Friday, 26 February 2016 03:00

TAMWA YASIKITISHWA KESI ZA UBAKAJI /ULAWITI KWA WATOTO KUTO HUKUMIWA

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA kinalaani vikali ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa za ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na baadhi ya madaktari hospitalini.

Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA kubaini kuwa kesi 62 za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu/ uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2014-2015

Kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi 43 bado ziko mahakamani, kesi 17 zimeshindwa kufika mahakamani, ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosekana ushahidi.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa TAMWA Bi Edda Sanga katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa TAMWA ambapo alihitimisha kwa kueleza kwamba TAMWA inaamini kuwa juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia hasa ubakaji zinaweza kufanikiwa endapo tu, vyombo vya mahakama, dawati la jinsia, madaktari, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wakiwa mstari wa mbele kusaidia kuhakikisha kesi husika zinafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa wakati, kwa haki na kwa mujibu wa sheria.

VISITORS COUNTER

5124911
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
10184
10790
53849
20974
272312
5124911

Your IP: 91.216.169.36
2020-07-02 21:28

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER