Jamii Forum yawapa TAMWA mafunzo ya usalama wa kimtandao
Jamii Forum yawapa TAMWA mafunzo ya usalama wa kimtandao
User Rating: 5 / 5
Chama Cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA) kimepewa mafunzo ya siku nne kwa ajili ya kujengewa uwezo kuhusu masuala ya usalama wa kimtandao ili kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kwa usalama.
Mafunzo hayo yametolewa na taasisi ya Jamii Forum Jijini Dar-es-Salaam ambayo kwa sasa inasimamia masuala ya demokrasia, utawala bora na usalama wa kimtandao.
Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Mello amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa TAMWA kwani taasisi hiyo inahitaji kuwa na ujuzi wa masuala ya usalama wa kimtandao ili kuepusha kupoteza takwimu muhimu.
Mello amesisitiza umuhimu wa mafunzo ya usalama wa kimtandao kwa kuwa dunia ya sasa imekuwa kwa kasi kiteknolojia hivyo kila wakati inapaswa kupewa mafunzo ili kuwa katika usalama zaidi.
“TAMWA na Jamii Forum tuna uhusiano wa muda mrefu na hivyo daraja hili liwe imara na tuendelee kuwasiliana na ikiwezekana muwe mabalozi wetu’’ alisema Mello
Kwa upande wake, Mkufunzi wa Mafunzo hayo, John Kaoneka ameiomba TAMWA kuboresha vifaa vyake ili viwe katika mfumo wa kisasa zaidi kwa ajili ya kuboresha mawasiliano na usalama wa takwimu na taarifa muhimu.