Print this page
Sunday, 12 April 2015 03:00

MKUTANO MKUU WA TAMWA 2014:MARCH 27,2015

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO MKUU WA TAMWA 2014 JUMAMOSI

Zaidi ya Wanachama 100 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA Jumamosi tarehe 28th Machi, 2015 wanafanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka 2014 ambapo pamoja na mambo mengine wanachama watapata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2014, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2015-2021. Mkutano huo utaanza saa 2:00 asubuhi katika ofisi za chama zilizoko Sinza Mori, Dar es Salaam.

 

Mkutano huo utakaoanza na mafunzo Ijumaa tarehe 27th Machi mwaka huu utawapa fursa wanachama kujadili mafanikio yaliyopatikana kwenye mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita (2009 -2014) pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji ambapo pia watamchagua Mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake.

Aidha Siku ya Jumamosi baada ya mkutano huo wanachama watajumuika pamoja katika hafla ya kuchangia mfuko wa shughuli za TAMWA (Gala Dinner) ambazo ni pamoja na kupiga vita vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto itakayofanyika jioni katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mkutano mkuu wa TAMWA ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.

Valerie N. Msoka

Mkurugenzi Mtendaji

Read 8158 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:45
Tamwa

Latest from Tamwa