Chama cha Wanahabari Wanawake nchini –TAMWA kimestushwa na kinalaani vikali tukio la mauaji yaliyofanywa na Bw. Respicius Diocless, baba mzazi wa watoto Deonidas Respicus (4) na Deocless Respicius (4) mapacha katika kijiji cha Bulambizi kata ya Kanyangereko halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.

 

 Mauaji hayo ya kutisha yamefanywa na baba mzazi wa watoto hao mapacha kwa kuwachinja na kuwatenganisha vichwa na viwiliwili usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 15th April, mwaka 2018 kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Ni kitendo cha kinyama ambacho kinastahili kukemewa na kukomeshwa kwa nguvu zote na kila mtanzania mpenda amani. TAMWA inaamini kuwa katika ugomvi wa wazazi kwenye familia, watoto hawapaswi kuhusishwa.

 TAMWA imebaini kwamba Vitendo vya mauaji kwa watoto wasio na hatia vimeendelea kushamiri na kutishia makuzi ya watoto ambao wana haki ya kupendwa na kulindwa. Hata hivyo baadhi ya wazazi  wamekuwa wakitumia nafasi zao katika familia kuwakatili  watoto wao bila kujali utu au ndoto za watoto waliowazaa wenyewe.

 Aidha ikumbukwe kwamba hawa watoto tulionao leo, ni kizazi cha sasa na nguzo ya taifa. Kwa mantiki hiyo TAMWA, inavitaka vyombo vya usalama na sekta husika kuchukua hatua za makusudi na kuhakikisha mzazi aliyehusika na unyama huo anachukuliwa hatua za haraka kisheria kukomesha vitendo vya kikatili kwa watoto ili taifa liishi maisha ya kistaarabu, yenye utangamano, utulivu na amani.

 TAMWA kama ilivyo taasisi ya kuelimisha jamii juu ya masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, kupitia kituo chake cha Usuluhishi cha (CRC), kwa mwaka jana 2017 matukio ya watoto kufanyiwa ukatili na wazazi, ndugu, jamaa wa karibu walikuwa 105. Matukio hayo ya ukatili yalihusisha kupigwa, kubakwa, kunyimwa chakula , kufanyishwa kazi nzito, kutelekezwa na mengine kama hayo. Idadi hiyo ni kubwa mno kwa ustawi wa jamii.

 Edda Sanga,

Mkurugenzi Mtendaji

VISITORS COUNTER

1522983
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
101
343
1823
72237
8209
9678
1522983

Your IP: 54.80.68.137
2018-05-24 04:18

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER