Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimewakutanisha wafanyakazi wake wapatao 26 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kwa lengo la kujadili kwa pamoja mpango mkakati wa mwaka mpya wa 2018.

 

Mkutano huo wa siku 3 ulianza tarehe 17 na kumalizika leo tarehe 19 mwezi wa Desemba mwaka 2017 katika hoteli ya Giraffe Mbezi Beach, Dar es salaam mbapo umewawezesha wafanyakazi wote kwa pamoja kujadili changamoto na mafanikio waliyopata kwa mwaka 2017 na kuona jinsi ya kuendelea mbele katika mwaka mpya ujao. Aidha mkutano umewawezesha wafanyakazi  kupanga na kukubaliana mpango kazi wa mwaka 2018 kwa kila idara ili kuhakikisha wanafikia malengo ya taasisi TAMWA.

Edda Sanga (Mkurugenzi mtendaji) akifungua rasmi mkutano wa siku 3 kujadili mpango kazi kwa mwaka 2018

 

Davis Lumala (Meneja mkakati) akiwasilisha mpango mkakati kwa mwaka 2018

 

Aimo Makunza (Muhasibu mkuu) akiwasilisha bajeti ya mpango mkakati kwa mwaka 2018

 

Labiybu Ramadhani (Meneja ufatiliaji na tathmini) akiwasilisha mpango mkakati kwa mwaka 2018

 

 

Baadhi ya wafanyakazi wa TAMWA wakiwa katika picha ya pamoja

VISITORS COUNTER

1522966
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
84
343
1806
72237
8192
9678
1522966

Your IP: 54.80.68.137
2018-05-24 04:13

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER