Sunday, 12 April 2015 03:00

MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI : FEBRUARY 22,2015

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kwa kushirikian na Shirika linalo hudumia Idadi ya Watu UNFPA Kinatoa mafunzo ya siku tatu kuhusiana na kuandika habari za uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia.Mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa habari mapema tarehe 23 hadi Tarehe 25 Februari mwaka huu katika kanda tatu nchini Tanzania.

Mafunzo katika kanda ya Kaskazini yatajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara Tanga na Kilimanjaro na yatafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika Kanda ya Kati, waandishi wa habari watatoka mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora ambapo mafunzo yatafanyika mjini Singida. Mafunzo katika Nyanda za Juu Kusini yatajumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma na yatafanyika mjini Iringa.

 

Miongoni mwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na ubakaji,wanawake kurithiwa, watoto wa kike kulazimishwa kuolewa na ukeketaji kwa wawanamke na watoto.

Aidha TAMWA kupitia mradi yake imeweza Kujenga na Kuimarisha Usawa na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa kutumia vyombo vya habari nchini. Imekuwa ikielimisha jamii namna ya kutambua ukatili wa kijinsia na madhara yake na kuitaka serikali na vyombo vya sheria kuweka mikakati itakayowezesha kuutokomeza.

TAMWA imesisitiza kuwa kama jamii na serikali hawatashirikiana kikamilifu kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia, itakuwa ni vigumu kutokomeza vitendo hivyo.

TAMWA inaamini kuwa endapo jamii itatoa taarifa mapema dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto pale vinapotokea, ingesaidia kuhakikisha vinashughulikiwa ipasavyo na hivyo kupungua kwa haraka na hatimaye kutokomezwa kabisa.

Valerie N. Msoka

Mkurugenzi Mtendaji

Read 9075 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:42

1 comment

  • Comment Link Modesto Jone Thursday, 01 August 2019 01:19 posted by Modesto Jone

    |I discovered your page accidentally nevertheless i'm happy i'm here. Good stuff i'm reading.

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5143333
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
6343
10942
72271
39396
272312
5143333

Your IP: 178.186.230.9
2020-07-04 13:16

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER