Thursday, 08 March 2018 08:09

TAMWA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA leo, kinaungana na mashirika yote nchini yanayotetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.

 Maadhimisho haya yanabeba kauli mbiu ya kitaifa inayosema  “Wakati ni sasa: Wanaharakati Mijini na Vijijini kubadilisha maisha ya wanawake”, ambayo inatutaka wote tushirikiane kikamilifu kubadilisha maisha ya wanawake kwa kuondokana na ukatili wa kijinsia ili kupanua wigo wa fursa za usawa kiuchumi kwa wanawake.

TAMWA leo kwa kushirikiana na mgeni rasmi Mbunge Anjelina Malembeka katika maadhimisho hayo inafanya Kongamano lenye lengo la kuwaleta pamoja wadau kutoka katika Wilaya ya Ilala na Kinondoni Kata ya Kitunda eneo la uwanja wa Lukolo Annex Florida, kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 7: 00 Mchana ambapo watajadili na kupanga mikakati ya pamoja ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

 Kwa mujibu wa takwimu za Jeshi la polisi nchini, makosa ya ubakaji na kunajisi yaliyoripotiwa yameongezeka kutoka 6,985 Novemba mwaka 2016  mpaka 7,460 mwaka 2017, ukatili ambao unawakumba hasa wanawake na watoto na kuzorotesha ukuaji wa maendeleo kiuchumi kwani jamii inatumia muda mwingi katika kufuatilia kesi za ukatili wa kijinsia badala ya kufanya shughuli za maendeleo ya kuinua uchumi. 

 

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yana lengo la kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa, kikanda  na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na zinalidwa.

 

Edda Sanga,

Mkurugenzi Mtendaji

Read 3905 times Last modified on Thursday, 15 March 2018 13:13

213 comments

 • Comment Link g Tuesday, 16 June 2020 23:45 posted by g

  Wow, amazing blog layout! How long have you been blogging for?
  you make blogging look easy. The overall look
  of your website is fantastic, as well as the content!

 • Comment Link g Tuesday, 16 June 2020 00:31 posted by g

  I enjoy what you guys are usually up too. This type of clever work and exposure!
  Keep up the terrific works guys I've added you guys to my personal blogroll.

 • Comment Link g Monday, 15 June 2020 15:22 posted by g

  I have been surfing online greater than three hours today, but
  I by no means discovered any attention-grabbing article like yours.
  It is beautiful worth sufficient for me. In my opinion, if all web owners and bloggers made just
  right content material as you probably did, the web will probably be a lot more helpful than ever
  before.

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5157194
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
8845
11359
8845
53257
272312
5157194

Your IP: 46.229.168.144
2020-07-05 19:05

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER