Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimethibitishwa na kutangazwa kuwa Sekretarieti mpya ya Mtandao wa Ushiriki wa Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Tanzania - MET).
TAMWA imepewa jukumu hilo baada ya kufanyiwa tathmini na Shirika la Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Afrika - MEA) mapema mwaka huu baada ya Mtandao huo nchini kuratibiwa na shirika la Child Diginity Forum (CDF) kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Katika jukumu hilo TAMWA itaendeleza historia yake ya utetezi wa haki za binadamu kwa mrengo wa kijinsia kwa kuwahusisha wanaume na wavulana kupinga ukatili na kuhamasisha mawasiliano kuanzia ngazi ya familia, jamii, kitaifa hadi kimataifa.
Pamoja na hilo, TAMWA imepewa jukumu la kufanya kazi pamoja na mashirika wanachama katika kujengeana uwezo, kuhamasisha haki, usawa,na kupambana na ukatili kijinsia.
Mtandao wa MEA una mashirika wanachama takribani 31nchini huku ukiwa na jumla ya mashirika wanachama zaidi ya 400 kutoka Afrika, Amerika ya Kusini,Amerika ya Kaskazini, Asia na Bara la Ulaya.
Mkurugenzi Mtendaji
TAMWA