Press Release

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimethibitishwa na kutangazwa kuwa Sekretarieti mpya ya Mtandao wa Ushiriki wa  Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Tanzania MET).

TAMWA imepewa jukumu hilo baada ya kufanyiwa tathmini na Shirika la Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Afrika MEA) mapema mwaka huu baada ya Mtandao huo nchini kuratibiwa na shirika la Child Diginity Forum (CDF) kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. 

Katika jukumu hilo TAMWA itaendeleza historia yake ya utetezi wa haki za binadamu kwa mrengo wa kijinsia kwa kuwahusisha wanaume na wavulana kupinga ukatili na kuhamasisha mawasiliano kuanzia ngazi ya familia, jamii, kitaifa hadi kimataifa. 

Pamoja na hilo, TAMWA imepewa jukumu la kufanya kazi pamoja na mashirika wanachama katika kujengeana uwezokuhamasisha haki, usawa,na kupambana na ukatili kijinsia.

Mtandao wa MEA una mashirika wanachama takribani 31nchini huku ukiwa na jumla ya mashirika wanachama zaidi ya 400 kutoka  Afrika, Amerika ya Kusini,Amerika ya Kaskazini, Asia na Bara la Ulaya.

Mkurugenzi Mtendaji

TAMWA

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Dar es Salaam, 8 Machi 2025. Machi 8, kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Wanawake Dunia. Siku hii huadhimishwa duniani kote ili kuukumbuka mchango, nafasi, ushiriki na changamoto zinazomkabili mwanamke na mtoto wa kike.

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) kinaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kauli mbiu ya kimataifa isemayo: ‘Chochea Mabadiliko’ na kitaifa kauli mbiu kwa mwaka huu ni: "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”

Katika maadhimisho haya TAMWA inaithamini siku hii kwani ni fursa muhimu ya kujadili hatua zilizopigwa katika kusimamia usawa wa kijinsia na kuweka mikakati ya kuharakisha mabadiliko yenye tija kwa wanawake na wasichana nchini.

Vilevile, Tanzania inaelekea kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu. Uchaguzi huu ni muhimu kwa taifa letu hasa tunapotimiza takwa hili la kidemokrasia.

Tunatoa pongezi za dhati kwa vyama vya CCM na ACT-Wazalendo ambavyo tayari vimempitisha Rais Samia Suluhu Hassan upande wa CCM na Dorothy Semu, kwa chama cha ACT-Wazalendo kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

Hii ni hatua kubwa demokrasia hapa nchini, na inaendelea kuweka hamasa kwa jamii ambayo awali ilidhaniwa wanawake hawawezi kuwa marais wala viongozi.

Hata hivyo Tanzania kama zilivyo nchi nyingine, bado kuna udhalilishaji mkubwa kwa wagombea wanawake katika vipindi vya uchaguzi. Udhalilishaji huo hufanyika majukwaani wakati wa kampeni  na kwenye mitandao ya kijamii ambao unachagiza kupungua kwa idadi ya wanawake viongozi ama ushiriki wao katika siasa na uongozi.

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wanawake, (UN-Women) zinaonyesha kuwa, mpaka kufikia Juni 2024, kulikuwa na nchi 27 tu duniani, ambako wanawake 28 ni wakuu wa nchi hizo. Takwimu hizo zinaeleza kuwa, mapengo ya kijinsia katika nafasi za juu za uongozi hayatazibwa katika miaka 130 ijayo.

Idadi ya wanawake ni 24 kati ya wabunge 264 ambayo ni sawa na asilimia 9.1 huku idadi ya wabunge wanawake wa viti maalumu ni 113 ambayo ni sawa na asilimia 29 ya wabunge wote na  jumla ya wabunge wanawake ni 141 sawa na asilimia 37 ya wabunge wote ambao ni 393.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya madiwani wanawake wa kuchaguliwa kutoka kwenye kata ni 204 ambayo ni sawa ana asilimia 3.8 ya madiwani wote huku madiwani wanawake wa viti maalumu ni 1,407 sawa na asilimia 26.2 ya madiwani wote

Hivyo basi tunapoadhimisha siku hii, na tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, TAMWA tunaomba yafuatayo:

i. Vyama vya siasa, wanasiasa na jamii, kutumia lugha ya staha wanapomzungumzia, kumuandika au kumuelezea mgombea mwanamke.

ii. Vyama vya siasa vijenge tabia ya kuwaamini na kuwapa nafasi wanawake katika majimbo ya uchaguzi ili kuongeza ushiriki wao.

iii. Wanasiasa kuacha kutumia kigezo cha talaka, sura yake, idadi ya watoto wake, umbile lake, aina ya ndoa yake, katika kampeni za uchaguzi huu na badala yake wagombea wapimwe kwa ufanisi.

iv. Jamii na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kusambaza maudhui ya utupu, udhalilishaji na lugha zisizo za staha kwa wagombea wanawake.

v. Jamii kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha sera kupinga kauli za chuki na maudhi kwa wanawake na wasichana wanaogombea nafasi za uongozi badala ya kumshambulia kwa kutumia maisha yake binafsi.

vi. Taasisi, asasi za kiraia, kukemea pale ambapo mgombea mwanamke anadhalilishwa au kutwezwa utu wake wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

vii. Wanawake wawape ushirikiano wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao na kuepuka kusambaza maudhui yanayowadhalilisha na kutweza utu wao.

vii. Vyombo vya habari, kuendelea kusimama maadili ya kihabari, ambayo yatatoa taarifa sawa kwa wagombea wote bila ubaguzi na kulenga katika sera badala ya kumshambulia mtu binafsi.

Tunapoadhimisha siku watanzania tuungane pamoja kuharakisha mabadiliko ya kuwa na jamii yenye mtazamo wa kijinsia iliyo tayari kwa maendeleo endelevu!

Dk Rose Reuben

Mkurugenzi Mtendaji-TAMWA

User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive

Novemba 25, 2024.Dar es Salaam.Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinaungana na watanzania, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali na watanzania kwa ujumla katika kuadhimisha Siku 16 za Ukatili wa Kijinsia.

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zina adhma ya kukumbusha jamii kuhusu mienendo na mitazamo inayochagiza vipigo, ukeketaji, ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni na rushwa ya ngono katika jamii. 

Kadhalika,siku hizi 16 zinatumika kutafakari kwa Pamojani wapi tulipofanikiwa, wapi penye mapengo nnikwa namna gani tutayaziba mapengo yaliyopo katika kupunguza ukatili wa kijinsia. 

Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni: Kuelekea miaka 30+ ya Beijing: Tuungane kumaliza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto

Kauli mbiu hii inalenga kuwakumbusha viongozi, wanaharakati na wadau wa masuala ya ukatili wa kijinsia hasa serikali, sekta binafsi na kampuni kuchukua hatua ili kumaliza ukatili huu.

Kama dhima ya mkutano wa Beijing, ilivyokuwa, kadhalika TAMWA kwa miaka 37 sasa kimebeba ajenda ya kumaliza ukatili wa kijinsia katika Nyanjazote, nakatika msimu huu bado kinaikumbusha jamii kuondokana na dhana potofu zote zinazomdunishakumnyima fursa , kumuharibia utu na kumwondolea staha, na wakati mwingine kusababisha ulemavu nhatakifo mwanamke na mtoto wa kike

Dhana hizo ni Pamojana mwanamke hawezi kuwa kiongozi, mtoto wa kike hana haja ya kupata elimu, ukeketaji, ubakaji na ulawiti.

Katika miaka 37 ya kufanya kazi katika eneo hili, tumeona mafanikioambayo kwa kushirikiana na serikali, tumeweza kupiga hatua na sauti zikasikika kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii,” Dr Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA.

Tumefanikiwa kupata sheria ya makosa ya kujamiiana ya SOSPA na tumefanikisha kuingizwa kwa kipengele cha rushwa ya ngono katika sheria ya rushwa. 

“Haya ni mafanikio ambayo tunajivunia katika miaka hii 37 ya uwepo wa TAMWA” Dr Rose

Hata hivyo bado kuna changamoto zinazoibuka ambazo zinachagizwa na kukua kwa teknolojia, sisi tumeona ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kijinsia kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Matumizi ya mitandao ya kijamii licha ya kuwa yameleta maendeleo lakini wanawake wamekuwa wakiathiriwa na mitandao hiyo kwa picha zao kusambazwa, au picha mjongezinazowadhalilisha zikisambazwa.

“Tumepata kesi kadhaa za Watotowa kike kutishiwa kutoa kiasi cha fedha kwa sababu wenza wao waliwarekodi picha za utuputunapokea kesi ambapo wanawake wanabakwa na kisha kupigwa picha zinazosambazwa mitandaoni,” Dr Rose 

Pamoja na hayo, kadhalika tumeona wanawake wanasiasa wakidhalilishwa mitandaoni hali inayochagiza kuacha kushiriki katika siasa au kuacha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jamii.

Hivyo basi TAMWA, katika kipindi hiki cha Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia, tunakemea udhalilishaji wa wanawake kwa kutumia mitandao ya kijamii

Tunawahimiza wanawake na Watotowa kike,wasiogope kutoa taarifa kwa mamlaka husika ikiwamo TAMWA, ambayo chini ya kitengo cha Usuluhisi wa Migogoro, (CRC) imekuwa ikisaidia wanawake/Watotowa kike wanaokumbana na udhalilishaji wa ain azote.

CRC itasikiliza kesi yako kwa hali ya faragha na kutoa msaada wa kisheria ili mwathirika apate haki yake” Dk Rose Reuben. 

TAMWA inatathmini miaka yake 37 ya harakati za kumaliza ukatili wa kijinsia katika mifumo yote na hata sasa inaendelea kuihimiza jamii kutathminimiaka 30 ya mkutano wa Beijing, kwa kuangazia nafasi ya wanawake wanasiasa, wanahabari na wanawake wote ambao wamekuwa walengwa katika ukatili wa kijinsia kwa njia ya mtandao. 

Kwa kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ina neno ‘Kuungana’ hivyo basi TAMWA tunahimiza  tuungane, wanaofanya ukatili huo wachukuliwe hatua bila kujali nafasi zao, ikiwezekana mikakati ya kitaifa ifanyike kuwasaidia wanawake na Watotowa kike wanaodhalilishwa mitandaoni

TAMWA inawaita wanawake na Watotowa kike wanaokumbana na ukatili mtandaoni na ukatili mwingine wowote, kuwasiliana kwa namba:  au kufika ofisi za TAMWA, Sinza, Mori kuanzia leo Novemba 25 hadi Desemba 10, kupata msaada wa kisheria bure. 

Mkurugenzi Mtendaji

DkRose Reuben

TAMWA

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinaungana na mashirika mbalimbali dunianikuadhimisha Siku ya Haki za Binadamuyenye kauli mbiu Haki Zetu, Mustakabali WetuHatma Yetu, NSasa” (Our Rights, Our Future, Right Now) kwa kuzingatia maadili, kujali usawa na kulinda haki za wanawake na watoto kwa maendeleo endelevu.

Katika maadhimisho hayo leo ndio kilele cha kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani yenye Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema, “Kuelekea Miaka 30+ ya Beijing: Tuungane Kumaliza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto.”

Ni umuhimu jamii kushirikiana kuimarisha maadili ya watoto na kupinga ukatili wa kijinsia, ambao bado ni changamoto kubwa hasa mauaji ya wenzakuwekeza katika ustawi wa watoto kwa mustakabali ymaendeleo ya taifa.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinazohusu makuzi ya watoto, inaonyesha kuwa watoto wanapopewa msingi mzuri wa maadili, wanakua wenye utu, heshima, na kuwa nmchango mkubwa kwa jamii. Hata hivyo, kutokana na changamoto mbalimbali za kiuchumi, teknolojiakuporomoka kwa maadili, ukatili wa kijinsia, na unyanyasaji katika jamii au familia ukuaji wa watoto katika kujiamini, ubunifu vinaathiriwa. 

Katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatii wa jinsia, TAMWA tunaendelea kuwasisitiza wazazi, walezi, walimu, na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuwajenga watoto katika misingi ya maadili, kuwafundisha kuheshimu haki za binadamu, kujua hatari za ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuripoti matukio ya ukatili wanapokabiliana nayo.

Ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni kikwazo chamaendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa kwa kuwa ndo waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia ambao unajumuisha ndoa za utotoni, ukeketaji, vipigo, ulawiti, na unyanyasaji wa kingono.

Huku tukihitimisha siku 16 za kupinga ukatili, na siku ya Haki za Binadamu, TAMWA tunasisitiza kuwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia kuendelea kukemewna wahusika wa vitendo vya kukatili kuchukuliwanahatuaza sheria ili kujenga jamii inayoheshimu haki za binadamu.

Kwa heshima ya siku hii muhimu, TAMWA inatoa wito kwa jamii nzima kushirikiana kwa dhati katika kuhakikisha kuwa watanzania wote na hasa wanawake na watoto wanalindwa dhidi ya ukatili na sauti za waathirika wa ukatili zinasikilizwa

Dkt. Rose Reuben

Mkurugenzi Mtendaji

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Oktoba 11, 2023. Dar Es Salaam.Kila ifikapo Oktoba 11, dunia huadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani. Siku hii inatukumbusha kutambua changamoto zinazowakumba watoto wa kike.

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) inatambua kwamba watoto wa kike hapa nchini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Hivyo tunapoadhimisha siku hii, hatuna budi kuziangazia ili kukumbushana kuwa mapambano yanaendelea ili kumfanya mtoto wa kike kupata haki zake katika jamii.

TAMWA katika safari yake ya miaka zaidi ya 35 ya kuhamasisha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto wa kike, imekutana na madhila mengi dhidi ya watoto wa kike na miongoni mwa hayo ni ukeketaji, mimba za utotoni, ndoa za utotoni na uminywaji wa haki za kupata elimu kwa watoto wa kike.

Lakini kadri dunia inavyobadilika ndivyo tunavyoona kuwa ili kuyaondoa hayo yote, basi suluhu la kudumu ni kuwekeza katika elimu. Ndiyo maana kauli mbiu ya mwaka huu inasema: “Wekeza katika haki za watoto wa kike: Uongozi wetu, ustawi wetu’

Kauli mbiu hii inajikita katika kuamsha hamasa kwa jamii, asasi za kiraia, serikali na watunga sera kuwekeza katika kuzitambua na kuzitekeleza haki za mtoto wa kike, na pia kutumia nafasi za uongozi kuwastawisha watoto wa kike.

Hivyo basi, TAMWA inaipongeza serikali kwa kuwekeza zaidi katika kujenga mabweni na shule za watoto wa kike, kutoa ufadhili wa masomo na kuwapa watoto wa kike kipaumbele katika nafasi za kielimu. 

Lakini bado kuna mapengo makubwa katika jamii yetu hasa ya kimtazamo kwamba watoto wa kike hawana umuhimu wa kupata elimu. 

“Na hili linakwenda sambamba na mila na tamaduni ambazo zinaamini mtoto wa kike hana haki ya kupata elimu. Hivyo wakati serikali na wadau wengine wakiwekeza katika elimu, wapo wazazi au familia zinazomtupa mtoto wa kike asipate elimu”Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk Rose Reuben

Katika kupata suluhisho la changamoto hizi, TAMWA tumefanya miradi kadhaa inayolenga kumuinua mtoto wa kike kielimu. Kwa mfano, TAMWA imefanya midahalo kadhaa na watoto wa kike, katika shule za Nambilanje na Likunja, mkoa wa Lindi, shule ya sekondari ya Mugabe, Sinza, Dar es Salaam, nia ni kusikiliza sauti zao na kujua wanachotaka. 

“Tunaposikiliza sauti zao, tunajua changamoto wanazopitia na hivyo tunajua wapi pa kuchukua hatua tunapozingatia haja zao, wasichana hawa nao wanaongeza kasi ya kutetea mabadiliko yao katika jamii wanazoishi” Dk Rose Reuben

Kwa mfano, katika mdahalo uliofanywa katika shule ya msingi Likunja, watoto wa kike walibainisha kuwa, wazazi huwaambia waandike makosa katika mitihani yao ya kumaliza darasa la saba, ili wasifaulu. 

Walimu katika shule hiyo walisema, matukio ya wazazi kuwafundisha watoto wa kike waandike ‘makorokocho’ kwenye mitihani yameongezeka baada ya serikali kujenga zaidi shule za sekondari na hivyo wanafunzi wanaofaulu kuongezeka. 

“TAMWA tunaamini katika dunia ambayo watoto wa kike wana nafasi ya kusoma na kuiwajibisha serikali, dunia ambayo watoto wa kike watakuwa viongozi katika ulimwengu wa teknolojia, tafiti na uvumbuzi. Na tunatamani mifano hii isiwe hadithi, bali mifumo yetu ya kawaida” Dk Rose Reuben

TAMWA inasisitiza jamii, hususan wazazi, kuwapa nafasi watoto wa kike na kuendelea kuwekeza katika elimu, kwani sio tu kwamba kundi hili wana uwezo kielimu lakini pia wana uwezo katika uongozi kama tunavyoona sasa Tanzania ina Rais mwanamke, ambaye ni Samia Suluhu Hassan. 

“Nafasi ya Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi, iwe chachu  na hamasa kwa jamii kuendelea kuwekeza kielimu kwa mtoto wa kike,” Dk Rose Reuben.

Mkurugenzi Mtendaji 

Dk Rose Reuben

TAMWA

Search