Friday, 21 June 2019 00:00

MKURUGENZI TAMWA ATWAA TUZO YA 'WANAWAKE KATIKA UONGOZI'

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben ametwaa tuzo ya ‘Wanawake katika Uongozi’ iliyotolewa na World Women Leaders Congress (WWLC) Juni 19 jijini Dar es Salaam. 

 

Tuzo hizo zilitolewa kwa wanawake viongozi wa Afrika Mashariki walioleta mabadiliko katika jamii, walioibua vipaji, wanawake mifano ya kuigwa na wenye uthubutu kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya binafsi na serikali kutoka katika ukanda wa Afrika Mashariki. 

Wanawake viongozi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walitunukiwa tuzo hizo kutokana na vigezo vya ushindi vilivyowekwa. 

Akizungumzia tuzo hiyo, Reuben amesema tuzo hiyo  inawatia moyo wanawake wengine kufanya bidii zaidi kwani kuna watu wanawakubali na wanaweza kuzitunuku kazi zao.

“Wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri, tuzo hii inaeleza kuwa uongozi wa wanawake unakubalika, hii ni tuzo ya dunia, kumbe ulimwengu umekubali kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi,” amesema

Ameongeza: “Jamii kwa ujumla ikubali  kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi. Wanahabari wafanye kazi zao kwa kujiamini, kazi zao zikajulikana na wasikatisshwe tamaa na kitu chochote.”

Wengine waliotwaa tuzo hizo kutoka Tanzania ni Emma Kawawa, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Tanzania Women CEO’S Roundtable.

Tuzo hizo zinatolewa ili kuhamasisha wanawake viongozi katika sekta za umma na binafsi, kutambua mafanikio ya wanawake  kikanda na kidunia pamoja na kuwatia moyo wanawake vijana kushika nafasi za mbalimbali za uongozi.

Read 111 times Last modified on Sunday, 30 June 2019 21:09

Media

5 comments

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

2525628
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
3977
3994
12294
132709
197824
2525628

Your IP: 46.229.168.150
2019-07-23 20:07

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER