Tuesday, 06 February 2018 10:51

TAMWA YAUNGANA NA WADAU NCHINI KUADHIMISHA SIKU YA UKEKETAJI DUNIANI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2018,  kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.

 Maadhimisho haya yanaenda sambamba na kauli mbiu ya “Kufanya kazi pamoja kuongeza nguvu ya kumaliza Ukeketaji katika Kizazi Kipya” ambayo inaitaka jamii kushirikiana pamoja kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ukiwemo ukeketaji.

 

 Kwa mujibu wa utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto (TDHS-MIS) mwaka 2015-16, umeeleza kuwa mwanamke mmoja kati ya kumi amekeketwa ambapo aina ya ukeketaji maarufu ni ile ya kukata nyama na kuiondoa kwa asilimia 81 licha ya elimu ya madhara ya ukeketaji kutolewa kwa jamii.

 Utafiti huo umebaini kuwa, uelewe kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadri  kiwango cha elimu kinavyoongezeka kutoka asilimia 71 ya wanawake  wasiokuwa na elimu hadi kufikia asilimia 97 ya wenye elimu ya sekondari na zaidi. Aidha, utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha wanawake wenye umri kati ya miaka 15-29 waliokeketwa kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwaka 2015.

 TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapata elimu endelevu ya kuondokana na mila kandamizi kwakua zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake kwa kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa  na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia.

 Aidha TAMWA inaamini kuwa endapo vyombo vya habari vitaendelea kutoa elimu ya kuondoa ukeketaji, itasaidia kupunguza ukatili huo kwani vina nguvu katika kuleta mabadiliko ya jamii ikiwemo kuondokana na ukeketaji na aina zote za ukatili wa kijinsia.

 Edda Sanga

 

Mkurugenzi Mtendaji.

Read 15495 times Last modified on Tuesday, 06 February 2018 11:07

577 comments

  • Comment Link Madeline Saturday, 16 May 2020 12:10 posted by Madeline

    Greetings from Colorado! I'm bored to tears at work so I decided to browse your blog on my iphone during lunch break. I enjoy the info you provide here and can't wait to take a look when I get home. I'm shocked at how quick your blog loaded on my phone .. I'm not even using WIFI, just 3G .. Anyways, wonderful blog!|

  • Comment Link Phylis Friday, 15 May 2020 16:28 posted by Phylis

    I do not even know how I stopped up right here, but I thought this put up was great. I don't know who you are however definitely you're going to a well-known blogger in the event you are not already. Cheers!|

  • Comment Link Leopoldo Servano Monday, 11 May 2020 05:20 posted by Leopoldo Servano

    Hello , I always read your nice blog posts and i really trust you , can you pleas tell me is this money making method effective ? ==> https://cutt.us/shSaR it is cheap making money method but i have limited budget and i am afraid , pleas tell me about it , waiting your reply , thanks again for your nic posts

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.

VISITORS COUNTER

4830836
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
5495
6612
5495
238179
81971
4830836

Your IP: 5.18.235.239
2020-05-31 21:57

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER