondoa ukeketaji ifikapo mwaka 2030” (“Building a solid and iteractive bridge between Africa and world to accelerate ending FGM by 2030) ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Kiafya wa demografia wa (TDHS-MIS) mwaka 2015-16, umeeleza kuwa mwanamke mmoja kati ya kumi amekeketwa licha ya elimu ya kuhusu madhara ya ukeketaji kuendelea kutolewa kwa jamii kila mara   Utafiti huo umebaini kuwa, uelewe kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka kutoka asilimia 71 ya wanawake hadi kufikia asilimia 97. Aidha, utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha wanawake wenye umri kati ya miaka 15-29 waliokeketwa kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwaka 2015.   TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapata elimu endelevu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake kwa kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.   Aidha TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ikiwemo vitendo vya ukeketaji na aina zote za ukatili wa kijinsia     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji.
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania – TAMWA kimefanya tathmini kuchunguza matumizi ya pombe, madhara, upatikanaji wake pamoja na uelewa wa jamii za kata za Makumbusho, Saranga na Wazo Hill wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.   TAMWA kwa ufadhili wa (IOGT-NTO Movement) imetekeleza mradi wa kupinga ulevi wa pombe wa kupindukia katika kata 3 kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Kupitia utekelezaji wa mradi huo, TAMWA tumeweza kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kupitia elimu iliyokuwa ikitolewa kwa jamii kupitia vyombo vya habari mbalimbali, ushauri nasihi na msaada wa kisheria kwa waliofanyiwa vitendo vya kikatili kijinsia.   Jumla ya dodoso 458 zilifanikiwa kujibiwa katika tathmini hii. Matokeo ya jumla ya utafiti huu ambao ni wa mwisho wa mradi, yamebaini kuwa kuna upungufu wa matumizi ya pombe ikilinganishwa na ‘Tathmini ya Hali ya Matumizi ya Pombe (Alcohol Situation Analysis-ASA)’ ya mwaka 2014. Matokeo ya utafiti yameonyesha kuwa pombe ilinyweka kwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 28 kwa mwaka 2016. Aidha, tathmini imeonyesha kuwa asilimia 13 ya waliohojiwa kwa mwaka 2014 pamoja na 2016 walianza kunywa pombe wakiwa na umri wa miaka 14 na 17.Matokeo ya mwaka 2016 ni asilimia 14.   Hata hivyo asilimia 29 kwa mwaka 2014 na asilimia 22 kwa mwaka 2016 ya wanawake waliohojiwa katika dodoso,walikubali kufanyiwa vitendo vya ukatili na wanaume kutokana na matumizi ya pombe. Utafiti pia umeonyesha kuwa 20% na 23% kwa mwaka 2014 na mwaka 2016 ya vijana wenye umri chini ya miaka 25 walisema kuwa walifanyiwa ukatili na wanaume kutokana na matumizi ya pombe. Utafiti huo aidha, umeonyesha kuhusu uwepo wa uuzwaji pombe katika makazi ya watu kuwa umbali wa vilabu vya pombe ni chini ya meta 100 kutoka kwa kila aliyejibu dodoso la utafiti huu. Hali hii ilijidhihirisha kwa sababu 63% ya waliohojiwa kwa mwaka 2014 na 46% kwa mwaka 2016 walikubaliana kuwa vilabu vya pombe katika makazi vipo umbali wa meta 100.   Kwa ujumla tathmini hii imedhihirisha wazi kuwepo kwa matokeo chanya katika maeneo ya mradi. Kuna kila haja ya kuwepo kwa mwendelezo wa mradi wa elimu kama hii kwa jamii. Cha msingi tushirikiane,kwani kwa pamoja,TWAWEZA.
Matukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.   Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50 hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.   Takwimu pia zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwa sababu ya makosa ya kibinadamu hasa uzembe wa madereva kutokutii sheria na kanuni za barabarani, ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi nchini Tanzania, asilimia 76% ya ajali barabarani husababishwa na uzembe wa madereva, asilimia 8% husababishwa na ubovu wa barabara. Aidha ubovu wa vyombo vya moto husababisha ajali kwa asilimia 16%.   Hata hivyo ajali nyingi zinaepukika kama madereva na watumiaji wengine wa barabara watazitii sheria na kanuni za Usalama barabarani.   Kutokana na ajali hizo kuongezeka ndio maana ikatengwa siku maalum ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani kila mwaka ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Novemba ya kila mwaka.   Siku hii inatambulika kama siku rasmi ya kimataifa ya kuwakumbuka waathrika wa ajali hizo na familia zao na kuzitaka nchi wanachama pamoja na jumuiya za kimataifa kuitambua siku hiyo.   Pia siku hiyo hutoa fursa kwa jamii nzima kukutana na kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani ,kutafakari madhara, gharama, na hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kuzuia ajali zisitokee. Vilevile siku ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani inatoa nafasi kwa wadau kuikumbusha serikali wajibu wake na jamii nzima katika suala la kuzifanya barabara kuwa sehemu salama kwa kila mmoja.   Hivyo basi mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania kama ambavyo unaratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria (TAWLA) pamoja na mambo mengine katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo   Maeneo ndani ya sheria ambayo mtandao huu utajielekeza kuona sheria inafanyiwa mabadiliko/maboresho ni pamoja na;   a)      Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.   Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu. Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.     b)      Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemii chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho. Vilevile pamoja na kuanishisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutovaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa.   Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa na kwa usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.   c)      Matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.   d)     Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisiszokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.   Tunatoa wito kwa watunga sera kutaka kujihulisha zaidi na wadu kuuelimisha umma zaidi katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo.     Asanteni kwa kunisikiliza

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper