News/Stories

Wanahabari wanawake 52 wajiunga na TAMWA

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Mwandishi Wetu, TAMWA

Dar es Salaam. Wanahabari Wanawake 52 wamefanikiwa kujiunga na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania -TAMWA mwaka huu hatua inayodhihirisha kuwa wigo wa kuripoti habari za ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia, utaendelea kupanuka.

Wanachama  hao wapya  kutoka Tanzania Bara(26) na Visiwani(26)  wamejiunga kwa ajili ya kuongeza wigo katika harakati za kuondoa mifumo yote ya ukatili wa kijinsia na kuwawezesha kitaaluma wanahabari wanawake nchini.

Akizungumzia kujiunga kwa wanahabari wapya katika chama hicho Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben amesema kujiunga kwa wanahabari hao kunaongeza jitihada za kutetea haki za wanawake na watoto zenye mrengo wa kijinsia.

“Wakati huu tunapaswa kuwa na taarifa mbalimbali zenye mrengo wa kijinsia zitakazosaidia wananchi , watunga sera na  jamii kwa ujumla  kuelewa kwamba jamii yetu inahitaji sera na taarifa za kiuchumi na kijamii.”alisema

Reuben amesema,  wanahabari ambao hawajajiunga wakati ni sasa ili kuungana pamoja katika kuinuana kitaaluma, kuungana na wanawake kutetea haki za wanawake na watoto na kuongeza wingo wa wanawake kuungana na kuwa na sauti moja.

 Amesesitiza faida za kuwa mwanachama wa TAMWA ni kupata mkopo wa kujiendeleza kitaaluma katika stashahada ya kwanza au ya pili na baadae kurudisha mkopo huo bila riba.

“Pia kuna mafunzo ya kubadilishana taaluma (exchange program) zinazopatikana nchini na hata nje ya nchi, kumuongezea uwezo wa kitaaluma kwa mafunzo yanayotolewa na TAMWA kwa wanahabari, pamoja na kuandika taarifa mbalimbali za kijamii ambazo zitaweza kumuongeza zaidi katika taaluma yake,” alisema

 Ili kupitishwa  kuwa mwanachama unatakiwa kuwa na Diploma ya Habari, uzoefu katika fani ya uanahabari usiopungua miaka mitatu na kisha kupata wadhamini watatu ambao ni wanachama wa TAMWA.

Mwanachama mpya wa TAMWA, Bupe Mwakyusa, Mwandishi wa Mlimani TV ameelezea matarajio yake baada ya kuchaguliwa kuwa mwanachama  kuwa ni pamoja na kupata uzoefu zaidi katika taaluma ya habari na kushiriki katika miradi mbalimbali ya masuala ya kijinsia.

“Kilichonishawishi zaidi kujiunga TAMWA nikiwa mwanahabari ni kujifunza zaidi kuhusu taaluma ya habari pamoja na kupata maarifa zaidi kutoka kwa waliofanikiwa katika taaluma ya habari kupitia TAMWA, pia naamini kupitia TAMWA ntafika mbali zaidi”, alisema

TAMWA ilianzishwa mwaka 1987 na wanahabari wanawake nchini na mpaka sasa kina wanachama zaidi ya 100.  

Latest News and Stories

Search