News/Stories

PUMZIKA KWA AMANI DK. REGINALD ABRAHAM MENGI

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania,(TAMWA), tumepokea kwa masikitiko kifo cha mmiliki wa kampuni za IPP nchini, Dk Reginald Mengi ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT.

 

Kifo hiki ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari nchini, pia kwa jamii ya Watanzania hasa kwa watu wenye ulemavu.

 

Dk Mengi ameacha alama katika tasnia ya habari kwa kuanzisha vyombo vya habari na alibeba dhamana ya kuwa mlezi kwa wanahabari nchini, na alileta heshima katika tasnia hii nchini.

 

Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tuzo za umahiri wa habari za Ejat hasa katika maudhui kuhusu watu wenye ulemavu, ambako amekuwa akidhamini tuzo hizo.

Atakumbukwa kwa upendo wake  mkubwa kwa wenye ulemavu. Dk Mengi amekuwa muumini mzuri wa masuala ya usawa wa kijisia katika taasisi zake ambapo ametoa nafasi za ajira na za uongozi kwa wanawake na wanaume.

 

Pia Dk Mengi alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini.

Dk Mengi alikuwa na ndoto nyingi, mojawapo ni ya kushirikiana  na serikali kutokomeza  umaskini kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa twitter Machi 19, ''Ndoto yangu ni kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa umaskini Tanzania''

 

Ulale salama Dk Mengi, tutaendelea kuyaishi maneno yako kwa mfano nukuu yake ya Januari 7 aliyotuma kupitia mtandao wake wa twitter akisema: ''Kwa unyenyekevu ninawashauri  watanzania wenzangu kuufanya mwaka 2019 kuwa mwaka wa upatanisho na msamaha, chuki ni mzigo mzito kuubeba mioyoni mwetu, kupendana ni njia peee ya kusonga mbele''.

 

Pumzika kwa amani Dk Mengi.

 

Rose Reuben

MKurugenzi TAMWA

 

Latest News and Stories

Search