Tuesday, 20 December 2016 13:06

TAMWA YAZINDUA MATOKEO YA TATHMINI YA MWISHO KWA MRADI ULIOTEKELEZWA KUANGALIA HALI YA MATUMIZI YA POMBE KUPINDUKIA

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania – TAMWA kimefanya tathmini kuchunguza matumizi ya pombe, madhara, upatikanaji wake pamoja na uelewa wa jamii za kata za Makumbusho, Saranga na Wazo Hill wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

TAMWA kwa ufadhili wa (IOGT-NTO Movement) imetekeleza mradi wa kupinga ulevi wa pombe wa kupindukia katika kata 3 kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Kupitia utekelezaji wa mradi huo, TAMWA tumeweza kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kupitia elimu iliyokuwa ikitolewa kwa jamii kupitia vyombo vya habari mbalimbali, ushauri nasihi na msaada wa kisheria kwa waliofanyiwa vitendo vya kikatili kijinsia.

 

Jumla ya dodoso 458 zilifanikiwa kujibiwa katika tathmini hii. Matokeo ya jumla ya utafiti huu ambao ni wa mwisho wa mradi, yamebaini kuwa kuna upungufu wa matumizi ya pombe ikilinganishwa na ‘Tathmini ya Hali ya Matumizi ya Pombe (Alcohol Situation Analysis-ASA)’ ya mwaka 2014. Matokeo ya utafiti yameonyesha kuwa pombe ilinyweka kwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 28 kwa mwaka 2016. Aidha, tathmini imeonyesha kuwa asilimia 13 ya waliohojiwa kwa mwaka 2014 pamoja na 2016 walianza kunywa pombe wakiwa na umri wa miaka 14 na 17.Matokeo ya mwaka 2016 ni asilimia 14.

 

Hata hivyo asilimia 29 kwa mwaka 2014 na asilimia 22 kwa mwaka 2016 ya wanawake waliohojiwa katika dodoso,walikubali kufanyiwa vitendo vya ukatili na wanaume kutokana na matumizi ya pombe. Utafiti pia umeonyesha kuwa 20% na 23% kwa mwaka 2014 na mwaka 2016 ya vijana wenye umri chini ya miaka 25 walisema kuwa walifanyiwa ukatili na wanaume kutokana na matumizi ya pombe. Utafiti huo aidha, umeonyesha kuhusu uwepo wa uuzwaji pombe katika makazi ya watu kuwa umbali wa vilabu vya pombe ni chini ya meta 100 kutoka kwa kila aliyejibu dodoso la utafiti huu. Hali hii ilijidhihirisha kwa sababu 63% ya waliohojiwa kwa mwaka 2014 na 46% kwa mwaka 2016 walikubaliana kuwa vilabu vya pombe katika makazi vipo umbali wa meta 100.

 

Kwa ujumla tathmini hii imedhihirisha wazi kuwepo kwa matokeo chanya katika maeneo ya mradi. Kuna kila haja ya kuwepo kwa mwendelezo wa mradi wa elimu kama hii kwa jamii.

Cha msingi tushirikiane,kwani kwa pamoja,TWAWEZA.

Read 5765 times Last modified on Tuesday, 20 December 2016 13:08

31 comments

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5202879
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
6460
14051
54530
98942
272312
5202879

Your IP: 5.18.235.239
2020-07-09 10:03

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER