Wafanyakazi pamoja na wajumbe wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania TAMWA wakutana kujadili mpango mkakati

Wafanyakazi pamoja na wajumbe wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania TAMWA wamekutana tarehe 31 July 2015 na 01 Aug 2015 kuweza kujadili mpango mkakati wa kipindi cha miaka mitano ijayo 2015 - 2020.

Mkutano huo ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano Ledger Bahari Beach Hotel ulikuwa na lengo la kuboresha na kuweka misingi imara na mathubuti zaidi ya chama.

Read more...

MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI : FEBRUARY 22,2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kwa kushirikian na Shirika linalo hudumia Idadi ya Watu UNFPA Kinatoa mafunzo ya siku tatu kuhusiana na kuandika habari za uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia.Mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa habari mapema tarehe 23 hadi Tarehe 25 Februari mwaka huu katika kanda tatu nchini Tanzania.

Mafunzo katika kanda ya Kaskazini yatajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara Tanga na Kilimanjaro na yatafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika Kanda ya Kati, waandishi wa habari watatoka mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora ambapo mafunzo yatafanyika mjini Singida. Mafunzo katika Nyanda za Juu Kusini yatajumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma na yatafanyika mjini Iringa.

Read more...

SIKU YA UKEKETAJI MKOANI SINGIDA:FEBRUARY 06,2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMWA KUAZIMISHA SIKU YA UKEKETAJI MKOANI SINGIDA LEO

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 mwezi wa pili, 2015 saa 2:00 asubuhi kuadhimisha siku ya Kitaifa ya kupinga ukeketaji duniani ambayo mwaka huu kilele kitafanyika mkoani Singida.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Katala Beach Hotel (KBH) mjini Singida yanahusisha mikoa yote iliyoathirika na ukeketaji ili kuunganisha nguvu za wabunge, wakuu wa mikoa, polisi, mahakimu, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirkia ya kimaendeleo, wahanga wa vitendo hivyo, wanafunzi, walimu, wazee wa mila pamoja na ng’ariba ili kuweka mikakati ya kuondoa ukatili huo kutoka asilimia 15 hadi sifuri.

Read more...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI :DECEMBER 01,2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SIKU YA UKIMWI DUNIANI IADHIMISHWE KWA KUPINGA UKATILI KIJINSIA

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kinaungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo hufanyika tarehe 1 Desemba kila mwaka, kikiitaka jamii kuvichukulia hatua vitendo vya unyanyasaji kijinsia ambavyo huchangia ongezeka la maambukizi ya Virusi Vinavyosababisha UKIMWI (VVU).

Miongoni mwa ukatili unaochangia ongezeko la VVU ni pamoja na ubakaji, wanawake kurithiwa, watoto wa kike kulazimishwa kuolewa na ukeketaji vitendo ambavyo hufanyika kwa wawanamke na watoto kwa kulazimishwa bila kujali hiari ya mtu husika.

Read more...

VISITORS COUNTER

4772884
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
5878
4523
10401
180227
81971
4772884

Your IP: 5.18.235.239
2020-05-25 22:53

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER