TAMWA YAUNGANA NA WADAU NCHINI KUADHIMISHA SIKU YA UKEKETAJI DUNIANI
Written by TAMWAChama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2018, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.
Maadhimisho haya yanaenda sambamba na kauli mbiu ya “Kufanya kazi pamoja kuongeza nguvu ya kumaliza Ukeketaji katika Kizazi Kipya” ambayo inaitaka jamii kushirikiana pamoja kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ukiwemo ukeketaji.
SIKU YA KIMATAIFA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI 19 NOVEMBA, 2017
Written by TAMWAMatukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.
Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.25 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50 hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.
TAMWA KUADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Written by TAMWAChama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Uzinduzi wa maadhimisho hayo yataanza kesho tarehe 25 Novemba na kufikia kilele tarehe 10 Desemba, 2017. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Funguka! Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Haumuachi Mtu Salama. CHUKUA HATUA”, kauli mbiu hii inatukumbusha wote wazazi, walezi, ndugu, jamaa na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali kuvitolea taarifa na kuvichukulia hatua stahiki vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na hasa watoto wa kike ambao wanakumbana na vishawishi na vizuizi ambavyo aghlab husababisha ndoto zao kutotekelezeka.
HOTUBA YA UFUNGUZI WA MAONESHO YA MIAKA 30 YA TAMWA 14th Nov. 2017
Written by TAMWANdugu Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini TAMWA,
Mkurugenzi wa TAMWA,
Board ya TAMWA
Wanachama wa TAMWA
Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali.
Habari za asubuhi!
Nafurahi kuwepo na ninyi hapa leo katika ufunguzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TAMWA. Hongera sana Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA
Pia pokeni salamu nyingi kutoka kwa wafanyakazi wote wa ITV/Radio One !
Tarehe 16 Julai, 2018,Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA),lina Ujumbe Kutoka Jumuia ya Umoja Ulaya (EU) kwa Tanzania Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Ireland, Ubalozi wa Uholanzi, pamoja na ubalozi wa Kanada kwa pamoja watakuwa wenyeji wa shughuli ya kuonesha juhudi zinazohitajika katika kukomesha suala la ukeketaji hapa nchini. Katika tukio hilo Kutakuwa na hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na Watoto. Pia kutakuwa na Hotuba ya mwakilishi wa Jeshi la polisi Tanzania na wanaharakati wa haki za binaadamu pia kutakuwa na uzinduzi wa filamu mpya yenye hadi ya kimataifa inayoitwa “In the Name of Your Daughter”,. Baadsa ya filamu hiyo kutakuwa na wasaa wa maswali na majibu kutoka kwa washiriki wa tukio hilo.
On 16 July, 2018,the United Nations Population Fund (UNFPA),the Delegation of the European Union (EU) to Tanzania and the East African Community (EAC), the British High Commission, the Embassy of Ireland, the Embassy of the Kingdom of the Netherlands, and the High Commission of Canada will host an event to highlight the intensified efforts that are needed to end female genital mutilation (FGM) in the country. The event will include remarks by the Government of the United Republic of Tanzania represented by the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and the Tanzania Police Force, as well as human rights activists, and the screening of the internationally acclaimed film “In the Name of Your Daughter”, followed by a Question and Answer (Q&A) Session with the audience.
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kimefadhaishwa na kinalaani vikali vitendo vya mauaji vinavyoendelea kutekelezwa na baadhi ya wanandoa kwa makusudi na kuwanyima haki ya kuishi wenza wao kwa kuwaua kinyama kwa sababu ya wivu wa mapenzi.
Zaidi ya Wanachama 150 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA, Jumamosi tarehe 14th April, 2018 wanafanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine, wanachama watapata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2017, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2018-2019.
MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA
Written by TAMWAMtandao wa wadau kutoka Asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania, tunapenda kumpongeza na kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Pombe Magufuli kwa kuguswa na kutoa maagizo kunapo kuwa na matukio ya ajali za barabarani yanayotokea nchini ambayo yamekuwa na athari nyingi kiuchumi na kijamii.
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA leo, kinaungana na mashirika yote nchini yanayotetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.
Maadhimisho haya yanabeba kauli mbiu ya kitaifa inayosema “Wakati ni sasa: Wanaharakati Mijini na Vijijini kubadilisha maisha ya wanawake”, ambayo inatutaka wote tushirikiane kikamilifu kubadilisha maisha ya wanawake kwa kuondokana na ukatili wa kijinsia ili kupanua wigo wa fursa za usawa kiuchumi kwa wanawake.