Monday, 06 February 2017 12:52

TAMWA YAUNGANA NA WADAU KUADHIMISHA SIKU YA UKEKETAJI DUNIANI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2017, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.

 

Kauli mbiu mwaka huu ni “Ujenzi wa daraja shirikishi na imara kati ya Afrika na Dunia kuondoa ukeketaji ifikapo mwaka 2030” (“Building a solid and iteractive bridge between Africa and world to accelerate ending FGM by 2030) ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Kiafya wa demografia wa (TDHS-MIS) mwaka 2015-16, umeeleza kuwa mwanamke mmoja kati ya kumi amekeketwa licha ya elimu ya kuhusu madhara ya ukeketaji kuendelea kutolewa kwa jamii kila mara

 

Utafiti huo umebaini kuwa, uelewe kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka kutoka asilimia 71 ya wanawake hadi kufikia asilimia 97. Aidha, utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha wanawake wenye umri kati ya miaka 15-29 waliokeketwa kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwaka 2015.

 

TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapata elimu endelevu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake kwa kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.

 

Aidha TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ikiwemo vitendo vya ukeketaji na aina zote za ukatili wa kijinsia

 

 

Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji.

Read 3292 times Last modified on Monday, 06 February 2017 12:54

13 comments

 • Comment Link Harris Tuesday, 12 November 2019 04:25 posted by Harris

  Hey! I just wanted to ask if you ever have any problems with hackers?
  My last blog (wordpress) was hacked and I ended up losing
  many months of hard work due to no back up. Do you have any solutions to protect against hackers?

 • Comment Link Darrin Villasenor Thursday, 16 May 2019 01:26 posted by Darrin Villasenor

  HI! I like your article. It is very helpful. Tank You for posting it.

 • Comment Link Stacia Sunday, 12 May 2019 23:11 posted by Stacia

  I have learn some good stuff here. Certainly worth bookmarking
  for revisiting. I surprise how so much attempt you put to create any such fantastic informative site.

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5139835
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
2845
10942
68773
35898
272312
5139835

Your IP: 54.36.149.67
2020-07-04 06:10

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER