Print this page
Thursday, 06 February 2020 15:08

VIJANA WANA MCHANGO KUTOKOMEZA UKEKETAJI

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Na Mwandishi Wetu, TAMWA.

Februari 6 kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji. Kihistoria  siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 2003 baada ya  Baraza la Umoja wa Mataifa kuidhinisha  rasmi maadhimisho ya  kupinga Ukeketaji duniani.

 

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: Nguvu ya vijana katika kumaliza ukeketaji. Ripoti ya Utafiti wa Demografia na Afya hapa nchini ( TDHS 2016) inaonyesha kuwa wanawake wengi wanaokeketwa wana umri wa kati ya miaka 15 na 49 ikimaanisha kuwa vijana ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili.

Hivyo basi katika kuadhimisha siku hii Chama cha Wahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinahimiza ushiriki wa vijana katika kumaliza au kupunguza vitendo vya ukeketaji nchini.

TAMWA inawahimiza vijana kukataa kuwa watunza siri za matukio ya ukeketaji bali watoe elimu juu ya athari za ukeketaji pamoja na kufichua matukio hayo yanapopangwa katika maeneo wanayoishi.

Sasa umefika wakati wa vijana kupinga ukeketaji kwa nguvu zote ili kutokomeza vitendo hivi.

Read 854 times Last modified on Thursday, 06 February 2020 19:00
TAMWA

Latest from TAMWA

19 comments