TAMWA

TAMWA

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH GEORGE SIMBACHAWENE KATIKA KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI LILILOANDALIWA NA TAMWA

 

 

MUUNGANO WA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOSHAWISHI MABORESHO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI

 

TAREHE: 23 MEI 2020

 

UKUMBI: PIUS MSEKWA DODOMA

 

KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI

 

Ndugu Waheshimiwa Wabunge;

 

Ndugu wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya  Ndani Ya Nchi;

 

Ndugu wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto;

 

Ndugu Wakurugenzi Asasi za Kiraia zinazoshawishi Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani;

 

Ndugu Waandishi wa habari na wadau wote wa Usalama Barabarani, Mabibi na Mabwana;

 

Ndugu Waandaaji wa hafla hii Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mwananchi Communication; - Habari za asubuhi.

 

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kutupa uhai na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo kuhudhuria Kongamano hili. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa taasisi ya zilizo shiriki kuandaa kongamano hili kuanzia wafadhaili, Wabunge, Mwananchi Communications, na Asasi zote za kiraia zinazoshawishi maboresho ya sharia ya usalama barabarani. Aidha, ninawashukuru kwa kunialika kuwa Mgeni rasmi katika kongamano hili muhimu kwa usalama wa watumiaji wa barabara nchini Tanzania. Hakuna shaka kongamano hili ni ishara ya juhudi zinazofanyika katika kuhakikisha suala la usalama barabarani linatiliwa mkazo.

 

Ndugu Washiriki

 

Kipekee pia Namshukuru Mh Raisi Dkt John Pombe Magufuli kwa kuniteua kusimamia Wizara hii yenye changamoto mbalimbali Ikiwemo changamoto ya Ajali za barabarani. Ninatambua kwamba changamoto hii ni kubwa lakini nipo tayari kuikabili kwa kutumia uwezo wangu na kwa kushirikiana nanyi nyote.

 

Ndugu Washiriki

Naomba pia kutumia fursa hii kuwashukuru waheshimiwa Wabunge, Wanahabari pamoja na wadau wote wa Muungano wa asasi za kiraia unaoshawishi maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani. Nawashukuru wote kwa kuweza kuitikia wito huu na  kushiriki nasi katika kongamano hili lenye mada isemayo Kuelekea Malengo ya Usalama Barabarani ya 2030: Tulipofikia, Fursa na Changamoto zijazo, ASANTENI SANA.

 

Ndugu Washiriki

Kongamano la usalama barabarani ni siku muhimu sana ya kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Masuala hayo ni pamoja na kuwakumbusha madereva juu ya kuwa waangalifu na kuzingatia sheria, hususani alama na ishara mbalimbali  wanapoendesha au kuegesha magari yao barabarani. Lakini pia ni siku muhimu kama nchi kuweza kutathimini juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali na wadau katika kukabiliana na ajali, kubaini changamoto zinazokwamisha kufikia malengo, na kutambua fursa mpya katika kukabiliana na ajali.

 

Ndugu Washiriki

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni  zinaonyesha kwamba zaidi ya watu 1,350,000 hufariki kwa ajali za barabarani duniani kote. Pia Ajali za barabarani zinatajwa kama sababu namba moja ya vifo kwa watoto wa umri kati ya miaka 5 hadi 14 pamoja na vijana wa umri kati ya miaka 15 hadi 29 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

 

Ndugu Washiriki

Ajali bado zimeendelea kuwa tatizo sugu katika taifa letu. Kama takwimu zinavyoonesha bado idadi ya vifo na majeruhi ni kubwa licha ya juhudi zinazofanyika. Mimi mwenyewe mara kwa mara nimesikia na kushuhudia ajali mbalimbali sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Ajali hizi zimekuwa zikiigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi, kupoteza nguvu kazi ya taifa, mada na vifaa tiba hospitalini. Wananchi pia wamekuwa wakipoteza wapendwa wao katika ajali na baadhi kusababishiwa ulemavu na majeraha ya kudumu. Na hii ndio sababu serikali kupitia Wizara yangu ipo katika mchakato wa kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani 1973, ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa. Wizara yangu itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kwamba tunaboresha Sheria hii ya Usalama Barabarani ya Mwaka 1973.

 

Ndugu Washiriki

Sisi kama Serikali tunayo nia dhabiti ya kuhakikisha kwamba Ajali zinapungua kwa Asilia 50 ifikapo 2030 kama ambavyo tumeahidi katika mikataba ya kimataifa na kama matakwa ya sheria za kimataifa zinavyosema. Hivyo ninawaomba wadau waendelee kushirikiana na serikali kwa kutoa maoni ni kwa namna gani tunaweza kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo 2030.

 

Ndugu Washiriki

 

Pia ninatambua mjadala huu ulioandaliwa na Wadau wa Usalama barabarani na wenzetu wa Mwananchi communications ni mojawapo ya njia muafaka ya kuleta mawazo pamoja ya kujadiliana namna bora ya kupunguza ajali barabani.

 

Ndugu Washiriki

Natambua kuwa bado wapo madereva wanaendesha magari wakiwa wamelewa; wapo watembea kwa miguu wanavuka barabara wakiwa wamelewa; wapo madereva wanaendesha kwa mwendokasi hatarishi katika maeneo ya makazi ya watu au yasiyoruhusiwa na alama za barabarani, ikiwa ni pamoja na kuyapita magari mengine sehemu zisizoruhusiwa.  Aidha, waendesha pikipiki, pamoja na abiria wao wamekuwa wakipuuzia kuvaa kofia ngumu (helmeti) kwaajili ya kujikinga na madhara yatokanayo na ajali za pikipiki. Mambo yote haya kwa pamoja ndiyo yanayotuletea majonzi kila siku. Hivyo nitumia fursa hii kuwaasa madereva kuendesha magari kwa uangalifu na kutii sheria zilizopo. Aidha, ninaliagiza Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

 

Ndugu Washiriki

Ili kuweza kufikia lengo la kupunguza vifo na majeruhi wa ajali za barabarani, inampasa kila mmoja wetu kubadili tabia. Njia mojawapo ya kubadili tabia za watumiaji barabara ni elimu na adhabu. Kama elimu inatolewa lakini bado kukakuwa na ukaidi wa utii wa sheria za barabarani basi adhabu hutumika. Hata hivyo, kwa hali ilivyo sasa adhabu zilizopo kwenye sheria ya usalama barabarani yam waka 1973 hazina meno ya kutosha kuweza kubadilisha tabia ya watumiaji wa barabara wasiotaka kutii sheria. Hivyo, ipo haja ya kufanya mabadiliko ya sheria ili kuweza kuwa na adhabu zenye nguvu zaidi na zinazoendana na uzito wa kosa. Ni matarajio yetu kuwa mara sheria mpya itakapopitishwa na Bunge tutakuwa na sheria bora na yenye adhabu kali kwa wavunjifu wa sheria. Hivyo nawaomba wadau wote ikiwemo waheshimiwa Wabunge mara Sheria hiyo itakapoletwa Bungeni tuweze kuiunga mkono kwaajili ya kuipitisha.

 

Ndugu Washiriki

Nimeeleza mengi. Naomba niishie hapa. Lakini kabla sijahitimisha, napenda niwashukuru tena kwa kunialika kwenye shughuli hii. Nawaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha usalama barabarani na kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha maendeleo katika sekta ya usafiri.  Aidha tutasimamia na kutekeleza sheria ipasavyo kwa faida ya watumiaji wote wa barabara. Kila mmoja wetu hapa leo aondoke akiwa balozi mwema wa usalama barabarani ili tushuhudie kupungua au kuondoka kabisa kwa ajali zinazoepukika.

 

Mungu Ibariki Tanzania!

“Ahsanteni sana kwa kunisikiliza”

 

 

Read more...

HOTUBA YA MKURUGENZI WA TAMWA KATIKA KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI LILILOANDALIWA NA TAMWA

HOTUBA

 

YA

 

BI ROSE REUBEN - MKURUGENZI MTENDAJI (TAMWA)

  

KWENYE

 

KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI

 

 

MADA: USALAMA BARABARANI KWA AFYA NA MAENDELEO YA UCHUMI

 

 

UKUMBI: UKUMBI WA BUNGE PIUS MSEKWA- DODOMA

 

 

TAREHE: 23 MEI 2020

 

Kipengele cha 1: Mtandao wa asasi za kiraia/zisizokuwa za kiserikali zinazoshawishi maboresho ya sheria ya usalama barabarani.

 

"Mtandao wa Usalama Barabarani Tanzania ni nini?. Kitu gani mtandao umefanya kuhusiana na Usalama barabarani?. Dhumuni kuu ni nini?"

 

I.Utangulizi

 

Ndugu Mgeni Rasmi, Waheshimiwa Wabunge, wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya  Ndani Ya Nchi, wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Viongozi wa Serikali, Wawakilishi Asasi za Kiraia zinazoshawishi Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Washirika wa Maendeleo, Wanahabari na Vyombo vya habari mliopo, Waathirika wa ajali za barabarani, Wageni waalikwa Mabibi na Mabwana,

 

Ni heshima kubwa kwangu kutoa hotuba hii, kwa niaba ya mtandao katika kongamano hili muhimu.

 

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo.  Napenda kuwapongeza TAMWA na Mwananchi communications  kwa maandalizi bora ya mkutano huu.

 

Napenda pia  kulishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hii.

 

Napenda pia kushukuru na kutambua juhudi kubwa za wajumbe wa Mtandao ambao wamefanya kazi kwa bidii kutayarisha hafla hii, haswa katika kufikia adhma ya


Naomba nianze kwa kutoa historia fupi ya mtandao huu wa asasi za kiraia unaoshawishi maboresho ya sheria ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kazi na mafanikio yake;

 

II.Shirikisho la Usalama BarabaraniTanzania

 

Mabibi na Mabwana,

 

Shirikisho la Usalama Barabarani Tanzania (CSO's) lilizinduliwa mnamo Mei 2016, na wanachama sita tu chini ya uratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), lakini umeongezeka hadi leo hadi wanachama wapatao kumi na tano ambao ni pmaoja na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), Amend Tanzania, Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT), Tanzania Media Foundation (TMF), Safe Speed Foundation, Women Legal Aid Centre (WLAC), WILDAF, Mwanza Youth and Children Network (MYCN), Media Space Tanzania, pamoja na watu binafsi wenye utaalamu na mapenzi na usalama barabarani.

 

Wajumbe wa umoja huo wamekuwa wakifanya kazi na Serikali (haswa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Uchukuzi na idara / mashirika chini ya wizara hizi), Shirika la Afya Duniani (WHO), Wabunge na watendaji wengine kuunga mkono utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Sheria, haswa juu ya mabadiliko ya sera kwa marekebisho kamili ya Sheria ya Sheria ya Usalama Barabarani (RTA). Sekretarieti ya Ushirikiano kwa sasa upo chini ya usimamizi wa TAWLA.

 

III.Kazi ya mtandao kuhusiana na usalamabarabarani

 

Mtandao huu ulianzishwa kwa malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa na sauti ya pamoja katika kuendesha kampeni ya kushawishi maboresho ya sheria ya usalama barabarani pamoja na kuongeza uelewa kwa umma juu ya masuala mbalimbali ya usalama barabarani.
vilevile mtandao huu uliundwa kwa lengo la kuwa kama kiungo kati ya watumiaji wa barabara pamoja ba viongozi wa serikali/watunga sera ili kushawishi kuwepo kwa mfuno wa kisheria na kisera unaoendana na viwango vya kimataifa.

 

Mtandao umerekodi mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara juu ya ukubwa wa tatizo hasa kwenye viashiria vitano vinavyochangia ongezeko ajali.

 

Mtandao umefanya kazi kwa karibu na kamati mbalimbali za bunge, hii ilipelekea wao kushawishika na kuamua kuanzisha mtanao wa kibunge unaojihusisha na masuala ya usalama barabarani ambao una takribani ya wabunge 120.

 

IV.Masuala ambayo Mtandao unayafanyiauchechemuzi;

 

Mtandao unafanya uchechemuzi juu ya mfumo bora wa kisheria juu ya usalama barabarani ili kuhakikisha kuwa ajali za barabarani zinapungua, ikiwa ni pamoja na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani pamoja na vifo. Pia shirikisho linatetea na kupigania uwepo wa Sheria ya Usalama Barabarani (RTA) ya mwaka 1973. Kuna mapungufu ambayo yalitambuliwa katika Sheria ya Usalama Barabarani (RTA) na kwamba ikiwa yataboreshwa, ajali za barabarani zitapungua, idadi ya majerahi na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani zitapungua.

 

Mapungufu yaliyotambuliwa yanahusiana na visababishi vitano hatarishi  ambavyo ni; Mwendo kasi, Matumizi ya vilevi wakati wa kuendesha chombo cha moto, Kutotumia kofia ngumu (helmet) kwa abiria na dereva wa pikipiki, Kutokufunga mikanda wakati wa safari, na kutotumia vizuizi vya watoto.

 

a.    Kwenye upande wa Mwendokasi – Mtandao unashawishi uendeshaji wa vyombo vya moto kwa spidi ya kilomita 50 kwa saa katika maeneo ya mijini na makazi, na kilomita 30 kwa saa mahali ambapo kuna alama za watembea kwa miguu na wanyama, Utafiti umeonyesha kuwa hatari ya kufa ni chini ya asilimia 20 wakati gari liko chini ya kasi ya kilomita 50 kwa saa na asilimia 60 wakati gari liko kwenye kasi ya kilomita 80 kwa saa. Inakadiriwa kuwa kupunguzwa kwa asilimia 5 kwa mwendokasi, kunapunguza asilimia 30 ya ajali mbaya ambazo zinazowezakutokea.

 

b.    Kwenye upande wa kuendesha chombo cha moto ukiwa umelewa – Mtandao unashawishi kupunguzwa kwa kiwango cha kilevi kutoka kwa miligramu 80 kwa kila mililita 100 za damu (0.08g / dl) hadi miligramu 50 kwa kila mililita 100 za damu (0.05g / dl) kwa angalau dereva mwenye uzoefu, na kutofautisha kati ya dereva mwenye uzoefu na asiye na uzoefu ambaye kiwango cha pombe cha damu kinapaswa kisizidi miligramu 20 kwa kila mililita 100 za damu (0.02g / dl.) Lazima kuwe na utekelezaji mzuri wa sheria inayohusiana na kunywa hadi kupitiliza mipaka iliyowekwa. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 ya vifo vyote vya barabarani vilivyoripotiwa ulimwenguni kote vinahusiana na ulevi (Ripoti ya hali halisi ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya 2018). Sheria yetu inaruhusu hadi kiwango cha pombe cha miligramu 80 kwa kila mililita 100 za damu (0.08g / dl.) Kuwa ndiyo Kiwango cha juu cha pombe kinachohitajika. Hatari ya ajali huongezeka mara tatu kwa madereva ambao hutumiavilevi.

 

c.    Kwenye matumizi ya kofia ngumu (helmet) – Mtandao unashawishi utumiaji wa lazima wa kofia ngumu kwa wote yaani, dereva na abiria kwa kwa sasa shiria inamtaja dereva pekee. Inakadiriwa kuwa asilimia 22 ya vifo vya ajali za barabarani uimwenguni kote vinatokana na pikipiki na bajaji. Imeelezwa kuwa majeraha mabaya yanajumuisha wapanda pikipiki ni yaleyaliyohusisha kichwa na shingo. Matumizi sahihi ya kofia ngumu yanaweza kusaidia kuzuia majeraha haya kwa asilimia 42 na kupunguzwa kwa asilimia 69 ya jeraha la kichwa (Ripoti ya hali halisi ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya 2018).

 

d.    Kwa upande wa matumizi ya mikanda – Mtandao unashawishi uwepo wa vifungu vinavyohitaji abiria wote wa gari kufunga mikanda ya kiti katika gari bila kujali wamekaa kiti cha mbele au nyuma. Takwimu zinaonyesha kuwa kufunga mkanda kunapunguza hatari ya ajali kwa abiria wa kiti cha mbele kwa asilimia 45-50 katika tukio la ajali. Vivyo hivyo, hatari ya majeraha madogo na makubwa hupunguzwa kwa asilimia 25 na 45 kwa abiria wa viti vya nyuma.  Kiwango cha kimataifa kinachokubalika kinahitaji matumizi ya mikanda ya kiti kwa viti vya mbele na nyuma. Sheria yetu inahitajikiti cha abiria wa mbele tu kufungaMkanda.

 

e.    Kwa upande wa kuwakinga watoto - Mtandao unapigania uwepo wa sheria ambayo itaweka matumizi ya lazima ya vifaa vya kukinga watoto (Vizuizi vya watoto). Ushahidi unaonyesha kwamba wakati watoto wameketi katika viti vyao vyenye vizuizi, kulingana na uzito na saizi ya mwili wao, hatari ya majeraha na kifo hupunguzwa kwa karibu asilimia 70. Viwango vya kimataifa vinahitaji kuwa watoto wa umri wa miaka chini ya 7 wanapaswa kutumia vizuiziili kuzuia majeraha na vifo ikiwa ajali itatokea. Hakuna toleo juu ya vizuizi vya watoto katika Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168.

 

Kwa mara nyingine ninawashukuru na kuwapongeza wote ambao wamefanikisha tukio hili. Ni matumaini yangu kuwa maazimio yote tutakayoafikiana hapa katika kongamano hili, yatafanyiwa kazi na kuja na njia ambazo ni bora na sahihi zaidi katika kupunguza ajali za barabarani .

 

 

USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.!

 

“Ahsanteni sana kwa kunisikiliza”

Read more...

VIRUSI VYA CORONA NA USALAMA WA WANAHABARI

Aprili 11, 2020. Wakati huu ambapo dunia nzima inapambana na ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya Corona, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinawakumbusha wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kufuata miongozo ya kutekeleza majukumu yao kwa kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huu, na kutumia zaidi teknolojia ya mawasiliano.  Ugonjwa wa Covid-19 unaweza kumuathiri mtu yeyote, hivyo wanahabari, wamiliki wa vyombo vya habari na wadau wote wa habari wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya kiutendaji kazi yatakayowaepusha dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu. TAMWA inawashauri wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kujikita katika kutumia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano kupata habari badala ya kwenda katika mikusanyiko isiyo ya lazima kwani taarifa zinaweza kutumwa kimtandao au mahojiano kwa njia ya simu. “Bila shaka hofu ya ugonjwa wa Covid 19 itabadili mfumo wa utendaji kazi wa tasnia ya habari kama taasisi inayohudumia jamii na kuanza kujiona kuwa na wao pia ni sehemu ya jamii,” TAMWA tunathamini usalama wa wanahabari kwa kuwa sisi ni sehemu na mdau wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa chanzo cha ufikishaji wa taarifa za kutetea haki za wanawake na watoto zenye lengo la kuwa na Tanzania inayoheshimu misingi ya usawa wa jinsia.  Wanahabari wanaoripoti kuhusu COVID-19 na wanahabari wengine, wanashauriwa kufanya maandalizi kabla ya kwenda katika mikutano, kwa kufuata mbinu za kujikinga na maambukizi. 

Read more...

VISITORS COUNTER

5209364
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
12945
14051
61015
105427
272312
5209364

Your IP: 66.249.64.16
2020-07-09 19:51

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER