Sunday, 12 April 2015 03:00

KUPINGA NDOA ZA UTOTONI :FEBRUARY 24,2015

Written by 
Rate this item
(0 votes)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UBALOZI WA KANADA KUMTUNUKU MKURUGENZI MTENDAJI WA TAMWA KUWA BALOZI WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI

Ubalozi wa Canada nchini Tanzania kwa mara ya kwanza utamkabidhi Muurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Msoka kuwa balozi wa kampeni ya kupinga ndoa za utotoni (CEFM).

Kwa mujibu wa Ubalozi huo, tukio hilo litafanyika leo, Februari 24, 2015 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Hafla hiyo itahudhuriwa, miongoni mwa watu wengine, na Katibu Mkuu Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe, Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Lévêque, Msaidizi wa Balozi wa Canada anayehusika na masuala ya kisiasa, Eric Bertram, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari.

 

CEFM inatambua mchango uliotolewa na mtu ambaye ametumia jitihada na muda wake mwingi katika kutetea haki za watoto na ambaye amekuwa akiunga mkono harakati za kuhakikisha taifa letu linakua mahali salama kwa watoto hasa watoto wa kike katika kizazi cha sasa na kijacho.

Kutokana na uzoefu wake wa kupigania haki za biandamu hasa haki za wanawake na watoto, Valerie, ameifanya TAMWA kuwa jina la kukumbukwa katika kuleta usawa na haki za wanawake na watoto. Majukumu yake ya hivi karibuni ni pamoja na:

Mbunge katika Bunge Maalum la Katiba: Alifikisha masuala ya ndoa za utotoni nchini Tanzania katika bunge hilo na haja ya kuingiza umri wa motto unaotambulika kisheria katika katiba. Hii ilisababisha kamati za Bunge hilo kupendekeza umri wa motto kikatiba kuanzia 0 hadi miaka 18.

Mjumbe wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba: Aliweza kutetea masuala ya usawa ndani ya kamati ikiwa ni pamoja na haki ya kumlinda mtoto wa kike na wanawake dhidi yya mila potofu ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni, ukeketaji, haki ya kumiliki ardhi na uongozi.

Mjumbe wa Mtandao wa Kupinga Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN): Aliwezesha kuundwa kwa ukanda huru wa kukomesha ndoa za utotoni nchini Tanzania (Agosti 2014) kwa kuwa mwezeshaji wa tukio hilo jijini Dar es salaam mbele ya rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, mgeni rasmi Graca Machel, wakuu wa Balozi mbalimbali nchini na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Kutambuliwa kwake kuwa Balozi wa Kampeni ya Kupinga Ndoa za Utotoni, kutaleta hamasa zaidi na kumfanya kuongeza jitihada, nguvu na kutoa muda wake zaidi katika kutetea haki za watoto nchini Tanzania.

Valerie N. Msoka

Mkurugenzi Mtendaji

 

Read 130245 times Last modified on Sunday, 12 April 2015 11:39

105 comments

  • Comment Link jordan 11 concord Sunday, 08 September 2019 02:36 posted by jordan 11 concord

    rglpzfm,Definitely believe that which you said. Your favourite justification appeared to be on the net the simplest thing to remember of.I LOve your Blog!

  • Comment Link NFL Jerseys Sunday, 08 September 2019 01:29 posted by NFL Jerseys

    qullqj,Very informative useful, infect very precise and to the point. I’m a student a Business Education and surfing things on Google and found your website and found it very informative.I LOve your Blog!

  • Comment Link Yeezy Friday, 06 September 2019 14:17 posted by Yeezy

    fmoiapom,Some really nice stuff on this website, I enjoy it. I LOve your Blog!

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5240975
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
13872
15992
92626
137038
272312
5240975

Your IP: 189.115.71.124
2020-07-11 21:24

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER