Press Release

TAARIFA YA POLE KWA TAIFA

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Dar es Salaam, Novemba 5, 2025.Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinatoa pole za dhati kwa Watanzania wote waliopata madhila kwa ndugu, jamaa, Tasnia ya Habari na marafiki kutokana na vurugu zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

TAMWA inawapa pole maalum familia zote zilizopoteza wanawake, watoto, na wanahabari, sambamba na wale wote walioumia au kuathirika kwa namna yoyote kutokana na matukio hayo ya kusikitisha.

Wakati Taifa likipita katika kipindi hiki kigumu, TAMWA inaungana na Watanzania wote wanaofanya jitihada za kuijenga upya hali ya utulivu, mshikamano na amani nchini. Tunaendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda utu, kuheshimu haki za binadamu, na kudumisha mazungumzo ya amani kama nguzo ya taifa letu.

Dkt. Rose Reuben
Mkurugenzi Mtendaji.

Search