Friday, 24 November 2017 12:36

TAMWA KUADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Written by

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

 Uzinduzi wa maadhimisho hayo yataanza kesho tarehe 25 Novemba na kufikia kilele tarehe 10 Desemba, 2017. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Funguka!  Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Haumuachi Mtu Salama. CHUKUA HATUA”, kauli mbiu hii inatukumbusha wote wazazi, walezi, ndugu, jamaa na jamii kwa ujumla kushirikiana na serikali kuvitolea taarifa na kuvichukulia hatua stahiki vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na hasa watoto wa kike ambao wanakumbana na vishawishi na vizuizi ambavyo aghlab husababisha ndoto zao kutotekelezeka.

 TAMWA kupitia kitengo chake cha Usuluhishi cha CRC, kimebaini kuwa ukatili wa kijinsia hasa ubakaji umeongezeka kwa watoto kwani katika kipindi cha miezi minane  kuanzia Mwezi Januari hadi Augusti mwaka 2016 kesi zilizohudumiwa katika kituo hicho zilikuwa ni 9 wakati kwa kipindi kama hicho hicho mwaka huu 2017 vitendo vimeongezeka na kufikia 57 kwa vigezo vyovyote vile, ukatili unatisha.

 Taarifa ya tathimini ya utendaji kazi ya Kituo cha One Stop Centre cha Hospitali ya Amana, Dar es Salaam imeonesha kiwango cha ubakaji kwa mwaka huu kiko juu kwa idadi ya watoto 141 walio chini ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na idadi ya watu wazima 27.

Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa kuanzia Julai 2016 hadi Juni 2017 wanawake 168 walibakwa. Kituo hicho pia kimehudumia jumla ya waathirika 420 ambapo kati ya hao watoto ni 316 sawa na asilimia 75 na watu wazima ni 104 sawa na asilimia 25 ya ukatili wa kijinsia.

 Taarifa hiyo aidha imeonyesha kuwa idadi ya waliolawitiwa na kuripoti katika kituo hicho ni 44 sawa na asilimia 10.47 kati ya hao watoto ni 39 ukilinganisha na watu wazima ambao ni 5 kwa mwaka. Hali hii ya ukatili iko juu sana kwani watoto waliofanyiwa vitendo hivi wana uwezekano mkubwa wa kuwafanyia wengine katika kipindi cha makuzi yao.

 TAMWA inaamini kuwa jukumu la ulinzi na malezi bora kwa watoto ni la jamii nzima wakiwemo marafiki, wazazi, ndugu, walezi, majirani na viongozi tukishirikiana na serikali kuboresha na kusimamia utekelezaji wa sera na kubadilisha sheria kandamizi ili wahusika wa ukatili huu hasa kwa watoto wa kike wawajibishwe kwa mujibu wa sheria. 

 Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia ni kampeni  ya Kimataifa  inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 kutokana na mauaji ya kinyama ya kina dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960. Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 iwe siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa Desemba 10 ya kila mwaka.

 

 Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji

Matukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea.

 Takwimu zinaonyesha  kuwa takribani watu milioni 1.25 duniani hufariki kila mwaka kutokana na  ajali za barabarani, aidha,  watu milioni 20 mpaka 50 hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na  madhara ya ajali hizi zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.

 Takwimu pia zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea sababu ya makosa ya kibinadamu hasa uzembe wa madereva ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi, nchini Tanzania asilimia 76% ya ajali barabarani husababishwa na uzembe wa madereva, asilimia 8% husababishwa na ubovu wa barabara. Aidha ubovu wa vyombo vya moto husababisha ajali kwa asilimia 16%.

 Hata hivyo ajali nyingi zinaepukika kama madereva na watumiaji wengine wa barabara watazitii sheria na kanuni  za Usalama barabarani.

 Kutokana na ajali hizo kuongezeka ndio maana ikatengwa siku maalum ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani kila mwaka ambayo huadhimishwa kila ifikapo Jumapili ya tatu ya Novemba ya kila mwaka. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Ifikapo 2020: Kupunguza vifo na ajali za barabarani kwa asilimia 50%”.

 Siku hii inatambulika kama siku rasmi ya kimataifa ya kuwakumbuka waathrika wa ajali hizo na familia zao na kuzitaka nchi wanachama pamoja na jumuiya za kimataifa kuitambua siku hiyo.

 Pia siku hiyo hutoa fursa kwa jamii nzima kukutana na kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani ,kutafakari madhara, gharama, na hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kuzuia ajali zisitokee. Vilevile siku ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani inatoa nafasi kwa wadau kuikumbusha serikali wajibu wake na jamii nzima katika suala la kuzifanya barabara kuwa sehemu salama kwa kila mmoja.

 Hivyo basi mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani pamoja na mambo mengine katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo

 

Maeneo ndani ya sheria ambayo mtandao huu utajielekeza kuona sheria inafanyiwa mabadiliko/maboresho ni pamoja na;

 

a)      Matumizi ya mikanda na vizuizi vya watoto; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.

 Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu.

Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.

 Kadhalika sheria yetu ya sasa ipo kimya juu ya suala la vizuizi vya watoto katika vyombo vya moto hasa Kwa magari binafsi (private cars) na tumeendelea kushuhudia madhara makubwa katika ajali zilizohusisha watoto vikiwemo vifo.  

b)      Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemii chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho. 

Vilevile pamoja na kuanishisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutovaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa na kwa usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.

c)      Matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva  mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.

d)     Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisiszokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.  Mfano Sheria  ya usalama barabarani ya 1973 Kifungu cha 51(8) inatambua maeneo machache katika kuzuia mwendokasi, ni muhimu Sheria itamke maeneo yote na si yale ya mjini tu au makazi, itamke wazi kuhusu maeneo ya shule, nyumba za ibada, maeneo ya michezo na mbuga za wanyama.

Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaokufa katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii. Tunatoa wito kwa watunga sera na wabunge kuwalinda wapiga kura wao dhidi ya ajali na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani kwa kuunga mkono na kupitisha marekebisho ya sheria ya usalama barabarani ya 1973.

 

TAMKO HILI IMETOLEWA LEO NA MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA: TAWLA, TAMWA, WLAC, TCRF NA TLS.

Friday, 19 May 2017 14:55

TAMWA YAMLILIA DR. SUBILANGA KAGANDA

Written by

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kimepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Madaktari Tanzania (MEWATA)

Dr. Subilanga Kaganda kilichotokea Jumatano tarehe 17/05/2017 huko APPOLLO nchini INDIA.

 Kifo cha Dr. Kaganda kimeacha pengo kubwa ambalo halitasahaulika kamwe kwani alikuwa mtetezi mahiri, shujaa aliyefanya kazi kwa upendo, huruma na weledi usio kifani na alijipambanua kuwasaidia wanawake wa hali zote dhidi ya saratani ya mlango wa uzazi na matiti ambazo zimekuwa kero kwa wanawake wengi mijini na vijijini hapa nchini.

 TAMWA inaungana na Watanzania wengine kutoa pole katika kipindi hiki kigumu kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, madaktari na wanachama wote wa MEWATA.

 Aidha wakati TAMWA tukiwasihi familia, ndugu, jamaa na wanachama wa MEWATA waupokee msiba huu KWA UNYENYEKEVU na UTULIVU, tunaomba wamshukuru mwenyezi Mungu kwa muda wote aliowapa kuishi na kushirikiana na marehemu katika harakati mbalimbali za kijamii,tunaomba pia wanachama wa MEWATA waendeleze juhudi za marehemu pale alipoachia na Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu.

 Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, na ampe raha ya milele marehemu, apumzike kwa amani, AMEN

 

 Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji

Mapendekezo ya Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani kwa mtazamo wa visababishi vitano vya ajali

Mtandao wa wadau kutoka Asasi za Kiraia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera inayohusu Usalama Barabarani Tanzania, umeungana na watanzania katika Maadhimisho ya Nne ya Umoja wa Mataifa ya Wiki ya Usalama Barabarani (UN Road Safety Week) yalionza tarehe 08/05/2017 na kufikia kilele chake tarehe 14/05/2017. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Udhibiti wa Mwendo Kasi kwa Vyombo vya Usafiri”.

Wakati tunaadhimisha Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani, tumeshuhudia matukio mbalimbali ya ajali ambazo chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Mfano mmojawapo ni ule wa tukio la tarehe 6 Mei mwaka huu, ambapo taifa letu  lilipatwa na simanzi, pale wanafunzi 33 na walimu wao wawili pamoja dereva walipata ajali na kufariki papo hapo katika wilaya ya  Karatu, Mkoani Arusha.

Kama sehemu mojawapo ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani, Mtandao wa wadau kutoka Asasi za Kiraia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera inayohusu Usalama Barabarani Tanzaniasiku ya tarehe 12 na 13 Mei, 2017 wamefanikiwa kukaa na baadhi ya Wabunge kutoka kamati saba za Bunge. Kamati hizo ni Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Katiba na Sheria, Kamati ya Bajeti, Huduma za Jamii,  Kamati ya Sheria Ndogo, Viwanda na Biashara pamoja na Kamati ya Miundombinu.

Vikao na Kamati hizo viliongozwa chini ya Uenyekiti wa Mwenyeketi wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mbunge wa Muheza. Katika Vikao hivyo Wabunge  walionyesha dhamira kubwa na kuunga mkono mapendekezo ya kuboresha usalama bararani kwa maendeleo ya Taifa letu.

Wajumbe wa Kamati hizi walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani. Kwa mujibu wa moja ya mada hizo iliyyoelezea hali ilivyo sasa, ilielezwa kuwa madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.25 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani. Wakati huo huo, watu zaidi ya milioni 20 hadi 50 wamebaki na majeraha makubwa na au ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizo kwa mwaka. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2015.

Kwa mujibu ya ripoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2015. Jumla ya ajali 5,152 ziliripotiwa kwa Jeshi la Polisi kuanzia Januari hadi Juni 2016. Pia takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani Nchini.

Aidha kwa upande wa Tanzania Bara, taarifa kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha  Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016  jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.  Katika vifo hivyo  wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676.  Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati  yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo yalisababisha ajali 3,649 ikifuatiwa na pikipiki zilizosababisha ajali 2,544

Kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini, Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera zinazohusu usalama barabarani Tanzania  umeona  umuhimu na kuchukulia jambo hili na kulifanyia kazi kwa kina. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 76 ya ajali zote zinatokana na vyanzo vya kibinadamu kama vile Ulevi, Mwendokasi, Uzembe, Uchovu, kupuuzia au kutokuwa makini uwapo barabarani na kutokutii sheria za Usalama Barabarani. Tuna amini matendo haya ya kibinaadamu yanadhibitika kisheria, hivyo basi tunaisihi serikali kuboresha sheria.

Kama wadau wa Usalama Barabarani, tunadhani kuna umuhimu wa sheria sasa kuboreshwa, na hivyo utashi wa kisiasa unatakiwa.  Ndiyo maana tukaitisha majadiliano ya pamoja na Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko ya sheria kwa ufanisi na kwa haraka. 

Umoja wa mataifa na Shirika la Afya Duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii. Katika muda wa miaka mitatu iliyopita Nchi karibia 17 zinazowakilisha wananchi milioni 409 zimetunga na kufanyia maboresho ya sheria angalau kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndio vyanzo vikubwa vya ajali na Nchi hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika kudhibiti ajali. TanZania si miongoni mwa nchi hizo. Ni muda mwafaka sasa Tanzania kuchua hatua kwa matendo.

Wabunge waliohudhuria vikao hivi kwa ujumla wao waliona umuhimu wa kuwa na mikakati ya kitaifa ya kupunguza ajali na walionyesha nia na kukubali kuunda Mtandao wa Wabunge wanaotetea usalama barabarani.

Maeneo ambayo tunayapa kipaumbele katika maboresho ya sheria ni kama haya yafuatayo:

a)     Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu.

Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari.

b)    Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemi chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho. 

Vilevile pamoja na kuanisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutokuvaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa  kwa usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.

c)     Ulevi: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani na kupendekeza kiwango cha asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva  mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.

d)    Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili limeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisizokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.

 Tunatoa wito kwa watunga sera kushirikiana zaidi na wadau kuuelimisha umma katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo.

TAMKO HILI LIMETOLEWA LEO NA MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA:

 1. TAWLA
 2. TAMWA
 3. WLAC
 4. TCRF
 5. TLS
 6. TMF
 7. RSA
 8. AMEND TANZANIA
 9. SHIVYAWATA
 10. TABOA &
 11. SAFE SPEED FOUNDATION

 

On the occasion of United Nation Road Safety Week (08/05 – 14/05/2017)  with the theme of Save Lives: #SlowDown” TAMWA joins with all Tanzanians and road safety stake holders to call for government reforms of the road safety legal and policy environment in the country specifically the Road Traffic Act of 1973.

The reforms should address identified risk factors in road safety which is not well addressed in our current law, therefore over speeding, drinking and driving, non use of seat belts, helmets and child restraints continue to be major causes of deaths and severe injuries.

TAMWA calls for stronger road safety laws as a matter of urgency given the number of road crash deaths which occur at an alarming rate in the country.

As we commemorate the 4th United Nations global road safety week we have continued witnessing number of road crashes which have taken lives of our loved ones, this trace us back to the fatal crash happened last week on May 6, 2017 in Arusha resulting to the death of 32 pupils, two teachers and a driver .

 According to Tanzania human rights report of 2016, road crashes showed a slight decrease in the first half of 2016 compared to the same period in 2015. A total of 5,152 crashes were reported to the police from January to June 2016. However, statistics show that average of 3000 lives are lost each year to road crashes. Globally, every year 1.25 million people die due to road crashes. Additionally 20 and 50 million people suffer non-fatal injuries with many incurring a disability as a result of their injury.

 By adopting and enforcing good road safety laws, Tanzania can significantly reduce the road carnage and the emotional and economic toll these deaths and injuries take on families.

TAMWA realises that a lot of women and children bear the brunt of road crashes, although data on direct victims of road safety shows that men are the most affected. In actual fact women and children are strongly affected through loss of income and the need to care for seriously injured family members.  By strengthening road safety laws for all road users, we can help to make our villages, towns and cities safe. Every action we take, as drivers or as passengers, can change the outcome of a journey and the future of families.

Edda Sanga, Executive Director of TAMWA stated “The United Nations and the World Health Organization acknowledge that strong road safety laws are effective in reducing the number of people killed on our roads. Tanzania must have strong road safety laws to stop this public health crisis. Also in the last three years, 17 countries representing 409 million people have amended their laws on one or more key risk factors for traffic injuries to bring them into line with best practice, Tanzania is not one of them.  It is time for Tanzania to take the action”.

 

Edda Sanga

Executive Director

Chama cha wanahabari wanawake tanzania -TAMWA kinaungana na watanzania katika maadhimisho ya nne ya umoja wa mataifa ya wiki ya usalama barabarani (UN Road Safety week) yatakayoadhimishwa kuanzia tarehe 08/05 na kufikia kilele tarehe 14/05. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “udhibiti wa mwendo kasi kwa vyombo vya vya usafiri”

 TAMWA inawaasa wadau wa usalama barabarani wakiwemo Wabunge  kuadhimisha wiki hii kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani hasa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi,  ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto.

 Kutokana na idadi kubwa ya vifo na ajali  barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara.

 Wakati tunadhimisha wiki ya umoja wa mataifa ya Usalama Barabarani, tumeshuhudia matukio mbalimbali ya ajali ambayo chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Mfano wa tukio ni la tarehe 6 Mei, wiki iliyopita ambapo watanzania walipatwa na simanzi pale ambapo wanafunzi 32 na waalimu wao wawili pamoja dereva walivyopata ajali na kufariki papo kwa papo.

 Madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ambapo inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.25 hufa kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.Wakati huo huo watu zaidi ya milioni 20 hadi 50 wamebaki na majeraha makubwa na aidha ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi kwa mwaka.

Kwa mujibu ya repoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2015 ambapo jumla ya ajali 5,152 ziliripotiwa kwenye Jeshi la Polisi kuanzia Januari hadi Juni 2016. Pia takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani Nchini.

Edda sanga, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii . Lakini pia kwa mda wa miaka mitatu iliyopita Nchi karibia 17 zinazowakilisha wananchi milioni 409 zimetunga na kufanyia maboresho ya sheria angalau kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndio vyanzo vikubwa vya ajali na Nchi hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika kudhibiti ajali, ila Tanzania haipo miongoni mwa nchi hizo. Ni mda mwafaka sasa Tanzania kuchua hatua kwa matendo”.


Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini kinaungana na mashirika ya kihabari nchini kote kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ulimwenguni ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 3 Mei ambapo mwaka huu kitaifa yatafanyika mjini Mwanza.

Maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu yake mwaka huu ni “Fikra Yakinifu kwa wakati Muhimu; Jukumu la Vyombo vya Habari katika kuendeleza Jamii zenye Amani, Haki Jumuishi” TAMWA imewataka wanahabari kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi hasa katika kuhakikisha wanazingatia usawa katika kutoa taarifa mbalimbali zikiwemo zile zinazohusu wanawake,watoto na wanaume.

Aidha katika maadhimisho ya mwaka huu, TAMWA inawapongeza wanahabari na vyombo vya habari nchini kwa jinsi vinavyoshirikiana katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatolewa taarifa bila woga na wahusika wanachukuliwa hatua stahiki kwakua vitendo hivyo huchangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

TAMWA katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto, kwa kipindi cha mwaka 2015 na 2016 wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2,350 na wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsi ya kuandika habari za ukatili wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali.

TAMWA katika kutekeleza mradi wake wa GEWE II kimeweza kuhunda kamati za kuelimisha jamii jinsi ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya kumi za Tanzania na Bara na visiwani ambazo zinawahusisha wanahabari ili kuziwezesha jamii kushirikiana na vyombo vya habari kuweza kuvitolea taarifa vitendo hivyo bila woga ambapo kamati hizo zimesaidia kuibua matukio hayo.

TAMWA inaamini kuwa kupitia maadhimisho haya wanahabari kote nchini watafanya kazi zao kwa weledi na uaminifu na kuandaa habari zenye usawa wa pande zote husika pamoja na kuibua mambo yanayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo ili yafanyiwe kazi pia kujihepusha na habari ambazo kwa sehemu zinaweza kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao wenyewe au wananchi katika taifa la Tanzania.

Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji - TAMWA

Thursday, 16 March 2017 17:22

SERIKALI IUNDE SERA KWA MATUMIZI YA POMBE

Written by

Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kupiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe hasa zile zilizofungwa kwenye mifuko aina ya viroba ziambatane na uundwaji wa sera ya pombe ya Taifa itakayosaidia katika kudhibiti matumizi ya vilevi hapa nchini.

 

Sera ya hiyo  italazimisha sheria zinazoambatana  kurekebishwa ambapo pia zitawawezesha wafanyabiashara, watengenezaji na wauzaji wa kinywaji hicho kutambua haki, madhara na makosa yao mapema katika utoaji  huduma, na hiyo    itaisaidia serikali katika usimamizi madhubuti, na mwenendo wa udhibiti utakuwa wazi  tofauti na  sasa ambapo serikali imeamua kupiga marufuku kwa kushtukiza, jambo ambalo  limepelekea   kuleta madhara kwa wafanyabiashara ambao kwa namna moja au nyingine hawakuwa wanajua madhara yake.

 

Matumizi ya pombe aina ya viroba hayana budi kuwekewa sera, na sheria ziboreshwe hasa juu ya matumizi kwani yanachangia madhara makubwa ya kiafya kwa jamii  pamoja na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, migogoro majumbani, utelekezaji wa familia, ubakaji, ajali barabarani na pengine kuharibu nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla

 

Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA, kupitia kupitia kituo chake cha usuluhishi (CRC), kimekuwa kikiomba uwepo wa sera ya Taifa juu ya matumizi ya Pombe nchini kama ilivyo nchini Kenya na Uganda, aidha kimekuwa kikitoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya pombe kupita kiasi ambapo kwa mwaka 2016 kiliweza kuwapa ushauri nasihi wananchi wapatao 490, kati ya hao wanawake walikuwa 355, wanaume 92 na watoto walikuwa 45 walioathirika kwa namna mbalimbali kutokana na unywaji pombe kupindukia.

 

 

Edda Sanga

Mkurugenzi Mtendaji

Iringa Stakeholders of 2015 General Elections have said that media failed to report enough stories from women, youths and people living with disabilities during the 2015 general elections. They associated the less media coverage of these groups to several reasons include lack of confidence to deal with media, low skills on media engagement, stigmatization of PWDs and corruption in the election process which twisted media to cover some candidates from these groups in negative ways.

 

Aspirants/candidates from these groups were also lacking enough financial capacity to support election campaigns including engaging with the media.

 

They suggested that to address the challenges of women, youth and PWDs aspirants/candidates less media coverage in the future, TAMWA should continue to conduct trainings to marginalized groups before elections on how to use media for campaign.

 

TAMWA should also collaborate with government to provide civic education on the rights to vote and be voted. It should also work closely with journalists to remind them their professional ethics to avoid bribes and negative coverage of marginalized groups.

The workshop held on 23rd December 2016 which brought 30 participants (16 female, 14 male) was attended by journalists, editors, bloggers, former candidates and elected leaders.


Edda Sanga

Executive Director

TAMWA

 

Wadau wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 mkoani Iringa wamesema kuwa vyombo vya habari vilishindwa kuripoti habari za kutosha kutoka makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015. Walihusisha suala hilo na sababu kadhaa ikiwemo watangaza nia au wagombea kutoka makundi hayo kushindwa kujiamini kuzungumza katika vyombo vya habari, kukosa maarifa ya kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya habari, unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu na rushwa katika mchakato mzima wa uchaguzi ambayo ilisababisha vyombo vya habari kuripoti taarifa hasi za watangaza nia au wagombea kutoka makundi hayo.

 

Watangaza nia au wagombea kutoka makundi maalum pia walikosa uwezo wa kifedha katika kampeni zao ikiwa ni pamoja na fedha za kutumika katika kujenga mahusiano na vyombo vya habari.

 

Walipendekeza kuwa ili kushughulikia changamoto hizo zinazowakabili wanawake, watu wenye ulemavu na vijana inabidi TAMWA kuendelea kutoa mafunzo ya watangaza nia au wagombea kutoka makundi maalum ya jinsi ya kutumia vyombo vya habari wakati wa uchaguzi. Wamependekeza pia TAMWA kushirikiana na serikali kutoa elimu ya mpiga kura ili wanajamii wafahamu haki zao za kupiga na kupigiwa kura. Pia wametaka TAMWA kufanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari ili kuwakumbusha maadili ya uandishi ili kuondokana na rushwa na kutoa taarifa hasi dhidi ya makundi maalum.

Warsha iliyofanyika Disemba 23 2016 mjini Iringa ilihudhuriwa na washiriki 30 (wanawake 16, wanaume 14) kutoka makundi ya waandishi wa habari, wahariri, waandishi wa blogu, watangaza nia, wagombea na viongozi wa kisiasa kutoka mkoani Iringa kujadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti masuala ya wanawake wakati wa uchaguzi mkuu 2015.


Edda Sanga

Executive Director

Arusha Stakeholders of 2015 General Elections have urged media to increase their reporting of women aspirants/candidates in the future elections. The stakeholders attending workshop to disseminate media analysis report of 2015 General Elections produced by TAMWA under the support of UN Women said that most media outlets failed to report enough stories on women aspirants/candidates because they were more business oriented, hence their coverage focused on what would sale most.

 

The stakeholders also pointed out that some journalists demanded financial payment and other forms of favour from some of women aspirants/candidates to get their stories reported something which most women aspirants/candidates were not willing to give. In another observation they said that most women aspirants/candidates did not get enough media coverage because they lacked enough media engagement skills.

 

They suggested that to address the challenges of women aspirants/candidates less media coverage in the future, trainings should be conducted to Tanzania Editors Forums (TEF), Tanzania Press Clubs’ representatives from each region (both male and female), Tanzania Communication Regulatory Authority, media owners and Media Council of Tanzania to support women aspirants/candidates in the future elections. They also suggested continuing with joint seminars/dialogues between the media and politicians to create platforms for networking and building better relations.

The workshop held on 23rd December 2016 which brought 28 participants (17 female, 11 male) was attended by journalists, editors, bloggers, former candidates and elected leaders.


Edda Sanga

Executive Director

TAMWA

 

Wadau wa Uchaguzi Mkuu 2015 mkoani Arusha wamevitaka vyombo vya habari kuripoti zaidi masuala ya watangaza nia au wagombea wanawake katika chaguzi zijazo nchini.  Wadau waliohudhuria warsha ya kujadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti habari za wanawake wakati wa uchaguzi mkuu 2015 iliyotolewa na TAMWA kwa msaada wa shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) walisema kuwa vyombo vingi vya habari vilishindwa kuripoti habari za watangaza nia ama wagombea wanawake kutokana na kujikita zaidi katika biashara, na hivyo kuripoti zaidi habari wanazoona zinauzika zaidi wakati wa uchaguzi.

 

Wadau pia walisema kuwa baadhi ya wanahabari walitaka kupewa malipo ya aina fulani kutoka kwa baadhi ya watangaza nia au wagombea wanawake ili kuripoti habari zao jambo ambalo watangaza nia au wagombea hao wanawake walishindwa kulitekeleza. Pia walisema kuwa watangaza nia au wagombea wengi wanawake hawakupata nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kutokana na kukosa maarifa ya kutosha ya jinsi ya kutumia vyombo vya habari.

 

Walipendekeza ili kuondokana na changamoto hizo katika siku zijazo, kunapaswa kutolewa mafunzo ya kutosha kwa Jukwaa la Wahariri (TEF), Wawakilishi wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (wanawake na wanaume) kutoka mikoa yote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Baraza la Habari Tanzania, Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania ili kuunga mkono watangaza nia au wagombea wanawake katika chaguzi zijazo. Pia walipendekeza kuendelea na warsha za pamoja kati ya vyombo vya habari na wanasiasa kujenga majukwaa ya kimtandao na kujenga mahusiano mazuri.

Warsha ilifanyika Disemba 23 2016 na kuhudhuriwa na washiriki 28 (wanawake 17, wanaume 11) kutoka makundi ya waandishi wa habari, wahariri, waandishi wa blogu, watangaza nia, wagombea na viongozi wa kisiasa.

Edda Sanga

Executive Director

Page 3 of 5

VISITORS COUNTER

5209508
Today
Yesterday
This Week
This Month
Last Month
All days
13089
14051
61159
105571
272312
5209508

Your IP: 66.249.70.4
2020-07-09 20:35

OUR VIDEOS

FOLLOW US ON FACEBOOK

FOLLOW US ON TWITTER