PRESS RELEASE

PRESS RELEASE (41)

Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kupiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe hasa zile zilizofungwa kwenye mifuko aina ya viroba ziambatane na uundwaji wa sera ya pombe ya Taifa itakayosaidia katika kudhibiti matumizi ya vilevi hapa nchini.   Sera ya hiyo  italazimisha sheria zinazoambatana  kurekebishwa ambapo pia zitawawezesha wafanyabiashara, watengenezaji na wauzaji wa kinywaji hicho kutambua haki, madhara na makosa yao mapema katika utoaji  huduma, na hiyo    itaisaidia serikali katika usimamizi madhubuti, na mwenendo wa udhibiti utakuwa wazi  tofauti na  sasa ambapo serikali imeamua kupiga marufuku kwa kushtukiza, jambo ambalo  limepelekea   kuleta madhara kwa wafanyabiashara ambao kwa namna moja au nyingine hawakuwa wanajua madhara yake.   Matumizi ya pombe aina ya viroba hayana budi kuwekewa sera, na sheria ziboreshwe hasa juu ya matumizi kwani yanachangia madhara makubwa ya kiafya kwa jamii  pamoja na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, migogoro majumbani, utelekezaji wa familia, ubakaji, ajali barabarani na pengine kuharibu nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla   Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA, kupitia kupitia kituo chake cha usuluhishi (CRC), kimekuwa kikiomba uwepo wa sera ya Taifa juu ya matumizi ya Pombe nchini kama ilivyo nchini Kenya na Uganda, aidha kimekuwa kikitoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya pombe kupita kiasi ambapo kwa mwaka 2016 kiliweza kuwapa ushauri nasihi wananchi wapatao 490, kati ya hao wanawake walikuwa 355, wanaume 92 na watoto walikuwa 45 walioathirika kwa namna mbalimbali kutokana na unywaji pombe kupindukia.     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji
Iringa Stakeholders of 2015 General Elections have said that media failed to report enough stories from women, youths and people living with disabilities during the 2015 general elections. They associated the less media coverage of these groups to several reasons include lack of confidence to deal with media, low skills on media engagement, stigmatization of PWDs and corruption in the election process which twisted media to cover some candidates from these groups in negative ways.   Aspirants/candidates from these groups were also lacking enough financial capacity to support election campaigns including engaging with the media.   They suggested that to address the challenges of women, youth and PWDs aspirants/candidates less media coverage in the future, TAMWA should continue to conduct trainings to marginalized groups before elections on how to use media for campaign.   TAMWA should also collaborate with government to provide civic education on the rights to vote and be voted. It should also work closely with journalists to remind them their professional ethics to avoid bribes and negative coverage of marginalized groups. The workshop held on 23rd December 2016 which brought 30 participants (16 female, 14 male) was attended by journalists, editors, bloggers, former candidates and elected leaders. Edda Sanga Executive Director TAMWA  
Wadau wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 mkoani Iringa wamesema kuwa vyombo vya habari vilishindwa kuripoti habari za kutosha kutoka makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015. Walihusisha suala hilo na sababu kadhaa ikiwemo watangaza nia au wagombea kutoka makundi hayo kushindwa kujiamini kuzungumza katika vyombo vya habari, kukosa maarifa ya kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya habari, unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu na rushwa katika mchakato mzima wa uchaguzi ambayo ilisababisha vyombo vya habari kuripoti taarifa hasi za watangaza nia au wagombea kutoka makundi hayo.   Watangaza nia au wagombea kutoka makundi maalum pia walikosa uwezo wa kifedha katika kampeni zao ikiwa ni pamoja na fedha za kutumika katika kujenga mahusiano na vyombo vya habari.   Walipendekeza kuwa ili kushughulikia changamoto hizo zinazowakabili wanawake, watu wenye ulemavu na vijana inabidi TAMWA kuendelea kutoa mafunzo ya watangaza nia au wagombea kutoka makundi maalum ya jinsi ya kutumia vyombo vya habari wakati wa uchaguzi. Wamependekeza pia TAMWA kushirikiana na serikali kutoa elimu ya mpiga kura ili wanajamii wafahamu haki zao za kupiga na kupigiwa kura. Pia wametaka TAMWA kufanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari ili kuwakumbusha maadili ya uandishi ili kuondokana na rushwa na kutoa taarifa hasi dhidi ya makundi maalum. Warsha iliyofanyika Disemba 23 2016 mjini Iringa ilihudhuriwa na washiriki 30 (wanawake 16, wanaume 14) kutoka makundi ya waandishi wa habari, wahariri, waandishi wa blogu, watangaza nia, wagombea na viongozi wa kisiasa kutoka mkoani Iringa kujadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti masuala ya wanawake wakati wa uchaguzi mkuu 2015. Edda Sanga Executive Director

OUR YOUTUBE VIDEOS

Events - Calendar

November 2017
Mon Tue Wed Thu Fri Sat Sun
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

FOLLOW US ON FACEBOOK

JoomShaper