News/Stories

Mkurugenzi TAMWA aonya wanafunzi na  matumizi ya mitandao ya kijamii

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Godwin Assenga, TAMWA.

Septemba 22, 2020. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben amewataka wanafunzi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuzingatia maadili.

Reuben, ameyasema hayo hivi karibuni wakati akiwakabidhi vyeti wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne wa Shule ya Filbert Bayi, jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 16 ya shule hiyo.

Akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, Reuben aliwaasa wanafunzi hao kuwa makini na matumizi ya teknolojia ikiwamo mitandao ya kijamii kwa kuzingatia maadili waliyofunzwa na walimu, wazazi ili wafikie ndoto zao.

"Mimi ni Mwanahabari, natambua kwamba sasa hivi teknolojia imekua kiasi kwamba kuna mitandao. Mitandaoni kuna mambo mazuri sana, lakini pia yapo mabaya. Mitandaoni kunaweza kukupoteza, mitandaoni kunaweza kukujenga,” amesema.

Amewaasa wanafunzi hao kuwa, pindi watakapoitumia mitandao hiyo wakumbuke kuzingatia maadili waliyofunzwa na wazazi pamoja na walimu wao.

"Sina namna ya kuwazuia kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu ndiyo dunia ya sasa, lakini itumieni mkijua kwamba mnaingia mitandaoni masikio yenu na macho yenu yakiwa wazi kwamba wewe ni mtu unaetegemewa na Taifa letu, unaetegemewa na wazazi wako" amesisitiza Reuben.

Kadhalika, amewasisitiza  wanafunzi kutumia vyema vipaji maalum walivyo navyo huku akiwakumbusha kwamba kila wanachokifanya, wakifanye katika ubora huku wakitumia vyema muda wao vizuri ili kuhakikisha wanafikia malengo na ndoto zao.

Amewapongeza wazazi kwa  kujitoa vyema kimalezi na kielimu licha ya kuwepo kwa janga la Corona, lililoathiri uchumi.

Wakati huo huo, uongozi wa shule ya Filbert Bayi, ulitoa punguzo la ada la Sh500, 000 kwa wanafunzi waliohitimu darasa la saba walioamua kuendelea na kidato cha kwanza katika shule hiyo.

Latest News and Stories

Search