Gallery

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania na kuratibiwana Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) kwa pamoja tunaungana na watanzania wote na Dunia kwa ujumla kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa ajali za Barabarani.

Siku hii huadhimishwa kimataifa, kila ifikapo Jumapili ya wiki ya tatu (3) ya mwezi Novemba kila mwaka Kwa ajili ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani na kuwaenzi mamilioni ya watu waliopoteza maisha na wengine wengi walioathirika kwa njia moja au nyingine kutoka na ajali hizo.

Kauli mbiu ya kimataifa kwa mwaka huu inasema; ‘Kumbuka, Saidia,Chukua Hatua’.

 

Ripoti (Taarifa) ya kimataifa juu ya usalama barabarani ya mwaka 2018, iliyozinduliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  inasema,  takribani  watu milioni 1.35 kila mwaka  hufariki kutokana na ajali za barabarani duniani huku  wengine milioni 20-50 kujeruhiwa kila mwaka. Kadhalika ripoti hiyo inasema, wahanga wengi wa ajali hizo ni vijana wenye umri wa kati ya  miaka 5-29.

Aidha, mtandao wa asasi za usalama barabarani wa,epokea taarifa ya muongo wa pili wa Umoja wa Mataifa katika kushughulikia masuala ya wanabari kwa kuongeza utendaji kazi kwa kuzingatia masuala ya kijinsia ambayo yamekuwa yakigusa jamii kubwa katika kuathirika zaidi jamii.

Kwa hapa Tanzania, ripoti zinaonyesha ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi kubwa inayofanywa na asasi za kiserikali na sizizo za kiserikali katika kutoa Elimu husika, Vyombo vya Habari na Wana Habari nchini pamoja na usimamizi wa kina wa vikosi vya usalama barabarani.

Kamanda na Afisa Mrakibu Msaidizi wa Polisi Deus Sokoni kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani alinukuliwa hivi karibuni akisema idadi ya ajali, vifo na majeruhi ikiwa ni pamoja na makosa ya usalama barabarani imepungua katika kipindi cha mwaka 2019 hadi 2020.

Aidha, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslimu katika mkutano wake na wanahabari mwanzoni mwa mwaka huu 2020 alisema kuwa mwaka 2017 ajali za gari zilikuwa 5578, mwaka 2018 ajali 3732 na mwaka 2019 ajali 2704. Hivyo basi   ‘Kwa mwaka 2019 ajali zimepungua kutoka  asilimia 35 hadi  asilimia 28 vifo kutoka  asilimia 31 hadi asilimia 19  na majeruhi kutoka  asilimia 32 hadia silimia 20.

Gharama za majeruhi wa ajali hizi duniani, inasaidikika kuwa kiasi cha dola za kimarekani 518 bilioni kila mwaka.

Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unao tetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo  usalama barabarani Tanzania, tunaamini kwamba  ajali hizi zinaepukika kama madereva, wananchi na watumiaji wengine wa barabara watazitii sheria na kanuni  za usalama barabarani.

Katika kuadhimisha siku hii muhimu Mtandao unaisihi serikali na watunga sheria kukubali na kupokea mawasilisho na mapendekezo ikiwa ni pamoja na kutunga/kurekebisha sheria za barabarani zina zoweza kupunguza kabisa ajali za barabarani.

  • Tunashauri kuendeleza kampeni za mara kwa mara  zinazo wakumbusha wananchi, wakiwamo watembea kwa miguu na madereva juu ya kujilinda na ajali za barabarani.
  • Tunasisitiza matumizi sahihi ya kofia ngumu, mikanda  na viti/vizuizi vya watoto katika magari ili kulinda usalama wetu na pia tukishauri zaidi madereva kuepuka mwendokasi.
  • Mtandao huu pia unahimiza watunga sera kuendelea kubuni sera zitakazo saidia ushiriki kamilifu wa mamlaka katika kudhibiti ajali za barabarani.
  • Kadhalika tuna shauri utafiti wa kina kufanyika baada ya ajali kutokea ili kujua namna ya kuzuia ajali hizo kutokea tena kwa namna hiyo siku za usoni.
  • Elimu itolewe kwa wanafunzi shuleni kwa ajili ya kuwapa elimu wanafunzi wajue namna ya kusoma alama za barabarani.

Mpaka sasa mtandao  wawadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania imewapa mafunzo  jumla ya wanahabari 142 (69 wanaume and 73 wanawake);Wahariri  47 (28 wanaume na 19 wanawake); pamoja na  wanahabari wa Mtandao wa kijamii 38 (wanaume 24 na wanawake 14)Tanzania.

TAMWA na Mtandao wa Usalama Barabarani, wanatoa RAI kwa serikali hii ya Awamu ya Tano inayoingia madarakani kwa miaka mingine mitano (5) kuhakikisha kuwa Sheria ya usalama Barabarani nchini (Road Traffic Act of 1973)inafanyiwa marekebisho kwa uharaka zaidi.

Tamko hili limetolewa leo Novemba 13, 2020 na mtandao wa asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania:

1. TAMWA

2. TAWLA

3. WLAC

4. TCRF

5. TLS

6. TMF

7. RSA

8. AMEND TANZANIA

9. SHIVYAWATA

10. TABOA

11. SAFE SPEED FOUNDATION

 

 

 

Search