News/Stories

TAMWA YAMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA BODI

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Aprili 6, 2019. Wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA), kimemchagua Joyce Shebe kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya chama hicho.

Katika uchaguzi huo, pia wanachama waliwachagua wajumbe wa bodi ambao ni wanahabari Leah Mushi, Raziah Mwawanga na Halima Muselem kutoka Zanzibar.

Kabla ya Shebe, Alakok Mayombo alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya chama hicho aliyeongoza kuanzia 2016 mpaka mwaka huu.

Uchaguzi huo umefanyika katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Aprili 6, 2019.

“Mimi si mzungumzaji sana, mimi ni msikilizaji zaidi. Lakini ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa TAMWA ni wanachama. Sisi wanachama ndiyo tutakaoijenga TAMWA,”Joyce Shebe.

Shebe aliwataka wanahabari wanawake kuongeza ushirikiano kwa kuwa kwa kutumia kalamu zao wanaweza kuibadili au kuibomoa jamii.

Rose Reuben

Mkurugenzi Mkuu

TAMWA

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

Mobile: 0764438084

Latest News and Stories

Search