News/Stories

VIRUSI VYA CORONA NA USALAMA WA WANAHABARI

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Aprili 11, 2020. Wakati huu ambapo dunia nzima inapambana na ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya Corona, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinawakumbusha wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kufuata miongozo ya kutekeleza majukumu yao kwa kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huu, na kutumia zaidi teknolojia ya mawasiliano.  Ugonjwa wa Covid-19 unaweza kumuathiri mtu yeyote, hivyo wanahabari, wamiliki wa vyombo vya habari na wadau wote wa habari wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya kiutendaji kazi yatakayowaepusha dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu. TAMWA inawashauri wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kujikita katika kutumia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano kupata habari badala ya kwenda katika mikusanyiko isiyo ya lazima kwani taarifa zinaweza kutumwa kimtandao au mahojiano kwa njia ya simu. “Bila shaka hofu ya ugonjwa wa Covid 19 itabadili mfumo wa utendaji kazi wa tasnia ya habari kama taasisi inayohudumia jamii na kuanza kujiona kuwa na wao pia ni sehemu ya jamii,” TAMWA tunathamini usalama wa wanahabari kwa kuwa sisi ni sehemu na mdau wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa chanzo cha ufikishaji wa taarifa za kutetea haki za wanawake na watoto zenye lengo la kuwa na Tanzania inayoheshimu misingi ya usawa wa jinsia.  Wanahabari wanaoripoti kuhusu COVID-19 na wanahabari wengine, wanashauriwa kufanya maandalizi kabla ya kwenda katika mikutano, kwa kufuata mbinu za kujikinga na maambukizi. 

Latest News and Stories

Search