Wednesday, 18 September 2019 03:00

VIONGOZI TAMWA WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Mwandishi Wetu, TAMWA

Dar es Salaam. Viongozi wapya wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) wamefanya ziara katika vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha.

 Viongozi hao, Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben na Mwenyekiti wa chama hicho, Joyce Shebe walitembelea vyombo vya habari kumi ikiwa ni awamu ya kwanza ya ziara hiyo.

Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyotembelewa na viongozi hao wa TAMWA ni pamoja na Tumaini Media, Upendo Media, Radio Maria ,Star TV, Channel Ten, EFM Radio, Times FM Radio, Azam Media na kampuni  ya magazeti ya  Mwananchi Communication na The Citizen  na New  Habari Co-operation.

Shebe alisema lengo la ziara hiyo ni viongozi hao wapya wa TAMWA kujitambulisha kwa vyombo vya Habari ili kuimarisha uhusiano, kuhamasisha waandishi wanawake kujiunga na chama hicho cha kitaaluma.

“Ongezeko la wanachama wapya ndani ya TAMWA litawasaidia kunufaika na nafasi za kitaaluma kupata mikopo ya kujiendeleza na masomo ya elimu ya juu kama Shahada na kuhudhuria makongamano ya kitaaluma, fursa za mafunzo ya kitaalum,”alisema Shebe

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben alipongeza jitihada za baadhi ya vyombo vya habari katika kutunga sera za  kuimarisha usawa wa kijinsia  na kutoa nafasi za uongozi kwenye  vyombo vyao.

 Kadhalika viongozi hao walipongeza jitihada za baadhi ya vyombo vya habari katika kutunga sera za kuimarisha usawa wa kijinsia kwenye nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyumba vya habari.

TAMWA ni shirikisho lisilo la kiserikali lililoanzishwa  miaka 31 iliyopita kwa lengo la kutetea haki na ustawi wa wanawake na watoto kupitia vyombo vya habari.

Vigezo vya kujiunga na TAMWA ni pamoja na kuwa mwanamke mwanahabari, shahada ya mawasiliano ya umma au ya habari na uzoefu wa kazi ya uandishi wa miaka mitatu.

Katika ziara hiyo TAMWA imekutana na kuzungumza na viongozi wa vyombo  vya habari  kama  wakurugenzi na wahariri wakuu, na kujifunza mambo mengi yanayoendelea ndani ya vyumba vya habari nchini.

 

Read 537 times Last modified on Tuesday, 24 September 2019 15:01

20 comments

 • Comment Link Dortha Briddick Wednesday, 01 January 2020 14:00 posted by Dortha Briddick

  I was reading some of your posts on this internet site and I conceive this site is rattling informative! Keep on putting up.

 • Comment Link Gertie Gierisch Saturday, 28 December 2019 02:25 posted by Gertie Gierisch

  Dreamwalker, this drop is your next piece of data. Feel free to message the agency at your convenience. No further information until next transmission. This is broadcast #5684. Do not delete.

 • Comment Link hollinsfh Wednesday, 18 December 2019 05:10 posted by hollinsfh

  nike air force 1 07 lv8 zwart mens nike dallas cowboys 8 troy aikman game navy blue team color nfl jersey sale cheap boston red sox baseball hats vancouver ky nike air max 90 leder child white yellow uk 2015 16 nba western all stars 13 james harden revolution 30 swingman red jersey nike air vapormax flyknit moc 2 womens grey black shoes
  hollinsfh http://www.hollinsfh.com/

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

4505875
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
1488
2434
3922
89481
214712
4505875

Your IP: 41.75.221.11
2020-03-30 12:51

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER