News/Stories

Dk Tulia aipongeza TAMWA kuzungumza na wabunge wanawake

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Sauda Msangi, TAMWA.

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)kimefanya midahalo miwili iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake na vijana namna ya kuzuia ukatili wa kijinsia, rushwa ya ngono na kuwepo kwa usawa wa kijinsia ndani ya vyombo vya habari.

Midahalo hiyo iliwalenga wanahabari na wabunge wanawake ili kuongeza idadi ya viongozi wanawake pamoja na kutengeneza mazingira salama yatakayowawezesha kufikia malego yao ya kiuongozi. Midahalo hiyo iliwashirikisha wabunge wanawake na wanahabari kutoka katika mikoa mitatu nchini.

TAMWA inatekeleza mradi wa miaka miwili wa kuwajengea uwezo wanawake na vijana katika vyumba vya habari unaofadhiliwa na International Media Support IMS.

Akizungumza wakati akifungua mdahalo wa wabunge, Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson aliipongeza TAMWA na kusem imekuja mapema, wakati ndiyo mwanzo wa miaka mitano kukiwa na mambo mengi ya kuyaweka vizuri.

“Tuna mambo mengi ya kuyaweka vizuri na wanawake wenzetu, idadi hii ya wabunge inatakiwa kuongezeka walioko katika viti maalumu waende kugombea majimboni na wengine kuingi viti maalumu, amesema Dk Tulia amesema wanawake wabunge waliochaguliwa na kuteuliwa jukumu lao sio tu kuwakilisha vyama bungeni bali pia katika kuwatumikia wananchi ili kuongeza idadi ya wanawake viongozi zaidi nchini kufikia 50/50. “

Wakati ni sasa wa kujiwekea mipango madhubuti ya kuendelea kuwa viongozi, amesema Akizungumzia hofu ya wanawake kujitokeza kuzungumza mbele ya vyombo vya habari Dk Tulia amesema ni kutokanana hofu ya jinsi watakavoandikwa na kuzungumziwa.

Kwa upande wake, Mkurungezi wa TAMWA, Rose Reuben amesema wanawake waliopata nafasi za uongozi wapange mikakati ya kuangalia kuendelea kuwepo na wengine waongezeke kwa kuonyesha wigo mpana wa uongozi, kuonyesha ujasiri na kujitokeza kuzungumzia masuala ya wanawake katika vyombo vya habari.

Reuben amesema wabunge wanawake hawajitokezi kwa wingi katika vyombo vya habari hivyo ni vyema kijitokeza na kuzungumza ikiwa ni njia mathubuti za kujiinua zaidi kisiasa na kiuongoz. Wabunge wanawake waache kuhofia vyombo vya habari kwa kuwa mkiwa bungezi mna nafasi kubwa kuzungumzia na kutilia mkazo masuala ya ukatiki wa kijinsia hivyo kupunguza unyanyasaji dhidi ya wanawake,alisema Reuben amesema TAMWA iko tayari kushirikiana na wabunge wanawake katika kuwaelimisha namna ya kuvitumia vyombo vya habari pamoja na kutumia mitandao ya kijamii.

Kadhalika ameiomba Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo iwe na Dawati la Jinsia litakalowasaidia wanahabari wanawake kupata kwa urahisi, eneo la kusemea pindi wanapokabiliwa na ukatili wa kijinsia, pia litakalowezesha masula ya kijinsia kuzungumziwa katika mikutano ya wafanyakazi.

Katika mdahalo wa waandishi wa habari, wanahabari walionyesha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuwepo wa vitendo vya rushwa ya ngono katika vyumba vya habari Wanahabari wamesema zipo sera za jinsia ndani ya vyombo vya habari hazifuatwi wala kuzungumziwa ndani ya vyumba vya habari.

Pia katika mdahalo huo wanahabari wametoa mapendekezo ya kuwepo kwa madawati ya kijinsia kwenye vyumba vya habari ili kutoa taarifa kwa uhuru iwapo vitendo vya ukatili wa kijinsia vitatokea.

Latest News and Stories

Search