News/Stories

TAMWA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUKEMEA AJALI ZA BARABARANI

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania – TAMWA, kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli kwa kuguswa na matukio ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikiathiri hali ya kijamii na kiuchumi nchini.

Takwimi za shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha Tanzania inapoteza 3.4 ya hali ya uzalishaji (GDP) katika kugharamia masuala yoyote yanayotokana na ajali za barabarani yakiwemo matibabu na madhara mengine kama kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na vifo vya wananchi. 

 

Kutokana na hali hiyo, TAMWA inampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kauli aliyoitoa hivi karibuni kutoa maagizo kwa vyombo vya usalama barabarani kufanya uchunguzi wa kina wa ajali iliyotokea katika mteremko wa Iwambi Mkoani Mbeya tarehe 01 Julai, 2018 na kusababisha vifo vya watu 20 na zaidi ya 40 kujeruhiwa ikiwa ni ajali ya tatu kutokea mkoani humo.

Aidha kitika kipindi cha mwezi mmoja tu, wananchi 40 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani mkoani Mbeya ambazo zinaweza kuzuilika. Takwimu kutoka Jeshi la Polisi nchini zinaonyesha kuwa asilimia 76 ya ajali zinasababishwa na makosa ya kibinadamu wakati asilimia 16 zinatokana na ubovu wa vyombo vya moto na asilimia 8 ni miundo mbinu mibovu.

TAMWA, zikiwemo taasisi za kiraia tunaona kuna haja ya kufanyia tena mapitio ya sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 kwani tafiti zinaonyesha kuna mapungufu kadhaa ambayo yanahitaji kuboreshwa yaendane na hali ya sasa ili iweze kukabiliana na changamoto za ajali za barabarani hapa nchini.

Maeneo yanayohitajika kufanyiwa maboresho ni pamoja na  Mwendokasi, matumizi ya mikanda, vizuizi vya watoto katika vyombo vya moto, uvaaji wa kofia ngumu na matumizi ya vilevi ambapo kwa hali ya ajali zilizotokea nchini hasa Mbeya katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, suala la miundo mbinu na tabia za madereva liangaliwe kwa jicho la pekee.

Takwimu za Kikosi cha Usalama Barabarani zinaonyesha kuwa mwaka 2013 vifo vitokanavyo na ajali za barabarani nchini Tanzania vilikuwa 4002, mwaka 2014 vilikuwa 3760, mwaka 2015 vifo vilikuwa 3468 na mwaka 2016 vilikuwa vifo 3256. Hata hivyo TAMWA tunaamini kuwa vifo hivi vinaweza kupungua kama si kuisha kabisa endapo kutawekwa sera na sheria kuboreshwa pia kama vyombo vya habari vitatumika ipasavyo kutoa elimu kwa wananchi kuzielewa

Kwa muda  wa miaka minne iliyopita nchi 17 zikiwemo za Afrika na kusini mwa Afrika zimetunga na kufanya maboresho ya sheria angalao kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndiyo vyanzo vikubwa vya ajali za barabarani na zimefanya vizuri katika kudhibiti ajali, miongoni mwa nchi hizo Tanzania haimo.

 

Mkurugenzi Mtendaji

Edda Sanga

Latest News and Stories

Search