Friday, 13 April 2018 10:50

MKUTANO MKUU WA TAMWA JUMAMOSI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Zaidi ya Wanachama 150 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA, Jumamosi tarehe 14th April, 2018 wanafanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine, wanachama watapata fursa ya  kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2017, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2018-2019.

 

Mkutano huo utakaoanza saa 2:00 Asubuhi katika ofisi za chama zilizoko Sinza Mori, Dar es Salaam, utatanguliwa na mafunzo siku ya Ijumaa tarehe 13th April mwaka huu ambapo Afisa Mwandamizi Maudhui ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya TAMWA na miongoni mwa wanamke wa kwanza kupiga picha za Luninga Tanzania Bi Raziah Mwawanga atapata fursa ya kueleza jinsi Wakfu wa Vyombo vya Habari (Tanzania Media Foundation-TMF) ilivyowajengea uwezo wanahabari wanawake kuboresha taaluma yao na kuandika habari zinazoleta uwajibikaji katika jamii kwa kuzingatia jinsia , pamoja na kupokea maoni ya wananchama wa TAMWA juu ya uboreshaji wa mpango mkakati wa TMF ujao.

 Baada ya majadiliano hayo kutoka TMF, mmoja wa waasisi wa TAMWA ambaye ni Mkurugenzi Mkazi, Mradi wa Uzazi wa Mpango Johns Hopkins, Kitengo cha mpango wa Mawasiliano Dar es Salaam, Bi Halima Shariff atazungumzia nafasi ya mwanamke katika taaluma ya habari pamoja na kujadili jinsi ambavyo  mitandao ya kijamii inapunguza au kuendeleza ukatili na unyanyaswaji wa kijinsia hapa nchini.

 Majadiliano hayo aidha yatatoa fursa kwa TAMWA na TMF kujenga nguvu ya pamoja katika kuwajengea uwezo wanahabari wanawake kitaaluma hasa katika kuandika habari za kuelimisha jamii juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na jinsi yanavyozorotesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa familia na taifa zima.   

 Mkutano mkuu wa TAMWA ni wa 30 tangu kuanzishwa chama hicho na  ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.

Edda Sanga,

Mkurugenzi Mtendaji

Read 5889 times Last modified on Friday, 13 April 2018 10:51

412 comments

  • Comment Link Anunturi si Stiri Online Monday, 29 June 2020 20:29 posted by Anunturi si Stiri Online

    Cele mai bune pentru știri, sport, showbiz, celebrități

  • Comment Link Apabigh Monday, 29 June 2020 09:54 posted by Apabigh

    sofosbuvir daclatasvir effets secondaires daclatasvir daclatasvir 60 mg prix acheter daclatasvir acheter daklinza https://achetermedic.com/acheter-daklinza-france-fr.html - acheter daclatasvir commander daklinza

  • Comment Link Gordon Saturday, 27 June 2020 22:18 posted by Gordon

    Hello there, I think your web site might be having web browser compatibility issues. Whenever I take a look at your web site in Safari, it looks fine but when opening in IE, it has some overlapping issues. I merely wanted to provide you with a quick heads up! Aside from that, fantastic site!|

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

5202731
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
6312
14051
54382
98794
272312
5202731

Your IP: 46.229.168.133
2020-07-09 09:53

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER