News/Stories

TAMWA YAMPONGEZA JPM KUKEMEA MIMBA KWA WANAFUNZI

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinampongeza  Rais John Magufuli kwa kuzungumza kwa uwazi na kukemea  suala  la ongezeko la mimba kwa wanafunzi mkoani Rukwa.

Rais Magufuli ambaye yupo ziarani mkoani Rukwa amesema kwa takwimu alizonazo, kulikuwa na wanafunzi 229 waliopata mimba mkoani humo mwaka jana pekee.

 

“Ninawaomba ndugu zangu, ninawaomba sana, na ndugu zangu wasukuma acheni kuwaoza watoto wakiwa wadogo, tuwaache watoto wasome. Kwa sababu inawezekana tabia hizi hazikuwepo Rukwa, 229 kwa mwaka hawa ni wale waliojulikana, je wale wasiojulikana ni wangapi? Niwaombe ndugu zangu, wakina mama tuwakanye watoto wetu, wakina baba tuwakanye watoto wetu , ili wakaipate hii elimu wakawe wakombozi wa maisha ya baadaye,” amesema Rais Magufuli leo.

TAMWA ambayo miongoni mwa malengo yake ni kupunguza mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia, imefurahishwa na jinsi Rais Magufuli anavyoguswa na changamoto hii ya mimba za utotoni nchini na kuikemea hadharani.

 Kama Rais Magufuli alivyosema, mimba hizi za utotoni zinaitia hasara serikali inayotoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya elimu bure, shule za msingi na sekondari. Lakini si hivyo tu, bali mimba hizi ndicho chanzo cha vifo vya uzazi na pia chanzo cha maradhi ikiwamo Ukimwi.

 Taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa baadhi ya wanaohusika katika kuwapa mimba wanafunzi ni walimu, polisi na madereva bodaboda wasiofuata maadili. Wakati makundi hayo yanaaminiwa katika kuwapa ulinzi wanafunzi.

Kama Rais Magufuli alivyosisitiza, TAMWA  inawasihi wazazi na walezi wawafundishe watoto kuepuka vitendo vya ngono  na tunaziomba taasisi za dini kuwaelimisha watoto wa kike kujiepusha na vitendo vya ngono. Pia tunawaomba viongozi wa dini watoe mawaisha kuwakanya wanaume wanaolaghai wanafunzi.

 Pia tunaomba viongozi wa dini  watoe mawaidha ya kuwakanya  wanaume wanaowalaghai wanafunzi.

TAMWA imekuwa ikipigania haki za watoto wa kike na wanawake kwa ujumla na tunasisitiza kuwa tutaendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kupambana na kupunguza mimba za utotoni nchini kwa kutoa elimu kuanzia ngazi za vijiji, kata hadi ngazi ya mkoa.

Latest News and Stories

Search