News/Stories

UNFPA, EU KUZINDUA FILAMU YA UKEKETAJI TANZANIA

User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Tarehe 16 Julai, 2018,Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani   (UNFPA),lina Ujumbe Kutoka Jumuia ya Umoja Ulaya (EU) kwa Tanzania Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa  Ireland, Ubalozi wa Uholanzi, pamoja na ubalozi wa Kanada kwa pamoja watakuwa wenyeji wa shughuli ya kuonesha juhudi zinazohitajika katika kukomesha suala la ukeketaji hapa nchini.  Katika tukio hilo Kutakuwa na hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na Watoto. Pia kutakuwa  na Hotuba ya mwakilishi wa Jeshi la polisi Tanzania na wanaharakati wa haki za binaadamu pia kutakuwa na uzinduzi wa filamu mpya   yenye hadi ya kimataifa inayoitwa “In the Name of Your Daughter”,. Baadsa ya filamu hiyo kutakuwa na wasaa wa maswali na majibu kutoka kwa washiriki wa tukio hilo.

 

“In the Name of Your Daughter” ni filamu inayosimulia kuhusu msichana shujaa zaidi ulimwe    nguni. Watoto wa kaskazini mwa Tanzania wanajitoa muhanga na  wanakataa  kuchaguliwa maisha na na hivyo kuamua kufuata ndoto zao.  Baadi yao wakiwa na umri mdogo sana takribani miaka minane tu, watoto hawa huamua kuondoka katika familia zao kwa lengo la uepuka ukeketaji.               

 

Hili ni simulizi la Rhobi Samwelly, mwanamke jasiri kutoka wilayani Serengeti aliye jitolea kukomesha katika jamii yake.

Licha ya juhudi kubwa za Rhobi na wengine wengi, ukeketaji bado unaendelea kufanyika na hivyo kuonekana kwamba ni suala linalohitaji kutafutiwa ufumbuzi ikizingatiwa kwamba Tanzania imekwisha ridhia mikataba yam singi ya haki za binaadamu.

Tendo la ukeketaji ni hatari sana kwa maisha ya binadamu lakini bado linaonekana kama sehemu muhimu ya mila na utamaduni katika jamii nyingi. Cha kushangaza zaidi ni kuona ongezeko kubwa la vitendo vya ukeketaji hasa kwa watoto wadogo  walio chini ya umri wa mwaka mmoja.

 Katika tukio hilo kiongozi  wa ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya(EU) Balozi Roeland van de Geer, na Balozi wa Kanada Ian Myles, watatoa hotuba za ufunguzi. Pia kutakuwa na hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na Watoto,, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi  Mary Nzuki, pamoja na Mkuun wa polisi dawati la jinsia. Mwongozaji wa filamu ya  "In the Name of Your Daughter", Giselle Portenier, atapata fursa ya kuitambulisha filamu na kisha atapokea na kujibu maswalli akishirikiana na mwanaharakati wa haki za binaadamu Rhobi Samwelly na nyota wa filamu hiyo. Makamu wa Muwakilishi wa UNFPA, Dr Hashina Begum, atapata fursa ya kutoa hotuba ya kufunga shughuli kwa kutoa  tafakari fupi kuhusu jitihada za kutokomeza ukeketaji.

 

Waandaaji wa shughuli hii wana shukurani za pekee kwa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kuwaalika waandishi wa habari kushiriki katika tukio hili muhimu.


Utangulizi

Hali ya Ukeketaji nchini Tanzania

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimejizatiti kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2030 katika malengo yake ya  maendeleo endelevu.

Malengo ya Dunia ya mwaka 2030 yanaweka bayana nia yake ya kutokomeza ukatili wa aina zote wa wanawake na watoto na badala yake kuongeza jitihada na kuwekeza zaidi katika ulinzi na usalama na uwezeshwaji wa wanawake na watoto.  Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (NPA-VAWC) wa 2017/2018-2021/2022 unauelezea ukeketaji kama utamaduni wenye madhara makubwa kwa wanawake na watoto.

Katika mwaka 1998, Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili piga marufuku  ukeketaji. Tangia wakati huo, ukeketaji ulipungua  kutoka asilimia  18 mwaka  1996 hadi alisilimia  15 mwaka  2010 kisha hadi asilimia  10 mwaka 2016.

Mafanikio katika kutokomeza ukeketaji ni ya dhahiri; Kuna ongezeko la wasichana wanao tumia njia mbadala za kimila zenye lengo na madhumuni ya kuwaandaa kuwa wanawake bila kufanyiwa ukeketaji. Kuna matukio zaidi ya ukeketsaji  yanayo ripotiwa na kufanyiwa uchunguzi na jeshi la polisi kutokana na ongezeko la uelewa na mafunzo thabiti kwa askari wa jeshi la polisi kuhusu suala zinma la ukeketaji na hivyo kuwajengea uwezo katika  kudhibiti mila hii yenye athari kwa kiasi kikubwa.

Mnamo Juni 2018 taarifa za kidunia kutoka  UNFPA, zinaonesha kwamba, ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani linaathiri maendeleo yaliyofikiwa na idadi ya wasichana waliohatarini inaongezeka maradufu.  Licha ya  kupungua kwa matukio ya aukeketaji bado juhudi zilizopo dhidi ya mila hii zinahitaji uungwaji zaidi ili kuiondoa kabisa mila hii.

Tatizo la ukeketaji halimaliziki na wala halitamalizika bila kuwa na ushirikiano wa pamoja wa wadau mbalimbali na kwa kutumia njia anuai. Mara tatizo hili litakapoweza kutokomezwa hapa Tanzania ushahidi kutoka duniani unaonesha kwamba tatizo hili halitajirudia na utakuwa ni ushindi wa wanawake na watoto wa Kitanzania.

 

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania

Jumuiya ya Ulaya na wanachama wake 28 wanajizatiti katika kuongeza chahu ya ongezeko la usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake. Wanachama wote wanashiriki katika vuguvugu la kiulimwengu la kupinga ukeketaji. Jumuiya ya Ulaya inatambua kwamba ukeketaji unadhoofisha sana ubora wa maisha ya wanawake na wasichana na na unaathiri agenda ya maendeleo ya 2030. Jumuiya ya Ulaya inatoa usaidizi wa wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini wakiwemo Plan Internanal na  Save the children katika kupinga na kuzuia ukeketaji.

 

 

UNFPA

UNFPA Tanzania, ni sehemu ya ofisi za umoja wa mataifa (UN), ni mdau kiongozi katika kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kupiga vita ukeketaji kupitia Mpango kazi wa Taifa  dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wa 2017/18-2021/22. Programu ya UNFPA ya kupinga Ukeketaji unashirikiha wizarana Asasi mbalimbali kanma vile Jeshi la Polisi, Children’s Dignity Forum (CDF),  Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) na wengineo.

 

Ubalozi wa  Canada

Serikali ya Kanada ina dhamiria kuendeleza suala la usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa ulinzi wa wanawake, wasichana, haki za binadamu ndani ya Kanada na hata nchi za nje.

Sera yaa mambo ya nje ya Kanada inayozingatia usawa wa kijinsia na haki za wanawake inatoa kipaumbele kwa usawa wa kijinsia kupitia program yake maalum hapa Tanzania.

Pamoja na kuunga mkno juhudi za asasi za kiraia katika kutokomeza ukeketaji na ndoa za utotoni, Ubalozi wa Kanada umetoa usaidizi katika uzinduzi wa filamu ya “In The Name of Your Daughter sehemu mbalimbali dunianin ikiwa ni pamoja  kaskazini mwa Tanzania.

 

 

Ubalozi wa Uingereza   Tanzania

Uingereza imedhamiria kupambana dhidhi ya ukatili wa wanawake na watoto, utumikishwaji wa watoto, ndoa za utotoni nchini kwao na hata katika nchi nyingine.

Uingereza imeongeza rasilimali zaidi ya asilimia 60 katika kuongeza kasi ya mapambano hayo. Rasilimali hizo ni Pauni 35milioni za uingereza kupitia programu ya maendeleo maarufu kama DFID kwa ajili ya kutokomeza ukeketaji na pauni 36 milioni kwa lengo la kukomesha ndoa za uttoni.

 

Ubalozi wa  Ireland

Program ya ushirikiano wa kimaendeleo ya Ireland imejielekeza zaidi katika masuala ya afya, kilimo, lishe, utawala bora na haki za binaadamu. Pia ina mulengo thabiti wa haki za wanawake na wasichan.

Ubalozi huu hushirikiana na wadau wengine katika kuleta mabadiliko yanayolenga usawa katika mahusiano na kuwapa wanawake na wasichana fursa katika ngazi za maamuzi na kuchangia na kufaidika na malengo endelevu.

 

Latest News and Stories

Search