Print this page
Sunday, 12 April 2015 03:00

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI : DECEMBER 10, 2014

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTAFITI WA UNYANYASAJI KWA MAENDELEO YA MWANAMKE NA TAIFA

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini-TAMWA kikishirikiana na mashirika mengine manne ya kutetetea haki za wanawake na watoto , leo kinazindua ripoti ya utafiti kuhusu uelewa wa jamii juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika ofisi zake za Sinza Mori, Dar es Salaam saa 3 asubuhi.

Ripoti ya Utafiti huo uliofanyika katika wilaya 10 zikiwemo 3 za visiwani ambazo ni (Pemba Kaskazini), Magharibi (Unguja Mjini Magharibi),

Unguja Kusini na 7 za Tanzania Bara ambazo ni pamoja na Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara ), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini, Ruangwa (Mtwara), Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam itatoa matokeo baada ya kumalizika kwa mradi huo unaojulikana kama (GEWE II)

Aidha kutokana na Utafiti mkubwa wa Hali ya Afya Tanzania (Demographic Health Survey) uliofanyika mwaka 2010 umeonyesha kuwa, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 umeongezeka kutoka asilimia 33% miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia asilimia 44% mwaka 2010.

TAMWA inaamini kuwa utafiti huu uliofadhiliwa na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania utasaidia kuendelea kufichua hali halisi ya vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto vikiwemo, ukeketaji, ubakaji, vipigo kwa wanawake, mimba katika umri mdogo na vingine kama hivyo ambavyo vimekuwa vikimkwamisha mwanamke katika kuboresha maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi.

TAMWA, katika utafiti huu imeshirikiana mashirika ya Mtandao wa Kijinsia Tanzania-TGNP, Chama cha Wanasheria Wanawake-TAWLA, Jumuiya ya WanawakeWanasheria Zanzibar (ZAFELA), na Kituo Cha Usuhishi-CRC ambayo pia yalishirikiana katika kutekeleza mradi huo.

 

Valerie N. Msoka

Mkurugenzi Mtendaji

Read 10781 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:35
Tamwa

Latest from Tamwa