Sunday, 12 April 2015 03:00

SIKU YA UKEKETAJI MKOANI SINGIDA:FEBRUARY 06,2015

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMWA KUAZIMISHA SIKU YA UKEKETAJI MKOANI SINGIDA LEO

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 mwezi wa pili, 2015 saa 2:00 asubuhi kuadhimisha siku ya Kitaifa ya kupinga ukeketaji duniani ambayo mwaka huu kilele kitafanyika mkoani Singida.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Katala Beach Hotel (KBH) mjini Singida yanahusisha mikoa yote iliyoathirika na ukeketaji ili kuunganisha nguvu za wabunge, wakuu wa mikoa, polisi, mahakimu, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirkia ya kimaendeleo, wahanga wa vitendo hivyo, wanafunzi, walimu, wazee wa mila pamoja na ng’ariba ili kuweka mikakati ya kuondoa ukatili huo kutoka asilimia 15 hadi sifuri.

 

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mh. Sophia Simba huku kauli mbiu ikiwa ni “Piga vita ukeketaji” maadhimisho yanafanyika katika kipindi ambacho wanawake na wasichana zaidi ya 1,500 nchini hukeketwa kila msimu, hivyo yatajenga nguvu ya pamoja ili kuhakikisha vitendo hivyo vinapungua kama siyo kuisha kabisa.

TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapatiwa elimu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake, kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na taifa kwa ujumla.

Aidha TAMWA kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), shirika ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watoto wa kike, imekuwa ikipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ukiwemo ukeketaji kwa kuelimisha jamii ili iondokane na mila hizo hasa katika mikoa ya Mara, Manyara, Dodoma, Singida, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro na Tanga.

Valerie Msoka

Murugenzi Mtendaji

Read 10089 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:20

19 comments

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5134052
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
8004
11321
62990
30115
272312
5134052

Your IP: 5.18.235.239
2020-07-03 17:18

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER