Sunday, 12 April 2015 03:00

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI :DECEMBER 01,2014

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SIKU YA UKIMWI DUNIANI IADHIMISHWE KWA KUPINGA UKATILI KIJINSIA

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kinaungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo hufanyika tarehe 1 Desemba kila mwaka, kikiitaka jamii kuvichukulia hatua vitendo vya unyanyasaji kijinsia ambavyo huchangia ongezeka la maambukizi ya Virusi Vinavyosababisha UKIMWI (VVU).

Miongoni mwa ukatili unaochangia ongezeko la VVU ni pamoja na ubakaji, wanawake kurithiwa, watoto wa kike kulazimishwa kuolewa na ukeketaji vitendo ambavyo hufanyika kwa wawanamke na watoto kwa kulazimishwa bila kujali hiari ya mtu husika.

 

Tafiti zinasema kuwa 5.1% ya Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wanaishi na VVU. Maambukizi ya VVU ni makubwa na kati ya hao wanawake ni 6.2% na wanaume ni 3.8% katika Tanzania Bara, kiwango cha maambukizi ya VVU ni miongoni mwa wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 15-49 ambapo yamepungua kutoka 7.0% mwaka 2003-04 na 5.3% katika mwaka 2011-12.

TAMWA imesisitiza kuwa kama jamii na serikali havitashirikiana kikamilifu kushughulikia vitendo vya ukatili kijinsia kisheria, kauli mbiu ya mwaka huu ya Tanzania Bila Maambukizi Mpya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na UKIMWI na Ubaguzi na Unyanyapaa Inawezekana haitaweza kufanikiwa.

Aidha TAMWA kupitia mradi wake wa Kujenga na Kuimarisha Usawa na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia (GEWE II) kwa kutumia vyombo vya habari nchini kimekuwa kikielimisha jamii namna ya kutambua ukatili wa kijinsia na madhara yake na kuitaka serikali na vyombo vya sheria kuweka mikakati itakayowezesha kuutokomeza.

TAMWA inaamini kuwa endapo jamii itavitolea taarifa mapema vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto pale vinapotokea na kuhakikisha vikavishughulikiwa ipasavyo, maambukizi ya UKIMWI yanaweza kupungua kwa haraka.

Valerie N. Msoka

Mkurugenzi Mtendaji

Read 9912 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:37

18 comments

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5134163
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
8115
11321
63101
30226
272312
5134163

Your IP: 66.249.70.6
2020-07-03 17:33

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER